Nape: Lowassa ameanza kufanya kampeni, yuko hatarini kuenguliwa

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,913
Reaction score
3,242
Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema kitendo cha mgombea mmoja anayepokea makundi ya watu ili wamshawishi kupiga kura huko Dodoma ni kuanza kampeni na yuko hatarini kuenguliwa.

Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa ndiye anayepokea makundi ya watu wakiwemo masheikh, maaskofu na wanafunzi wakimshawishi kugombea.

Akizungumza na radio VOA, Nape alisema: "Labda niweke vizuri hili, mtu yoyote anayekiuka kanuni hatapitishwa labda kamaa anakwenda kugombea kwa chama kingine.

"Kinachofanyika Dodoma cha watu kuchukuliwa na magari huku wengine wakiwa hawajui, halafu wakifika wanakuta viti vimeshapangwa na vyakula;halafu eti wanamshawishi kugombea, ni kukiuka kanuni na anaweza kuondolewa," alisema Nape.

 
anachokosea lowasa ni timing,,angesubiri mda mwafaka na afanye anachofanya sasa angefaulu.
 
Nnatumai Nape anao ushahidi wa anayoyasema na kutuhumu watu. Kwamba watu wanaoenda dodoma wamelipwa na nani, kwa njia zipi na kwa sababu gani, la sivyo atakiaibisha chama kwa mara nyengine tena! Wananchi wameamua....acheni uzushi na uongo. Kwa nini mnawadhalilisha wananchi kiasi hiki? Waache kazi zao kwa kulipwa na kupewa chakula? Hivi wote walioonekana huko hawawezi kujinunulia chakula? Tena tunawaingiza mpaka viongozi wetu wa dini; maimamu na wachungaji!

Nnaungana na mtu wa Mungu mmoja aliyemtaka aokoke.....atubu na aokoke!!
 
Wamevujisha siri.Jina la El halitakuwepo ktk list ya CCM.
Yeye ni waziri mkuu mtarajiwa tu
 
Navyomjua jk hataki kupiga kelele na Lowasa anamsubiri kwenye kanuni dakika za mwisho amtandike hataamini masikio na macho yake.

Ni kweli mkwere anaweza kukuuwa huku anatabasamu lakini cha kujiuliza huyu mzee mamvi hayajui yote hayo? Je hamjui rafikiye? Je haogopi kuenguliwa? Au hiki kibri anakipata wapi maana kapewa onyo lakini hajali what is he up to?
 
Ki ukweli hata mimi nashindwa kuelewa, wagombea ambao wako ccm ni wengi mno ambao wamesimamishwa na wananguvu ya kumudu kufuturisha kipindi hiki cha kwaresma kama bwana edo anavyofanya ila kutokana na kanuni za chama, wameamaua kutulia. Mimi nashindwa kuelewa kitu gani kinamsumbua huyu mzee, nadhani atulie tu
 
Nashangaa sumu wanawekewa watu wasiokua na mvuto,hii ndo subject ambayo ni threat kwa Taifa
 
heeh! kumbe wanafunzi wa UDOM walichoka kula kwa wajas wakaona wabadilishe menu kwa naniliu! njaa mbaya!

Jenga hoja zenye mshiko.Acha kudhihaki watu.Umewaona Udom tu?,mipango;St John na CBE nao walienda kumshawishi EL kama Jk alivyoagiza akiwa Songea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…