Nape haifahamu katiba ya CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape haifahamu katiba ya CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jan 25, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [h=1][/h]

  [​IMG]
  Na Salum Maftah - Imechapwa 18 January 2012

  [​IMG][​IMG]
  KATIKA mdahalo wa wiki jana kwenye kituo cha ITV uliowakutanisha viongozi vijana watatu kutoka vyama vitatu vikuu vya siasa, tumejifunza mengi; na tumeweza kulinganisha uwezo wa vijana hao – John Mnyika (CHADEMA), Mtatiro Julius (CUF) na Nape Nnauye (CCM).


  Hata hivyo, kwa tathmini ya haraka, Mnyika aliwazidi wenzake kwa hoja. Yeye na Mtatiro walimbana Nape hadi akatoa kauli inayozidi kukiangamiza chama chake.

  Kwanza, alikiri kwamba vita ya ufisadi nchini illibuliwa na CHADEMA. Kwa mantiki hiyo, CCM haiwezi kujidai kwa kupiga vita ufisadi, kwa sababu jukumu kubwa ililo nalo ni kujitetea dhidi ya tuhuma za ufisadi ndani yake.


  Maana yake ni kwamba, chochote kinachoitwa mapambano dhidi ya ufisadi ndani ya CCM, ni maigizo tu. Chochote kinachofanywa na chama hiki katika mapambano haya, ni mkakati wa makusudi wa kuwanusuru mafisadi ambao wananchi wanataka washughulikiwe.


  Pili, Nape alikiri kuwa CCM kimejaa mafisadi. Alisisitiza kwamba orodha ya mafisadi wale 11 waliotajwa na Dk. Willibrord Slaa, 15 Septemba 2007 pale Mwembeyanga, Dar es Salaam, ni fupi sana.


  Kwa maelezo ya Nape, ufisadi wa CCM unaanzia chini kwenye mizizi ya chama. Hawa waliotajwa ni vigogo tu, ambao hata hivyo ndio walioohusika na ufisdi mkubwa ulioliingiza taifa katika maafa.


  Hoja ya Nape inapingana kabisa na kauli ya Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, ambaye Mei 2010 alidai ndani ya chama chake hakuna mafisadi.


  Ingawa wote ni viongozi waandamizi wa CCM, na kauli zao ni za chama chao; na kwa kuwa wametoa kauli zinazojikanganya na kupingana kuhusu suala lile lile; hii ya Nape ndiyo inachukuliwa kwa uzito zaidi kwa sababu inaendana na ukweli wa mambo; na imetolewa na mtu mwenye dhamana ya kueneza itikadi, mipango, kauli na matamko ya chama.


  Mantiki ya kauli ya Nape, ndiyo inafafanua kwa sehemu kubwa, kwanini chama hicho kimeshindwa kuchukua hatua dhidi ya mafisadi wakubwa ambao kimekuwa kinawatuhumu.


  Tunajua wazi kuwa jitihada za CCM zilikuwa za kujikosha, ili kupoza makali, kurejesha heshima yake iliyopotea na kuwanusuru watuhumiwa kwa mbwembwe.


  Na kama si mmoja wa watuhumiwa hao, Edward Lowassa kusimama kidete, kumkumbusha Rais Jakaya Kikwete asili ya hoja hii – na kwamba naye (Kikwete) yu miongoni mwa mafisadi; na kama si ujadiri wa Lowassa kusisitiza naye alishiriki kuingiza nchi kwenye mkataba tata wa Richmond, huku akihoji tataribu za kichama zilizokiukwa katika kushughulikia suala hilo, CCM ingekuwa imefanya maigizo ya kufukuza watu kama mradi wa kujisafisha.


  Hali hii ndiyo ilimfanya Nape ashindwe kueleza kwa kina msimamo wa chama chake kuhusu vita dhidi ya ufisadi; na ndiyo ilimsukuma katika kukianika chama chake kuhusu ufisadi uliokithiri kuanzia mashina hadi taifa.


  Tukichunguza vema maana ya ndani ya kauli ya Nape, tutagundua kuwa CCM kimesimikwa katika nguzo za kifisadi – kama kweli kina ufisadi kuanzia mashina hadi taifa.


