Kishindo cha mashairi ya Roma Mkatoliki kwenye wimbo 'Tundu Lissu Shujaa''

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980

Roma Mkatoliki ameshusha mzigo mpya YouTube. Moja ya mistari katika wimbo wake mpya Ni "wakati wa JK tulipinga sana ila hatukupigwa risasi wala kutekwa"....."Nani alijua Tundulisu atapona?"

Huu wimbo unakuja kipindi ambacho Chama cha Mapinduzi kimeapa kutotumia wasanii katika shughuli za siasa huku kikitumia wakata mitama mia tano jukwaani Uhuru Stadium kwa lengo la kupata wakata mitama wachache watakaotumika kwenye kampani.

Dhana ya kampeni na wakata mitama ilizinduliwa rasmi mbele ya Waziri mkuu na kijana anayedhani yeye ana uhai special na nchi hii kisa tu baba yake alimkabidhi kwa watawala wamlelee. Kijana huyu kwake dhuluma (bao la mkono) ni heshima, kwake yeye ukimpinga anaona unatakiwa kupigwa , kwake yeye ccm ni Bora kuliko Tanzania.

Niwakumbushe tu kuwa wimbo mmoja wa msanii anayezungumzia haki, democracy na usawa ni zaidi ya nyimbo miatano za watu wanaomtukuza binadamu ambaye ajakamilika na atokaa akamilike.

"Wakati wa JK tulipinga ila hatukupigwa risasi wala kutekwa."
 
Siku zote ukweli humuweka mtu huru. Na msanii akiwa kama kioo mbele ya jamii, anapaswa kuzingatia na kuuishi ukweli huu hasa kutokana na mazingira ya sasa ya kisiasa hapa nchini.

Wasanii ni vyema wakaepuka kutumbukiza nyongo kwenye vitumbua vyao, kwa kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi kupita. Soko la kazi zao halipaswi kufungamana na ushabiki wa wazi wa itikadi za kisiasa. Kwa muonekano wa matendo yao ya sasa ya kiushabiki, itakuja kuwaghalimu na kupelekea kupoteza mashabiki wengi wa kazi zao.
 
Kweli kabisa!
Lile bomu la mkono lililorushwa pale Arusha na kuua makamanda wanne mchana kweupe haikuwa wakati wa JK.
Yule kijana muuza magazeti alieuwawa na kitu chenye ncha kali haikuwa wakati wa JK.
Hata Mwangosi alivouwawa kwa kulipukiwa bomu pale Nyololo ni limagufuli tu lilisababisha.
Dah JK alikuwa peace balaa!
Makamanda TUNAMMISS kinoma!!!!!
 
..kipindi kile CCM walikuwa wanajua kucheza na akili za watu walikuwa wanayalaani matukio hayo.

..CCM ya awamu ya 5 yakitokea matukio ya KIKATILI makada wanaanza kuyasifia.
 
Kweli kabisa!
Lile bomu la mkono lililorushwa pale Arusha na kuua makamanda wanne mchana kweupe haikuwa wakati wa JK.
Yule kijana muuza magazeti alieuwawa na kitu chenye ncha kali haikuwa wakati wa JK.
Hata Mwangosi alivouwawa kwa kulipukiwa bomu pale Nyololo ni limagufuli tu lilisababisha.
Dah JK alikuwa peace balaa!
Makamanda TUNAMMISS kinoma!!!!!
Ndio magufuli alitoa ushauri
 
Back
Top Bottom