Nape: Magamba kuvuliwa baada ya uchaguzi wa Igunga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape: Magamba kuvuliwa baada ya uchaguzi wa Igunga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gambo Mrisho, Sep 26, 2011.

 1. G

  Gambo Mrisho New Member

  #1
  Sep 26, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Frederick Katulanda, Mwanza

  KATIBU Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, amesisitiza kuwa adhima ya chama chake kuendelea na mpango wake wa kujivua magamba, bado iko palepale ila kinasubiri kumalizika kwa uchaguzi wa Igunga.

  Akizungumza mjini Mwanza juzi, Nape alisema katika kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Dodoma Julai 31, mwaka huu, hatma ya makada wa CCM ambao walitakiwa kujivua gamba, ilielezwa kuwa itajulikana kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya chama kilichotarajiwa kufanyika Septemba.

  Nape alisema ingawa Septemba imefika, kikao hakijafanyika hivyo msimamo wa chama uko palepale kwa vile wanaopaswa kujivua magamba walishaelezewa kupima na kuamua wenyewe.

  “Jamani hili suala la kujivua gamba, siyo langu ni msimamo wa chama, tuliposema Septemba tulikuwa tukimaanisha kikao kitafanyika muda huo, lakini sasa katika busara ya kawaida huwezi kuwa na kikao huku kuna maafa na uchaguzi,” alisema.

  Alisema katika kikao kilichopita walijadili jambo hilo na kwamba, litajulikana hatma yake kikao kijacho Septemba, lakini wakati huo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), ilikuwa haijatangaza tarehe ya uchaguzi wa Igunga na kubainisha kuwa, adhima ya chaka bado ipo palepale kwa vile kikao hicho cha Septemba hakijafanyika.

  “Kikao kijacho tutamalizana nao hawa, tatizo ni kuwa watu wanataka tufanye haraka wanavyotaka wao, jamani uamuzi wa kikao kimoja unatoka na kwenda kikao kingine, hatujafanya kikao na kikifika tutajadili jambo hilo kwani litakuwa katika ajenda ya yatokanayo na kikao kilichopita,” alisisitiza Nape.

  Alisema wanapozungumzia kujivua gamba wanakuwa wamehusisha mpango wa chama kujifanyia mabadiliko katika mambo mengi na kueleza kuwa, hiyo siyo mara ya kwanza kwa CCM kufanya mabadiliko, huku akieleza yaliyofanyika tangu enzi za chama cha Taa, Tanu na mpaka kuzaliwa CCM.

  “Haya mabadiliko ni ya kila wakati kwa chama toka enzi za Taa, mabadiliko yalifanyika kukazaliwa Tanu ambayo iliunda azimio la Arusha, kisha tukaunganisha vyama ikazaliwa CCM, chama chetu kimepitia mabadiliko na kila baada ya miaka kumi kumekuwa na mabadiliko,” alisema.
   
 2. K

  Keil JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2011
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ninasikitika kusema kwamba huo mkakati umeishakwama tayari. Hayo magamba yameishapewa hoja na Kamati Kuu na hivyo hawawezi kuyavua kwa nguvu na ndio maana akina Lowassa na Chenge wamekaa kimya hasa baada ya upuuzi huu tunaouona unaendelea.

  Kama Rostam alikuwa amesababisha CCM ikapoteza mvuto, ilikuwaje akaombwa aende kumpigia debe mgombea wa CCM? Hivi kweli mtu aliyesababisha chama kionekane kibaya, utamwita au utamwalika aje kukusaidia kupiga debe? Hilo pekee litawaangusha kwenye mjadala wa NEC na hakuna gamba ambalo litavuliwa.
   
 3. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nadharia ya kujivua magamba ilishashindwa hivyo kumuuliza Nape suala hilo ni ujinga kwani CCM haitakuwa tayari tena kuvua gamba kutokana na inayoyaona huko Igunga.
   
 4. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Haka kajamaa kanafiki sana, jana kamejamba hapa Mugumu na kukiharibia chama chake kila kitu. Akili ndogo sana.
   