  Maana yake ni kwamba hakuna wa kumfunga pakae kengele! Wote wameoza. Swali ambalo wengi wanajiuliza, ni kwa nini Nape anakitumbukiza chama chake kwenye mkenge?


  Kushindwa kwa CCM kuchukua hatua kali, ndicho chanzo cha Nape kutapatapa hadi akatamka kuwa moja ya uamuzi mzito uliochukuliwa dhidi ya mafisadi ni kuivunja Kamati Kuu (CC) ya chama chake!


  Lakini inajulikana wazi kuwa CC ilijiuzulu ili kumpisha mwenyekiti aiunde upya, baada ya lawama kwamba haikuwajibika vema kuleta ushindi wa kishindo mwaka 2010. Ilitokana pia na lawama za wanachama na baadhi ya viongozi dhidi ya katibu mkuu aliyekuwapo, Yusuph Makamba na sekretarieti yake.


  Hivyo, kujiuzulu kwa CC ilikuwa njia ya rais kuitikia kishindo cha upinzani wa ndani kwa ndani dhidi ya uteuzi wake kwa Makamba, ambaye alikuwa analalamikiwa tangu alipoteuliwa na Kikwete mwaka 2006.


  Kimsingi, kitendo hicho hakikuwa ushindi kwa Kikwete bali ushindi kwa wapinzani wake, ambao wamekuwa wakilalamikia uteuzi wake usioridhika wa viongozi katika nafasi nyeti ndani ya chama na serikali.


  Hivyo, haikuwa sahihi kwa Nape kujisifu, kwamba hatua hiyo ilikuwa moja ya utekelezaji wa mkakati wa kupambana na ufisadi ndani ya chama.


  Na kama hilo alilosema ni kweli, basi maana yake ni kwamba kamati kuu ilikuwa ya mafisadi; kama kamati kuu ilikuwa ya mafisadi, CCM kimekuwa kinaongozwa kifisadi, na yote yaliyosimamiwa na kamati kuu hiyo ni ufisadi mtupu.


  Je, hii maana yake nini? Nape ametoa shitaka kubwa sana dhidi ya chama chake. Amethibitisha kile ambacho wazee wa chama chake, kina Kingunge Ngombale-Mwiru na Mukama wamewahi kukana huko nyuma.


  Lakini yote hiyo imetokana na kuelemewa kwa hoja kutoka kwa vijana wenzake. Alitumia asilimia karibu 60 za muda wote kujitetea, na nyingine 40 kushambulia wenzake, badala ya kujenga hoja.


  Na wakati akifanya hivyo, wenzake walikuwa wakijenga hoja kwa kutumia matukio ya kweli yanayofahamika. Alishindwa hata kukubaliana na wenzake juu ya ubovu wa katiba iliyopo katika vipengele kadhaa, ili apate pa kuanzia kujenga hoja yake.


  Badala yake, aliishia kushambulia vyama vya CUF na NCCR-Mageuzi ambavyo vinajitapa kwa kuwafukuza uanachama na ubunge Hamad Rashid Mohammed na David Kafulila.


  Katiba ya Tanzania, kutokana na ubovu wake, haizungumzii hatima ya mwanachama kufukuzwa, hasa akiwa pia ni mbunge. Badala yake inaongelea mwanachama kuacha kuwa mwanachama (si kuachishwa au kufukuzwa), kujiuzulu mwenyewe, pamoja na sababu nyingine.


  Hii ingewapeleka kina Mnyika, Dk. Sengodo Mvungi, Mtatiro kwenye mjadala wa katiba ya nchi zaidi; na hivyo Nape kupata ahueni hadi kipindi kiishe.


  Nape akitulia ni mzuri. Tatizo lake anajichanganya na kupoteza muda katika propaganda badala ya hoja.


  Kwa mfano, alisahau kwamba katiba ya CCM katika ukurasa wa wa 125, ibara ya 110 inazungumzia juu ya kazi za kamati kuu ya CCM, ambayo ameisifia sana kwamba ilijiuzulu; na kusababisha kuundwa kwa kamati kuu nyingine.


