Nape: Bajeti Mbadala ya Kambi ya Upinzani inadhihirisha uongo wa CHADEMA

There are currently 158 users browsing this thread. (56 members and 102 guests)
Mzito Kabwela,
bullet,
RINGO EDMUND,
Mwanakili90,
Mabel,
T.K,
Jituoriginal,
Dogo Tundu,
Kwaroz,
MARQ,
zebeya,
Obe,
Tympa,
Mshindo,
jenard.lazaro,
incent Augustino,
Hardwood,
NDOFU,
Meshili,
Mathias,
palalisote,
Mpaka Kieleweke,
Advicer,
ACHEBE,
makoye2009,
mfereji maringo,
Mlangaja,
Kibanga Ampiga MKoloni,
Mzee Wa Rubisi,
tumwe273us,
Eshacky,
Kiby,
FUSO,
gmosha48
, Ados,
STREET SMART,
Henge,
Dr.W.Slaa,
The dirt paka,
Mazoya,
Madago,
forty
, Ledio,
Buswelu,
mkute,
M-mbabe,
Mwiburi,
jogi,
Lunyungu,
Edmond,
maandamano
, Buchanan,
sailor1,
ibange,
Sangara
 
Hivi CCM katika tafuta tafuta yani kabisa wakaacha watu wote wakampa NAPE? Si bora wangempa January Makamba hii post? Kumpa nape hiki cheo ni sawa na alivyopewa Makamba ukatibu wa CCM.This is mistake number 2
 
NAPEEE!! Kwanin basi Usiangalie Ilani ya uchaguzi ya Chadema maana hiyo ndio ilieleza CDM itafanyanin ikipata madaraka na hiyo ndio inajibu maswali yako.Hapa Chadema wamechangia kama kambi ya upinzani yaani mchango wao kwenye bejati ya serikari ya ccm,CHADEMA HAWANA TRA walaa vyombo vingine vya serikali.Hata hilo haulijui 'kiongozi?!' au wewe ndio umeamua kupotosha uma?! Usiwe mpinzani wa kila kitu bana sifia inapobidi!.
 
Hivi huyu jamaa kule Nchingwea amefanya nini cha kujivunia? Wananchi wa Lindi hebu tujuzeni....
 
ACHEBE ambaye ni NAPE hajui anakokwenda wala alikotoka yeye anafikiri kuwa kupambana na CDM ndio ataonekana anafanya kazi .........
Juzi kwenye FB alijisahau na kupost hoja ya posho juuu ya Zitto na akarudia hayo hayo kwenye JF kwa jina la ACHEBE ndio maana niliweza kumtambua .
 
Siasa za Uchaguzi mbona ziliisha kitambo, na kama elimu kuwa si inaanza kwa kupunguza ada mwaka kwa mwaka, kumbuka ilani ya uchaguzi NAPE ni ya miaka mitano na hii budget ni ya mwaka wa kwanza tu. kwa hiyo chukua hatua.
 
Hivi CCM katika tafuta tafuta yani kabisa wakaacha watu wote wakampa NAPE? Si bora wangempa January Makamba hii post? Kumpa nape hiki cheo ni sawa na alivyopewa Makamba ukatibu wa CCM.This is mistake number 2
Nafikri Makamba snr.yuko vizuri kichwani kuliko huyu dogo
 
Huyu jamaa anatapatapa tu amekua kama marketing Manager wa makampuni ya simu. Hana jipya atasema kupiga simu bure, ukiweka vocha unapata dakika za bure, ukituma pesa kwa kutumia jia ya simu utashinda zawadi, ndio vitu tulivyo vizoea kutoka kwake.
 
