Nape na Kinana wamshitaki JK kwa wananchi

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,765
Reaction score
29,207
Kwa kuwa JK ameaumua kuziba nta masikioni na kupuuzilia mbali matatizo wanayoyapata wananchi kutokana na mawaziri mizigo, ninawashauri Nape na Kinana warudi kwa wananchi ‘wakamshitaki' kwa kushindwa kusikia kilio chao-kilichofikishwa kwake kufuatia ziara ktk mikoa ya kusini na nyanda za juu kusini. Wakifanya hivyo, watakuwa wamejiondolea lawana pindi wananchi watakapoamua kukitosa chama chao mwaka 2015.

Kuliko ikaonekana kwamba JK, Nape na Kinana lao ni moja, ni heri hawa mabwana wawili wakajitenga na JK na kuegemea upande wa wananchi ili kuepuka kuhukumiwa kwa pamoja. Wananchi ndio wanaotaabika na ugumu wa maisha kwa kubebeshwa mizigo ya mawaziri wasiobebeka na ambao JK ameamua waendelee kuwaelemea wananchi.

Litakuwa ni jambo la busara na hekima endapo Kinana na Nape watarejea kwa wananchi na kuwaambia kinagaubaga juu ya namna JK anavyofanya maisha kuwa magumu kwa kupuuzia kilio cha wananchi. Endapo hawa wawili hawatasoma alama za nyakati na kurejea kwa wananchi haraka kuwapa mrejesho wa kilio cha kwa JK, hali ya chama itakuwa mbaya sana mwaka 2015 kwani wananchi (waliokwisha kata tamaa) watakiweka katika wakati mgumu chama na hatimaye kuking'oa madarakani.

Yawezekana JK hajali kwa kuwa mwaka 2015 atamaliza ngwe yake ya uongozi lakini anapaswa kufahamu kwamba anawaharibia makada wenzake na kuwaweka katika wakati mgumu wakati watakporejea kwa wananchi kuomba ridhaa yao ya kuendelea kuongoza. Kwa jinsi hali ilivyo ni kwamba hata bwana mkubwa ameishakata tamaa na ameamua kwamba na ‘liwalo liwe'. Ukaidi wake wa kutozingatia kilio na matatizo ya walalahoi utakipeleka chama chake kuzimu punde si punde. Tatizo ni kwamba huyu bwana mkubwa akili za kuambiwa, huwa hachanganyi na za kwake. Madhara ya kutochanganya akili yatasababisha lawama ambazo zitakuja kumrudia yeye na atakosa mahali pa kuuficha uso wake.:israel:
 
Huwajui au HUWAFAHAMU wana siasa wewe.....

Those that smoke marijuana, Wanna thank you father ......

Politicians thank you father, For making them to be able
To lie with a straight face, While the nation cries
They wanna thank you lord
 
Last edited by a moderator:
Tangu slaa aruhusu gongo imekuwa ni shida kweli vijana wanazidi kuharibika kwa kiasi kikubwa sana.
 
Huyu naye eti ni miongoni mwa watu wenye jukumu la kuishauri chadema hii kweli balaa.
 
ccm hawa uwezo wa.kufanya maamuzi ya kinana wanalindana hawa mafisadi wakubwa kiama cha ccm 2015 chadema ndo mkombozi wao ccm ni maiti inayosubiri kuzikwa 2015
 
Kwa kuwa JK ameaumua kuziba nta masikioni na kupuuzilia mbali matatizo wanayoyapata wananchi kutokana na mawaziri mizigo, ninawashauri Nape na Kinana warudi kwa wananchi ‘wakamshitaki' kwa kushindwa kusikia kilio chao-kilichofikishwa kwake kufuatia ziara ktk mikoa ya kusini na nyanda za juu kusini. Wakifanya hivyo, watakuwa wamejiondolea lawana pindi wananchi watakapoamua kukitosa chama chao mwaka 2015.

Kuliko ikaonekana kwamba JK, Nape na Kinana lao ni moja, ni heri hawa mabwana wawili wakajitenga na JK na kuegemea upande wa wananchi ili kuepuka kuhukumiwa kwa pamoja. Wananchi ndio wanaotaabika na ugumu wa maisha kwa kubebeshwa mizigo ya mawaziri wasiobebeka na ambao JK ameamua waendelee kuwaelemea wananchi.

Litakuwa ni jambo la busara na hekima endapo Kinana na Nape watarejea kwa wananchi na kuwaambia kinagaubaga juu ya namna JK anavyofanya maisha kuwa magumu kwa kupuuzia kilio cha wananchi. Endapo hawa wawili hawatasoma alama za nyakati na kurejea kwa wananchi haraka kuwapa mrejesho wa kilio cha kwa JK, hali ya chama itakuwa mbaya sana mwaka 2015 kwani wananchi (waliokwisha kata tamaa) watakiweka katika wakati mgumu chama na hatimaye kuking'oa madarakani.

