Nape na posho za Wabunge

Nape na posho za Wabunge

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,930
Nimemuona Nnape kwenye ITV akiongelea posho za wabunge. Nashindwa kuelewa anaongelea kuhusu posho za wabunge akitumia wadhifa upi?
 
Nimemsikia Nape dakika chache zilizopita, anasema wanasiasa wanaoandika barua ndiyo wanaopeleka maneno mitaani, na kutafuta umaarufu usio na tija. Nionavyo ;Nape anazungumzia barua za Zitto zilizopo JF, inaonekana zinamkera sana. Source: ITV HABARI
 
Kauli ya Nnape kwamba CCM wanapinga kufuta posho zote akisema walimu wanapoajiliwa au kuhamishwa ni lazima wapate posho ni unafiki. Hoja kubwa nikuhadaa umma wakati lengo nikulinda posho kwa ajili ya wabunge wa chama chake wasio na uzalendo. Tangu lini ccm wakaonesha nia ya kuwajali walimu km sio matumbo yao? Nnauye alete hoja za maana kama ana lengo la kuyaokoa magamba. Zitto, Mbowe endeleeni kuwadhoofisha Magamba.
 
Na posho wanazolipwa walimu ni za kujikimu ambazo hazipingwi "per diems" zinazolipwa kulingana na sheria na kanuni za utumishi kuwa mtumishi yeyote anayeajiliwa kwa mara ya kwanza analipwa posho za kujikimu kwa siku kulingana na daraja lake, zinazopingwa ni posho za vikao yaani "sitting allowance"!!
 
Nape ni mchumia tumbo alipiga kelele sana za mafisadi alipokuwa anautaka ubunge wa Ubungo alipopewa ukuu wa wilaya sijui huko Ntwara sijui wapi na hako ka cheo huko Magamba sasa anatia kamata mafisadi men kimya kimya. jamaa hana lolote ni yale yale ya uendelezo wa mambo ya UKOO ktk Magamba. Walimu nao nawashangaa sana tuu miaka yote hii wanaonewa lkn hawashtuki tuu aaaaaaargh wataendelea kuonewa tu hivyo hivyo tu km hawatachagua MABADILIKO!
 
CCeM imekamatwa iwezi tena kuisha habari yake, ngoja tusubiri , wakiamua kuunga hoja posho ziendelee kulipwa tunarudi kwa wananchi hapo hawatoki ,kama ni nyoka ametandikwa kiwiliwili awezi tena kwenda popote, Nape ameishiwa yaani yeye kila hoja ni kudandia tu !
 
Kama wameweza kutoa barua za Zitto hadharani then tutawaona wakichukua mic Jumanne kupigania sh. 150,000 kwa siku public. Tunataka barua zao tuzione pia...

"Ignorance, selfishness, corruptions and ccm ni kitu kimoja
"
 
Tukiwa tunaanzisha thread, tuwe makini na headings zetu.
Ni ushauri tu.
 
Mi mwenyewe nimemuona lakini cjamuelewa maana anaongelea tena hela ya kujikimu kwa ajili ya walimu,anashindwa kuweka wazi kwamba wabunge waschukue posho maana vikao ni moja ya kazi zao!!!
 
Hii inadhitibisha kuwa CDM ni chama Kiongozi. Uamuzi wa Zito umeasha mjadala wa kitaifa na kuongeza 'visibility' yao kuliko CCM. Na wananchi wa kawaida wanaona kuwa matendo ya CDM yana nia nzuri ya kupunguza matumizi ya serikali na kuongeza fedha za maendeleo.
 
Nasikia pia amemuandikia katibu mkuu wa CDM ampunguzie posho yake kwa kuwa ni kubwa sana. Zitto sasa anapoelekea kubaya.
 
Back
Top Bottom