Mr Nape... Kama unaona waongo basi mshauri Bw JK awaazime Chadema kiti cha uongozi kwa Mwaka mmoja tu uone wataifanyia nini nchi hii mliyoitafuna na kuimaliza.... Kila kitu tunacho why are we still poor????..... if your Chairman & PM doesn't have the answer of this question am not expecting from you NAPE

ONDOKENI MADARAKANI CCM HATUWATAKI TENA
 
Hivi Kati ya hizi Ahadi Hapa Chini nani MUONGO

Ahadi za Kikwete:

  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu- Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  44. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
  45. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
  46. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
  47. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  48. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
  49. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
  50. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
  51. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
  52. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
  53. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
  54. Kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
  55. Kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
  56. Kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  57. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kibandamaiti mjini Zanzibar
  58. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
  59. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
  60. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
  61. Kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
  62. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
  63. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  64. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
  65. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
  66. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
  67. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha

Ahadi za Dk Slaa:

  1. Kujenga nchi isiyo na ufisadi
  2. Kurejesha maadili ya taifa, utumishi wa umma
  3. Kuanza mchakato wa katiba mpya ndani ya siku 100
  4. Kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili muungano na Zanzibar
  5. Kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo
  6. Kukata asilimia 20 ya mshahara wa rais
  7. Kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia 15
  8. Kuweka Mwenge wa Uhuru Jumba la Makumbusho
  9. Kutoa huduma bora za afya bure
  10. Kutoa elimu bure chekechea hadi kidato cha Sita (elimu ya lazima)
  11. Kufuta kodi ya vifaa vya ujenzi
  12. Kuwalipa wazee wa EAC fedha zao ndani ya siku 100
  13. Kuwalipa wanaoidai DECI
  14. Kubana matuzi ya serikali
  15. Kupunguza ukubwa wa serikali (Mawaziri 15, manaibu watano)

Ahadi za Profesa Lipumba

  1. Elimu ya bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu
  2. Kubana matumizi kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri
  3. Kuunda serikali shirikishi
  4. Kusimamia rasilimali
  5. Kuimarisha miundombinu
  6. Kusimamia na kuboresha afya
  7. Kuboresha kilimo, viwanda na uwekezaji
  8. Kurudisha chakula cha bure mahospitaliniAhadi za Kikwete:
  9. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
  10. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
  11. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
  12. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
  13. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
  14. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
  15. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
  16. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
  17. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
  18. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
  19. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  20. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
  21. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
  22. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
  23. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
  24. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
  25. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  26. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
  27. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
  28. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
  29. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
  30. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
  31. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
  32. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
  33. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  34. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
  35. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
  36. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
  37. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
  38. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
  39. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
  40. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
  41. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
  42. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
  43. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
  44. Kulinda haki za walemavu- Makete
  45. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
  46. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
  47. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  48. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
  49. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
  50. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
  51. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  52. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
  53. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
  54. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
  55. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  56. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
  57. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
  58. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
  59. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
  60. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
  61. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
  62. Kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
  63. Kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
  64. Kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  65. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kibandamaiti mjini Zanzibar
  66. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
  67. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
  68. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
  69. Kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
  70. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
  71. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  72. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
  73. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
  74. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
  75. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha

Ahadi za Dk Slaa:

  1. Kujenga nchi isiyo na ufisadi
  2. Kurejesha maadili ya taifa, utumishi wa umma
  3. Kuanza mchakato wa katiba mpya ndani ya siku 100
  4. Kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili muungano na Zanzibar
  5. Kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo
  6. Kukata asilimia 20 ya mshahara wa rais
  7. Kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia 15
  8. Kuweka Mwenge wa Uhuru Jumba la Makumbusho
  9. Kutoa huduma bora za afya bure
  10. Kutoa elimu bure chekechea hadi kidato cha Sita (elimu ya lazima)
  11. Kufuta kodi ya vifaa vya ujenzi
  12. Kuwalipa wazee wa EAC fedha zao ndani ya siku 100
  13. Kuwalipa wanaoidai DECI
  14. Kubana matuzi ya serikali
  15. Kupunguza ukubwa wa serikali (Mawaziri 15, manaibu watano)