  Katika ibara ya 110, sehemu ndogo ya 7 Katiba ya CCM inasema hivi kuhusu kazi za kamati kuu:


  "Kumsimasisha uongozi kiongozi yeyote isipokuwa mwenyekiti wa CCM na Makamu wa mwenyekiti endapo itaridhika kwamba tabia na mwenendo wake vinamwondolea sifa za uongozi."


  Hoja zake kuhusu vikao na kufuata taratibu, ingeeleweka kama kamati kuu ingechukua uamuzi wake, mfano iwapo wahusika wanakata rufaa, vinginevyo kamati kuu ya CCM ilitakiwa baada ya kujiridhisha, kukamilisha jukumu hilo la kuwavua magamba wanachama iliyodhamiria kuwashughulikia April 2011, kwa azimio kwamba hawana sifa za uongozi, kwa mujibu wa katiba.


  Vinginevyo aelezee umma kwamba, wanachama hao wana nguvu kuliko wale ambao katiba inasema hawawezi kuvuliwa madaraka – mwenyekiti na makamu wake.   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hata Mimi nilipokuwa Umoja Wa Vijana Wakati Ule tulikuwa hatuangalii katiba Kiundani
   
 3. B

  BigMan JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  huo ni mtazamo wa mwandishi kama mtu binafsi kwa upande wetu wengine mbona nape alifanya vizuri sana na ni kifaa kwa siasa za sasa
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  unamwita kifaa wakati ccm inapiga taarabu,chadema bongo fleva nape anaonekana kucheza mkono mmoja kashika zipu mwingine karusha juu kapiga kata k halafu anaghani yo!yo!yo!yo! Bado wanaccm mnaamini yupo na ninyi?

  Kalaghabaho.
   
 5. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wapiga soga kijiweni wameamka.
  OTIS
   
 6. H

  Honey K JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  tuhuma hizi si ndogo na kwakuwa mwandishi kaandika kwa kituo, naahidi hapa nitarudi kwa muda wa jioni nyumbani nijibu moja baada ya nyingine.....stay tuned!!
   
 7. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  kwani we si msemaji wa Chama kuna haja gani ya kusubiri usiku jibu sasa hivi mkubwa
   
 8. REBEL

  REBEL Senior Member

  #8
  Jan 26, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mimi nasikitika kitu kimoja kwa Nape.Maongezi yake hayawezi kumvutia msomi kama mimi(Mwanasheria) maana hajui kupanga hoja kama Mnyika kabisa(hata nusu yake).Hamna vifungu vyovyote hamna referance yoyote anayotumia yeye ni kama anaimba taarabu. Ndio maana mimi naichukia CCM yaani,mnaua chama hivi hivi.

  Na Mnyika atashine sana tu!Hivi hakuna mtu CCM anayejuakuongea kama Nyerere siku hizi?Muangalie LUsinde na Mwigulu wasivyojua kujenga hoja kwa wananchi wamekaa kipropaganda.maskini ccm!Halafu wengi wao hawapendi kusoma vitu vingi na elimu zao za kukariri.
   
 9. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  karibu hiyo jioni kaka tuone kama una jipya zaidi ya mipasho ya facebook.
   
 10. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tunakusubiri kwa hamu mkuu,vipi lini nafasi za u green guard mtatoa?Arumeru Mashariki byelection haiko mbali
   
 11. d

  davidie JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nape unachofanya hivi sasa ni kucheza sindimba kwenye ukumbi unaopigwa disco tena ya nyimbo za kizungu
   
 12. M

  Malova JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2012
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  huyo ndio Nape wa Chai Chapati Maharage. Lete majibu
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  Jan 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ni Midnight sasa bongo hatujakuona kujibu tuhuma hizo; kwahiyo ni za kweli...

  Wanasiasa ni kazi kutekeleza katiba ya Chama
   
 14. H

  Honey K JF-Expert Member

  #14
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naomba samahani jana nilibanwa na maandalizi ya MIAKA 35 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi nikakosa muda wa kuja kujibu hizi shutuma usiku. Mnisamehe sana mliosubiri.
   
 15. H

  Honey K JF-Expert Member

  #15
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  (Kwanza, alikiri kwamba vita ya ufisadi nchini illibuliwa na CHADEMA. Kwa mantiki hiyo, CCM haiwezi kujidai kwa kupiga vita ufisadi, kwa sababu jukumu kubwa ililo nalo ni kujitetea dhidi ya tuhuma za ufisadi ndani yake.)

