Nape: Ni vema ‘Bunge LIVE’ likaanzia kwenye Vikao vya Kamati za Bunge ambako ndiko mambo mengi hufanyika

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,976
Waziri wa Habari mh Nape amesema uamuzi wa bunge live ama la ni wa Bunge lenyewe na siyo la Serikali hivyo yeye yuko tayari kushirikiana na Bunge kama watahitaji kuwa live.

Nape amesema tena itapendeza kama Bunge live litaanzia kwenye Kamati za Bunge ambako ndiko maamuzi karibia yote hufanyika.

Nape amesema pale kwenye ukumbi wa Bunge wanakovaa suti na tai ni mbwembwe tu lakini maamuzi huwa yameshafikiwa kwenye vikao vya kamati.

Source: Clouds 360
 
Huyu ndumila kuwili!Eti uamuzi wa Bunge live ni wa Bunge na si serikali!Mbona kipindi kile akiwa Waziri yeye ndiye aliyezuia Bunge live Kwa visingizio vya gharama na ni muda wa kazi?

Wanasiasa sio watu wakuamini kabisa,Shwain!
 
Kwani unesahau maana ya Sii hasa. Siasa inaweza kuwa nzuri ila sii hasa ni mbaya wakati wote🏃.
 
Huyu ndumila kuwili!Eti uamuzi wa Bunge live ni wa Bunge na si serikali!Mbona kipindi kile akiwa Waziri yeye ndiye aliyezuia Bunge live Kwa visingizio vya gharama na ni muda wa kazi?
Wanasiasa sio watu wakuamini kabisa,Shwain!
Kasome kanuni za bunge utaelewa.

Bunge ina studio zake na utaratibu wake wa kikanuni wa urushaji matangazo!
 
Hata wakionyesha live toka nyumbani kwa wabunge, watu wengi hawana mpango nalo. Na maamuzi ya bunge kuwa live ama la, ni ya rais aliye madarakani na sio kinyume chake. Hivyo wala asipoteze muda wake maana hakuna mtu ana muda na bunge kibogoyo.
 
Si ndio maana Nasema wanasiasa ni ndumilakuwili,sio wakuamini kabisa!

Sababu zilizotajwa na Nape(serikali) kuondoa Bunge live ni...
Ufumbuzi ni kwa Bunge kujenga Studio zake.

TBC imeokoa tsh 4 bilioni ilizokuwa inatumia kurusha bunge live!
 
Back
Top Bottom