Nape hukuzaliwa kuwa waziri

Mpunilevel

JF-Expert Member
Sep 14, 2015
3,140
1,871
Jana nimekusikiliza kwa makini sana ufafanuzi wako juu ya yaliyotokea siku chache zilizopita.
Umezungumzia kuvamiwa kwa Mawingu TV, kutekwa kwa Roma Mkatoliki, kupotea kwa Ben Saanane.

Pia umemshauri Rais Magufuli hatua za kuchukua, Jambo jema.

Nikukumbushe Nape, utekaji nchi hii haujaanza Leo, matukio haya yapo nchini sema vyombo vyetu vya habari haviyapi umuhimu kama vilivyofanya kwenye tukio la Mawingu Fm na kutekwa kwa Roma Mkatoliki. Na yamehusishwa na Siasa moja kwa moja, sababu naamini unazijua.

Siku za nyuma viongozi wa kisiasa wa CCM na Chadema baadhi wameuwawa kwa kupigwa risasi,mfano hivi karibuni kiongozi wa CCM Rufiji ameuwawa kwa kupigwa risasi, Sikusikia Kauri yako juu ya hili tukio.

Unapofanya Siasa ujue ina gharama zake.
Hukuwahi kujitokeza hadharani kupinga uovu huu Mpaka ulipotemwa baraza la la mawaziri.
Huo ushujaa wako unatoka wapi?
Hujawahi ongerea kuhusu Ben, Jana Ndo nmekusikia, hasira za Nini?

Aliyekupa uwaziri ndie aliyempa Makonda URC.
Bifu lako na Makonda kuhusu vita dhidi ya Dawa za kulevya imekugharimu na si vinginevyo.
Nazi haiwezi shindana na Jiwe hata siku moja.
Kuwa mpole, elekeza nguvu zako kwa wapiga kura wako ili uwapatie maendeleo.
Hukuzaliwa kuwa waziri, waliopo nyuma yako hawakutakii mwisho mwema, ushauri wao kwako ni Wewe upotee kwenye mizania ya Siasa.

Wanamachungu na Kauri ulizozitoa mwaka 2015 wakati wa kampeni.

Kuthibitisha hili, rejea kauli ya Tundu Lissu, alisema Nape si shujaa bali anavuna alichopanda.
Namalizia tena kusema Nazi haiwezi shindana na Jiwe. Wengi walijaribu lakini walishindwa.
 
Amechemsha sana..eti watu wanaogopa kwenda kazini sababu wanatekwa..hivi kuna kipindi watu walitekwa na kuuawa kama kipindi cha jk..?? Mbona sasa nchi IPO salama na imetulia..hata harakati za kidini hatuzisikii tena..
Tujikumbushe matukio;
1. Said Kubenea kumwagiwa tindikali
2. Ndimara Tegambwage wa mwanahalisi kupigwa mapanga
3. Kiongozi wa mgomo wa madr kutekwa
4. Mauaji ya wafanyabiashara wa mahenge.
5. Kuuawa kwa Mwangosi.
6. Kuuawa kwa profesa Mwakyusa
7. Kuuawa kwa dr Mvungi
8. Kuwekwa ndani sheikh Ponda.
9. Kuvamiwa Absalom Kibanda
Nakumbuka awamu iliyopita ndipo umaarufu wa msitu wa mabwepande ulishamiri..
Huyo Nape alikuwa kisiwa gani wakati yanatokea hayo??
 
Nape kuwa makini sana na hawa wanaokukuza sasa, wewe ni target nzuri sana kwa kutekwa hata kuuliwa ili tu kumchafua Magu, watu wana njaa ya ikulu na wako radhi kufanya chochote ili watimize matakwa yao, Chacha Wangwe alitolewa kafara, wewe ni zaidi ya Ng'ombe uliyenona kwa kafara ili kumchafua Magu, mwenye masikio na asikie.
 
Amechemsha sana..eti watu wanaogopa kwenda kazini sababu wanatekwa..hivi kuna kipindi watu walitekwa na kuuawa kama kipindi cha jk..?? Mbona sasa nchi IPO salama na imetulia..hata harakati za kidini hatuzisikii tena..
Tujikumbushe matukio;
1. Said Kubenea kumwagiwa tindikali
2. Ndimara Tegambwage wa mwanahalisi kupigwa mapanga
3. Kiongozi wa mgomo wa madr kuuawa
4. Mauaji ya wafanyabiashara wa mahenge.
5. Kuuawa kwa Mwangosi.
6. Kuuawa kwa profesa Mwakyusa
7. Kuuawa kwa dr Mvungi
8. Kuwekwa ndani sheikh Ponda.
9. Kuvamiwa Absalom Kibanda
Nakumbuka awamu iliyopita ndipo umaarufu wa msitu wa mabwepande ulishamiri..
Huyo Nape alikuwa kisiwa gani wakati yanatokea hayo??
Nape anaweza kuwa Sauli yule wa kwenye Biblia aliyekuja kugeuka kuwa Mtume Paulo na kupambana na maovu kwa nguvu zote ingawa awali alikuwa mtenda maovu, muuaji na mpinga kristo.
Binadamu anaweza kuwa ndani ya maovu sana kama alivyokuwa Nape ndani ya kundi la ccm lenye uovu wa kila aina. Lakini kudra za mwenyezi zaweza kumuangukia akautambua uovu aliokuwa anautenda na akajiunga na wakemeaji wa uovu akajikuta anafanya kazi inayo mpendeza Mungu. Karibu sana Nape sema yote na ukweli utakuweka huru.
 
Yote hiyo kisa kumpigania Wema Sepetu, hizi nyingine ni sideshows tu, tatizo hasa na uchungu upo hapo kwa Wema.
 
Yote hiyo kisa kumpigania Wema Sepetu, hizi nyingine ni sideshows tu, tatizo hasa na uchungu upo hapo kwa Wema.
Hizo ni fikra za kitoto ungepeleka kwa watoto wenzako. Weka ushahidi wa kina kuhusu kauli zako ili GT wazijadili na kuona ukweli wako tusifanye hapa kama kijiwe cha kahawa.
 
Dah.... Kaka hao wanazidi kukunenepesha kesho wakugeuze mbuzi....tena utakuwa Mbuzi mtamu kweli kwa maneno unayoyatamka.... Wanaitaka Ile nyumba kwa namna yoyote.... hata hatujui lengo lao ni nini.... Wengi Wanajichanganya kati UJASIRI na UZEMBE...... Shtuka kaka
 
Hizo ni fikra za kitoto ungepeleka kwa watoto wenzako. Weka ushahidi wa kina kuhusu kauli zako ili GT wazijadili na kuona ukweli wako tusifanye hapa kama kijiwe cha kahawa.
Vita ya Nape na Makonda imeanzia kwa Wema, Nape aliumia sana Wema kutajwa kwa madawa ya kulevya, alitaka Wema wamsitiri kwa kuwa ni "mtu wao". Hizi nyingine zote ni sideshows tu, chochote Wema alichompa Nape si haba, kina thamani kubwa sana.
 
Nape kachoshwa na udikteta. Nampongeza kwa kuthubutu kutoa ushauri kwa rafiki yake na Kagame at the midday.
 
Ukiona watu wanatumwa kumshambulia Nape juwa fika kawashika pabaya
CCM bado inamuhitaji Nape kuliko Nape anavyoihitaji CCM
 
Back
Top Bottom