Ahadi za Profesa Lipumba

  1. Elimu ya bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu
  2. Kubana matumizi kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri
  3. Kuunda serikali shirikishi
  4. Kusimamia rasilimali
  5. Kuimarisha miundombinu
  6. Kusimamia na kuboresha afya
  7. Kuboresha kilimo, viwanda na uwekezaji
  8. Kurudisha chakula cha bure mahospitalini
 
NARUDIA : KATI YA AHADI HIZI HAPA CHINI NI ZIPI HAZINA UKWELI NA SI KWA MANUFAA YA TAIFA

Ahadi za Kikwete:

  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu- Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  44. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
  45. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
  46. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
  47. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  48. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
  49. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
  50. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
  51. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
  52. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
  53. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
  54. Kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
  55. Kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
  56. Kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  57. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kibandamaiti mjini Zanzibar
  58. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
  59. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
  60. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
  61. Kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
  62. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
  63. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  64. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
  65. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
  66. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
  67. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha

Ahadi za Dk Slaa:

  1. Kujenga nchi isiyo na ufisadi
  2. Kurejesha maadili ya taifa, utumishi wa umma
  3. Kuanza mchakato wa katiba mpya ndani ya siku 100
  4. Kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili muungano na Zanzibar
  5. Kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo
  6. Kukata asilimia 20 ya mshahara wa rais
  7. Kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia 15
  8. Kuweka Mwenge wa Uhuru Jumba la Makumbusho
  9. Kutoa huduma bora za afya bure
  10. Kutoa elimu bure chekechea hadi kidato cha Sita (elimu ya lazima)
  11. Kufuta kodi ya vifaa vya ujenzi
  12. Kuwalipa wazee wa EAC fedha zao ndani ya siku 100
  13. Kuwalipa wanaoidai DECI
  14. Kubana matuzi ya serikali
  15. Kupunguza ukubwa wa serikali (Mawaziri 15, manaibu watano)

Ahadi za Profesa Lipumba

  1. Elimu ya bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu
  2. Kubana matumizi kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri
  3. Kuunda serikali shirikishi
  4. Kusimamia rasilimali
  5. Kuimarisha miundombinu
  6. Kusimamia na kuboresha afya
  7. Kuboresha kilimo, viwanda na uwekezaji
  8. Kurudisha chakula cha bure mahospitalini
 
Nape naomba unisaidie kumuuliza katibu mkuu wa CCM Mkama alipoenda Musoma alisema hospitali ya rufaa iliyotelekezwa itajengwa kipindi hiki ,mbona haipo kwenye mpango wa miaka mitano?
 
Wana Jamvi naombeni mnisaiidie qualifications za huyu Nape maana simuelewi. Anauliza chanzo cha mapato cha kuwalipa hao walimu na kupandisha kima cha chini wakati kwenye bajeti mmbadala vimeelezwa au kuwalipa walimu na kupandisha mishahara inagharimu trilioni ngapi kwamba haiwezekani???
Pia anaongelea suala la elimu bure ina maana aliambiwa ndani ya mwaka mmoja ndo elimu itakuwa bure??? Atleast wenzao wanaonyesha kuelekea kwenye elimu bure CCM hata kupasogelea hawataki. Huyu naye ni fisadi hana lolote
 
Huyo dogo sijui akili imezidi kugandiana? unauliza vyanzo vya mapato katika nchi yenye rasilimali kama yetu? hivi huyo nape hajui nchi hii ina utajiri kiasi gani kama viongozi wetu wakionyesha japo chembe ya uzalendo?
tatizo jamaa wamezoea kujilipa mno mpaka wanafikiri kuwa hapa bongo hatuwezi simamia utajiri uliopo
 
BAJETI MBADALA YA KAMBI YA UPINZANI NI UTHIBITISHO WA UONGO WA CHADEMA

1.0 UTANGULIZI:

Leo tarehe 15/06/2011 kambi ya upinzani bungeni ambayo inaundwa na chama cha CHADEMA kupitia waziri wake kivuli wa fedha Mhe. Zitto Kabwe (Mb), imewasilisha bajeti yake aliyoiita bajeti mbadala kwa mwaka wa fedha 2011/2012.

