Makamu Mwenyekiti UVCCM Rehema Sombi apingana na Mwenyekiti wake, awataka vijana watumie mitandao yote ya kijamii

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
90,153
156,423
Makamu mwenyekiti wa UVCCM Taifa Rehema Sombi amewataka Vijana kuendelea kutumia mitandao ya kijamii bila kujali ni Mtandao gani

Sombi ametoa kauli hiyo mkoani Geita. Ikumbukwe mwenyekiti wa UVCCM Taifa mh Kawaida pamoja na mashehe weiomba serikali iufungie Mtandao wa X yaani twitter

Kwako Lucas pale Vwawa 😄

===========

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Rehema Sombi Akiwa Mkoani Geita amewataka vijana waendelee kuwa watumiaji wazuri wa mitandao ya kijamii haijalishi ni aina gani ya mtandao ya Kijamii wanayo tumia.

Sombi ametoa kauli hiyo wakati akifungua kambi la Vijana la umoja huo katika kijiji cha Namonge Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, amesema kipekee matumizi ya Mitandao ya Kijamii yanayotokana na sayansi na teknolojia yamehuishwa kupitia mkataba baina ya chama na wananchi.

Amesema Vijana wajikite kuelezea mafanikio ya serikali zote mbili, vilevile kujinufaisha na fursa mbalimbali za kibiashara ili kujiingizia kipato na kwamba matumizi yakiwa kinyume chake yataleta athari kwa kizazi hiki na kizazi kijacho.

Ikumbukwe kuwa Hivi karibuni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Mohamed Kawaida aliomba serikali kufungia matumizi ya Mtandao wa X (TWITTER) kutokana na kuwa na maudhui yanayokwenda kinyume na maadili ya Kitanzania.

Pia soma=> Kuelekea 2025 - UVCCM waitaka Serikali kuifungia X (zamani Tittwer)
 
Makamu mwenyekiti wa UVCCM Taifa Rehema Sombi amewataka Vijana kuendelea kutumia mitandao ya kijamii bila kujali ni Mtandao gani

Sombi ametoa kauli hiyo mkoani Geita

Source: Kitenge Tv

Ikumbukwe mwenyekiti wa UVCCM Taifa mh Kawaida pamoja na mashehe weiomba serikali iufungie Mtandao wa X yaani twitter

Kwako Lucas pale Vwawa 😄
🤣🤣🤣
 
Makamu mwenyekiti wa UVCCM Taifa Rehema Sombi amewataka Vijana kuendelea kutumia mitandao ya kijamii bila kujali ni Mtandao gani
Hukumuelewa Rehema Sombi, hakumaanisha hii mitandao ya X Insta, Facebook. Rehema alimaanisha vijana watumie tigoO na mingine.
 
Makamu mwenyekiti wa UVCCM Taifa Rehema Sombi amewataka Vijana kuendelea kutumia mitandao ya kijamii bila kujali ni Mtandao gani

Sombi ametoa kauli hiyo mkoani Geita

Source: Kitenge Tv

Ikumbukwe mwenyekiti wa UVCCM Taifa mh Kawaida pamoja na mashehe weiomba serikali iufungie Mtandao wa X yaani twitter

Kwako Lucas pale Vwawa 😄
Clinical Officer Vs Standard 7
 
Huyu Kawaida ni la 7?
Tangu ianzishwe UVCCM haijawahi kuwa na Mwenyekiti mwenye uwezo mdogo na akili ndogo kama huyu Kawaida, sijui hata alishindaje hiyo nafasi. Sijui hata alisomea nini na aliwezaje kusoma hicho alichosomea!
 
Guninita - Nchimbi - Masauni - Sadifa - James ina maana hawafikii wote hawa?
 
Back
Top Bottom