Nape: Niko tayari sasa kustaafu Uenezi

Madimbaone

Member
Feb 19, 2016
16
6
image.jpeg
Nimeikuta mahali hii!

"Kazi niliyotumwa na WanaCCM ya kuirudisha CCM madarakani Bara na Visiwani, nimeikamilisha kwa uaminifu!! Dr. Shein kaapa Rasmi kuwa Rais wa Zanzibar! Sasa niko tayari kustaafu Ukatibu Mwenezi na Itikadi wa Chama changu!! Nawashukuru wote kwa msaada wenu!!"
 
Kiungozi anaeachia madaraka pale muda wake ukifika
bila kushinikizwa ni kiongozi bora.

Hivi hii nafasi inakustaafu? Nape si bado mwanasiasa? mimi nadhani angesema anaiacha nafasi hiyo kwa mtu mwingine baada ya kufanya hayo mazuri, maana bado anaweza kuteuliwa kwa hiyo nafasi siku za mbeleni/usoni, umri bado unamruhusu.
 
Kiungozi anaeachia madaraka pale muda wake ukifika
bila kushinikizwa ni kiongozi bora.
Kwa bara letu la Africa. hii unayosema haina nafasi, inabidi ulazimishwe tu utoke....

wako wachache wanaojitambua ...lakini vyama vyao haviko Tayari kutoka madarakani..
 
Hongera Nape. Umevipiga vita vizuri vya kisiasa, kazi umeimaliza, umeilinda ccm na anguko la aibu na nafasi uliyopewa umestahili. Kama wanae Alexander the Great, sisi tuna wewe Nape the Great. Kiboko ya mafisadi, kiboko ya upinzani. Kila la heri.
 
Nimeikuta mahali hii!

"Kazi niliyotumwa na WanaCCM ya kuirudisha CCM madarakani Bara na Visiwani, nimeikamilisha kwa uaminifu!! Dr. Shein kaapa Rasmi kuwa Rais wa Zanzibar! Sasa niko tayari kustaafu Ukatibu Mwenezi na Itikadi wa Chama changu!! Nawashukuru wote kwa msaada wenu!!"
Kuirudisha au kuibakisha madarakani? kwani CCM ilishawahi kutoka madarakani? Au wakati wa uchaguzi CCM ilitoka kidogo madarakani?
 
Hongera Nape. Umevipiga vita vizuri vya kisiasa, kazi umeimaliza, umeilinda ccm na anguko la aibu na nafasi uliyopewa umestahili. Kama wanae Alexander the Great, sisi tuna wewe Nape the Great. Kiboko ya mafisadi, kiboko ya upinzani. Kila la heri.

Fungukeni vichwani mwenu jamani... Hakuna mtu ambae anajitambua ambaye anachuki na upizani.... Upizani ndio umemleta Jpm, otherwise ingekua na tafaout
 
Hongera Nape. Umevipiga vita vizuri vya kisiasa, kazi umeimaliza, umeilinda ccm na anguko la aibu na nafasi uliyopewa umestahili. Kama wanae Alexander the Great, sisi tuna wewe Nape the Great. Kiboko ya mafisadi, kiboko ya upinzani. Kila la heri.
Hapo kwenye bold, ili kuweka kumbukumbu sawa naomba ufanye hivi; weka hapa majina ya mafisadi 10 na utwambie wako chama gani?
 
Back
Top Bottom