  ..... Pengine tumepotoshwa sana katika vita hii ya ufisadi. Tukiwa wa kweli vita hii ilianza rasimi nchini wakati wa Azimio la Arusha na kusimamiwa sana na Marehemu Sokoine, ambao wote Sokoine na Azimio la Arusha ni kazi nzuri ya TANU na baadae CCM. KWA HOJA hii pekeake ukiacha zingine nyingi si kweli kwamba vita hii ya ufiasdi ilianzishwa na Chadema nchini, ilianza toka enzi za WAHUJUMU UCHUMI. kwa kuyajua haya SIWEZI KUSEMA KAMA MTOA HOJA ANAVYODAI, ETI NIMEKIRI KWAMBA VITA HII ILIANZISHWA NA CDM.
   
 16. N

  Ngoiva JF-Expert Member

  #16
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We omba Mungu akusamehe si tulishakuzoe. Uogo ndo mtaji wetu ktk CHAMA.
   
 17. H

  Honey K JF-Expert Member

  #17
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  (Maana yake ni kwamba, chochote kinachoitwa mapambano dhidi ya ufisadi ndani ya CCM, ni maigizo tu. Chochote kinachofanywa na chama hiki katika mapambano haya, ni mkakati wa makusudi wa kuwanusuru mafisadi ambao wananchi wanataka washughulikiwe.)

  .... Naomba mifano ya mafisadi unaodai wanatengenezewa mkakati wa kunusuriwa na kwa faida ya nani? Hivi si hapa ambapo mmekuwa mkiwanukuu baadhi ya watuhumiwa wakilalamika na baadhi yenu hapa jf mnatumika kunitukana mpaka matusi ya nguoni kisa ninasimamia kwa nguvu swala la kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika vizuri? Badala ya kuungwa mkono, ni rahisi hapa kukuta natukaniwa mpaka marehemu babaangu na matusi mengine mengi tu ya kudhalilisha, leo naambiwa ni mchezo wa kuigiza. Hebu tuongee kwa uwazi nani tunamkwepesha na kuchukuliwa hatua???
   
 18. V

  Vancomycin Senior Member

  #18
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo hapa nape umemaliza kuji shutuma ,too low
   
 19. H

  Honey K JF-Expert Member

  #19
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  (Pili, Nape alikiri kuwa CCM kimejaa mafisadi. Alisisitiza kwamba orodha ya mafisadi wale 11 waliotajwa na Dk. Willibrord Slaa, 15 Septemba 2007 pale Mwembeyanga, Dar es Salaam, ni fupi sana.)

  ... Huu nao uongo mwingine wa wazi kabisa! Nilichosema dhana ya kusafisha chama si finyu kama inavyotaka kuaminishwa kwa baadhi ya hoja dhaifu, kwanza hatukutumia orodha ya cdm kuanisha nani anapaswa kuwajibika, tulichosema kutokana na uchambuzi wa baada ya uchaguzi kuna baadhi ya maeneo watu wetu na hasa viongozi hawakutimiza wajibu wao ipasavyo, wengine wametumia nafasi zao kuzulumu haki za baadhi ya wagombea na ikawa ni chanzo cha wananchi kutopigia kura mgombea wa chama chetu, wawajibike.

  Kuna watu kwa tabia zao na mienendo yao wamekitukanisha Chama kwa nyakati mbalimbali, hasa wale ambao walipewa dhamana hasa serikalini wakifikia mahali wakatumia nafasi zao kuisababishia nchi hasara kwa mikataba mibovu na rushwa. Wengine chini huko serikali za mitaa kuna malalamiko ya kutisha, huwezi sema ni watu watatu na ukasema umemaliza wakati malalamiko yako mpaka chini.

  So nlichosema haitoshi kuwajibisha watu watatu, ni muhimu kupitia chama kizima, kuwarudisha viongozi katika maadili ya chama kama bado wanataka kuwa viongozi vinginevyo waachie uongozi tupate viongozi waadilifu.
   
 20. H

  Honey K JF-Expert Member

  #20
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Kwakweli kwa wenye akili nyingi kama wewe its too low hata kusoma majibu yangu
   
Loading...