Nape live on Star tv: Anazungumzia uchaguzi wa CCM

Katibu mwenezi wa CCM Nape Nnauye yuko live Star tv anadadavua kwa makini taratibu za uchaguzi ndani ya CCM.

Yeye amechukua fomu?Nafikiri uchaguzi unaweza kuwa njia nzuri ya kuona kama kweli anakubalika kuliko kuteuliwa na Mtu mmoja kwa matakwa yake mwenyewe.
 
Hapa ndio watakapo mwagana kama ilivyokuwa kwa ubunge! CCM wangejua wasingeitisha ata uchaguzi huo kwani ndio utakuwa shimo lao
 
Amesema wanajipanga kwa umakini wasije kuanguka 2014 & 2015 halafu wawe wapiga kelele!!!

Kuna mchangiaji mmoja (Ruhuza) kamtahadharisha wajitahidi kurudisha vijana chamani maana kiuhalisia asilimia kubwa sana wamekimbilia CDM.....jambo ambalo mwenzake (katibu wa ccm Kinondoni) kalipinga kwa nguvu akidai yeye anafahamu hali halisi mitaani kwamba vijana karibu wote bado ni ccm!!! Maajabu ccm hayaishi

''......hali halisi mitaani kwamba vijana wote bado ni CCM!''.
Mhh,haya ngoja tuone mwisho. Maana kama ni usingizi ni wa pono. Wake up man, times have changed. Vijana wanajua wanataka nn, hizi sweeping statements mwisho wa cku zitawa-cost.
 
Nilikuwa na baba yake Nape kwenye vita ya kagera. Baba yake yaani mzee moses nnauye alikuwa muadilifu na mzalendo wa kweli kwa nchi yake. Nashangaa mwanaye anakosa uzalendo na nchi yake. Mara nyingi "anaropoka" siyo kuongea na audience.Nina kushauri nape ww ni "public relations officer wa CCM", jipange katika kila kitu unachoongea. Watanzania wa sasa wanapima kila kitu au neno linaloongewa na mwana siasa. Kumbuka tupo kwenye mfumo wa vyama vingi. Hayo "maujinga" yako ungeyafanya enzi za chama kimoja ilikuwa haina shida. Take care usije haribu chama cha watu hukuwepo kilipo kuwa kina anzishwa
 
Back
Top Bottom