Yawezekana JK hajali kwa kuwa mwaka 2015 atamaliza ngwe yake ya uongozi lakini anapaswa kufahamu kwamba anawaharibia makada wenzake na kuwaweka katika wakati mgumu wakati watakporejea kwa wananchi kuomba ridhaa yao ya kuendelea kuongoza. Kwa jinsi hali ilivyo ni kwamba hata bwana mkubwa ameishakata tamaa na ameamua kwamba na ‘liwalo liwe'. Ukaidi wake wa kutozingatia kilio na matatizo ya walalahoi utakipeleka chama chake kuzimu punde si punde. Tatizo ni kwamba huyu bwana mkubwa akili za kuambiwa, huwa hachanganyi na za kwake. Madhara ya kutochanganya akili yatasababisha lawama ambazo zitakuja kumrudia yeye na atakosa mahali pa kuuficha uso wake.:israel:

Mie siamini kabisa kama kweli ujumbe ulimfikia, kumbuka mambo ya magazeti ya kibongo, naamini labda magazeti yetu na vyombo vya habari vilimnuu vibaya Mh. Kinana na Nape si unajua tena elimu zetu za shule za kata tena zilivyo. Halafu kumbukeni Mh. sasa anamaliza muda wake inabidi asiwe na maadui wengi zaidi ili apate angalau watu wa kumtembelea na kumshukuru katika enzi za ungozi wake. Jamani kama tumevumilia miaka minane sasa hii iliyobaki mbona tutapata tu maisha bora kwa kila Mtanzania.

Msisahau awamu ya tatu walichaguliwa MAWAZIRI WAKAITWA MAASKARI WA MIAMVULI, Sasa hawa nao pengine ndi Makomandoo kabisa......
 
Nape na Kinana ndio mizigo ndani ya CCM. Hata JK ameliona hilo, ndio maana kadharau hoja zao!
 
Issu ni too complicated kwa CCM..ni km unakimbia kutoka nje ya tannel ukiwa umebeba mabomu ya kurusha kwa mkono halafu moja mabomu kadhaa yanadondoka na kuselleka kueleke mlangoni..mara hayajalipuka na haupo sure km unaweza kwenda pita pale kabla halijalipuka...na ukipabki km utabaki..

CCM in no waya hawana tena njia..
 
Mtake mstake mtatawaliwa na ccm tu mpaka mwisho wa dunia kidumu ccm
 
Issu ni too complicated kwa CCM..ni km unakimbia kutoka nje ya tannel ukiwa umebeba mabomu ya kurusha kwa mkono halafu moja mabomu kadhaa yanadondoka na kuselleka kueleke mlangoni..mara hayajalipuka na haupo sure km unaweza kwenda pita pale kabla halijalipuka...na ukipabki km utabaki..

CCM in no waya hawana tena njia..
 
mie siamini kabisa kama kweli ujumbe ulimfikia, kumbuka mambo ya magazeti ya kibongo, naamini labda magazeti yetu na vyombo vya habari vilimnuu vibaya mh. Kinana na nape si unajua tena elimu zetu za shule za kata tena zilivyo. Halafu kumbukeni mh. Sasa anamaliza muda wake inabidi asiwe na maadui wengi zaidi ili apate angalau watu wa kumtembelea na kumshukuru katika enzi za ungozi wake. Jamani kama tumevumilia miaka minane sasa hii iliyobaki mbona tutapata tu maisha bora kwa kila mtanzania.

Msisahau awamu ya tatu walichaguliwa mawaziri wakaitwa maaskari wa miamvuli, sasa hawa nao pengine ndi makomandoo kabisa......
nilsimkia nape akitoa povu uwanja wa barafu rujewa kuhusu mawaziri mizigo sijui ataficha wapi uso wake mbele ya hao wazee. Nafikiri ni vizuri akajiuzulu au wakti mwingine ni vizuri kauli zake akawasilisha kwa mweneyekti kabla ya kutumia ugali wa wananchi kupayuka maneneo ambayo hana hakika nayo
 
Kwa hiyo Slaa ana mamlaka ya kuruhu na kuzuia bidhaa flani hapa nchini? Basi huyu ,mtu atakuwa ana madaraka makubwa kuliko Kikwete
Tangu slaa aruhusu gongo imekuwa ni shida kweli vijana wanazidi kuharibika kwa kiasi kikubwa sana.
 
Nape alianza uvuvuzela wa kung'oa Magamba akashindwa, kaimba wimbo wa mawaziri mizigo kashindwa tena, ni bora akajiunga na chama chake cha CCJ na kuzunguka kueleza mabaya ya maccm au apewe sara ya toba kabla ya kujiunga na CDM.
 
Back
Top Bottom