 5. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  hivi nape umeshakabidhi ofisi yetu ya wilaya au bado?unasubili nini?mia
   
 6. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Chenge alishasema kuwa gamba kimekwama kiunoni kwahiyo halivuliki!!
   
 7. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  yani Chenge ana masaburi makubwa, gamba limegomea kiunoni, Nape aende kwenye kiuno cha Chenge sasa akalivue!!
   
 8. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kitu gani kinamzuia kuyaeleza haya kwenye kampeni Igunga ?
   
 9. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Na ukitokea uchaguzi mwingine mdogo wanahirisha? huu ndio usanii wenyewe!
   
 10. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Siasa Uchwala . RA
   
 11. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nape hana jipya anatapa tapa tu.
   
 12. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani RA kwei kidume wa CCM, amejivua gamba akawakashifu akina Nape, Chiligati na wengineo na kuweka mkwala kwamba kama kweli mna ubavu nendeni Igunga peke yenu muone!!!!!! Jamaa wakajifanya hawakusikia mwisho waka-bow, RA akaitwa kwenye ufunguzi wa kampeni baada ya hapo akawaacha solemba. Nape, Sitta, Mwakyembe, Kilango wakapigwa marufuku kwenda Igunga,Stori za gamba zikasizi, mkutano mkuu wa chama ukaahisrishwa aliyeitwa gamba leo wanaCCM wanawambia wananchi Igunga mchagueni Kafumu aendeleze yale ya Rostam.

  Nani kama RA hahahaha ahahaha ahahah!!!!!!!!!!
   
 13. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,787
  Likes Received: 36,792
  Trophy Points: 280
  Kwa nini anaongea na waandishi wa habari mwanza na sio igunga.
   
 14. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Uwezo wake wakufikiri unadidimia lakini tumbo lake linaongezeka! Kazi kwelikweli.
   
 15. P

  Peter lilayon Member

  #15
  Sep 27, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Me nataka nape aendelee kumvua gamba na El hata lifikie shingoni kama anaweza mana la chenge limeishia kiunoni na bahati yake kupata mkoa mpya simiyu
   
 16. moblaze

  moblaze JF-Expert Member

  #16
  Sep 27, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  nape doesn't deserve 2 be a politicians..ni basi tu Sir name ndio inamweka mjini!
  Hana upeo wa kuona mbali zaidi ya tumbo lake na kujichubua, sorry bro, anza wewe kujivua gamba coz ndio unakizika chama..
   
 17. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mkuu una ushahidi kwamba Rostam aliwahi kuombwa kufanya hivyo?mbona walioombwa wote kina mkapa,mangula,aden rage na wakuu wa wilaya kadhaa waliowahi kufanya kazi igunga n.k.walipewa barua na kutangazwa hadharani na kampeni wanazifanyia hadharani mchana kweupe kila mtu anawaona,sasa iweje huyu aombewe chumbani kwake na kampeni azifanyie huko huko chumbani kwake?
   
 18. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #18
  Sep 27, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  ccm kitajua umuhimu wa NAPE baada ya kulikosa jimbo la Igunga...
   
 19. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #19
  Sep 27, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye list ya Nape,Sitta,mwakyembe umemsahau na LOWASSA pia nae alipigwa marufuku asikanyage igunga pia mbona hii hamuisemi?
   
 20. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #20
  Sep 27, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160


  Mkuu, kadri jf inavyopanda chati, documentation imekuwa ni tatizo. Ccm wangemwalika RA kwa barua, kesho yake ungeikuta hapa! Ukweli unabaki palepale, ccm si tu imemwomba, bali imemwangukia kabisa RA ahudhurie kampeni yao. Licha ya kuwaponda kwa siasa uchwara na kuwalaumu swala la kujivua gamba, bado amekubali kuwapigia kampeni! Ni kama mwanamke uliyezaa nae mkakorofishana. Ukimwangukia anasahau yote kwa kisingizio cha watoto. Upuuzi mtupu!!?
   
Loading...