Nichukue nafasi hii kumpongeza kijana mwenzangu kwa uwasilishaji wa bajeti na kwa baadhi ya mambo ya msingi yaliyomo ndani ya bajeti husika.Hata hivyo bajeti imeacha maswali kadhaa bila majibu.

Katika bajeti hiyo pamoja na mambo mengine kwa kiasi kikubwa imedhihirisha kuwa maneno mengi na ahadi nyingi zilizotolewa na CHADEMA wakati wa Uchaguzi kama sio zote basi nyingi zilikuwa ahadi hewa zilizolenga kuwa hadaa wapiga kura kwa nia ya kupata kura.

2.0 MANTIKI YA HOJA:

Moja kati ya misingi mikuu ya kutengeneza bajeti katika mazingira ya siasa za kwetu na nyingine nyingi duniani ni ahadi ambazo chama kimeahidi kwa Wananchi wake aidha kwa kupitia Ilani ya Uchaguzi au ahadi binafsi za Mgombea Uraisi alizozitoa kipindi cha kampeni ya uchaguzi. Kwa maneno mengine bajeti ni zao la Ilani ya Uchaguzi ya Chama husika na sera mbalimbali zilizopo.

2.1 Elimu Bure kwa Watanzania kwa ngazi zote;

Kwa mfano kupitia Ilani ya CHADEMA ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na ahadi kibao za kila mara za aliyekua mgombea urais wa chama hicho Dr. Slaa, waliahidi wakichaguliwa watatoa elimu bure kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu.

Itakumbukwa hii ni moja ya ahadi zilizovutia sana wakati huo, lakini huku wakijua kuwa wanadanganya waliendelea kutoa ahadi hiyo kwa muda wote wa kampeni hizo, sasa imefika wakati tulitegemea wangeonyesha kwa vitendo kwa kuweka kwenye bajeti yao jinsi wanavyoweza kutoa elimu bure lakini bajeti hii mbadala ya 2011/2012 ni uthibitisho wa hadaa ya CHADEMA kwa umma wa watanzania.

Hapa namnukuu Waziri kivuli wa fedha,
“..(ix)kuondoa ada kwa wanafunzi wa shule za sekondari za kutwa na kupunguza ada kwa sekondari za bweni kwa kiwango cha asilimia hamsini kwa wavulana na bure kwa wasichana...”

Lakini katika Ilani yao ya Uchaguzi ya mwaka 2010 ukurasa wa 15. Inaeleza CHADEMA itahakikisha “ Elimu ya ngazi ya msingi na sekondari itagharimiwa na serikali kuu pamoja na serikali za mitaa”.
Hapo ndipo tunapouona uongo dhahiri wa CHADEMA wa kukiri kuwa Serikali haiwezi ikatoa Elimu bure kwani katika Bajeti yao mbadala wanakiri kuwa watapunguza ada kwa asilimia hamsini kwa wavulana.

Kwa mantiki hiyo suala la wanafunzi wa sekondari kuchangia wanalikubali ila walitumia ghiliba kipindi cha kampeni ili kuwaongopea Watanzania kwa kitu ambacho hawawezi kukitekeleza.

Kinachosikitisha zaidi, kwenye bajeti hii mbadala iliyosomwa leo, inaonyesha dhahiri kwa upande wa elimu; hakuna mpango wowote unaozungumzia “Elimu ya Juu” kama vile si kitu kwao ukilinganisha na walivyokuwa wakihubiri kwenye majukwaa wakati wakitafuta kura. Hakika huu ni usanii mkubwa kumbe walikuwa wakitafuta kura za vijana hawa tu hawana mpango nao!!

2.2 Kushusha bei ya vifaa vya ujenzi;

Ahadi nyingine kubwa iliyovuta hisia za wengi ni ya kushusha bei ya mfuko wa saruji kufikia shilingi za kitanzania elfu tano, pamoja na vifaa vingine vya ujenzi. Kwenye bajeti hii mbadala tulitegemea wangewaeleza watanzania hili wangelifanyaje lakini badala yake waziri kivuli wa fedha anaishia kusema;
“..itakuwa marufuku kwa kituo cha uwekezaji kutoa ruhusa ya msamaha wa kodi kwa makampuni ya uwekezaji kwa bidhaa zinazozalishwa nchini na hasa Saruji....”

Hapa hakuna mkakati wowote wa kufanya mfuko wa saruji uuzwe shilingi za kitanzania elfu tano kama CHADEMA walivyotaka watanzania waamini wakati wa uchaguzi. Huu ni ushahidi wa hadaa ya CHADEMA.

Kwenye bajeti hii mbadala waziri kivuli anasema.... “ujenzi wa barabara za vijijni utatumia kwa kiasi kikubwa nguvu kazi watu (labour intensive)..”

Viongozi wengi wa CHADEMA wanasifika kwa kuzuia wananchi wasichangie shughuli mbalimbali za maendeleo huko vijijini, leo inashangaza kusema watatumia kwa kiasi kikubwa nguvu kazi watu, huu bila shaka ni unafiki na hadaa kwa wananchi.

2.3 Suala la kukwepa kodi;

Umejengeka utamaduni wa watu na taasisi mbalimbali kukwepa kodi na kuona kuwa suala hilo ni la kawaida. Lakini ikumbukwe kuwa kukwepa kodi kunaipunguzia mapato serikali na hivyo kupunguza uwezo wake wa kutoa huduma kwa jamii.

CHADEMA wanakiri hili kupitia Bajeti yao mabadala iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha Kivuli Mhe. Zitto Kabwe, kuwa ......”kuna watu wengi sana ambao wanapata mapato makubwa lakini hawalipi kodi......” Kauli hii ya CHADEMA inapingana na matendo yao halisi, kwani itakumbukwa wanamlipa katibu Mkuu wao Dr. Wilbroad Slaa zaidi ya shilingi Milioni saba, fedha ambayo haikatwi kodi yeyote.

Chakushangaza zaidi pamoja na CHADEMA kuendelea kumlipa Dr. Slaa mamilioni yasiyotozwa kodi, bila aibu Zitto anatoa wito kwa kila Mtanzania mwenye kipato alipe kodi ya kipato chake.
Na anaendelea kusema kuwa ... “kulipa kodi ndio ishara ya Uzalendo na ili raia aweze kuinyoshea kidole serikali yake lazima awe na uchungu na uchungu unapatikana kwa kulipa kodi.”

Kwa kauli hii ya Zitto, anauthibitishia umma wa Tanzania kuwa Dr. Slaa siyo mzalendo na wala CHADEMA pia siyo wazalendo. Kwani Dr. Slaa alitakiwa kukataa kuchukua mshahara usiokatwa kodi, na Chama chake kilipaswa kupeleka kodi za watumishi wake serikalini.

2.4 Kima cha chini cha mshahara;

Katika bajeti yao mbadala, CHADEMA wanaahidi kuongeza kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wa Umma mpaka kufikia Tshs. 315,000 kwa mwezi na kutoa motisha kwa walimu wanaofundisha Vijijini kwa kuwapa Mshahara mara moja na nusu ya wenzao wanaofundisha mijini.
Cha kushangaza hawajaainisha fedha hizo za ziada watazitoa wapi, hata katika mchanganuo wao wa mapato hawajaonesha kuwa kiasi hicho cha pesa kitatoka wapi. Huu ni usanii mkubwa na uongo ulikithiri.

3.0 HITIMISHO:

Ukipitia mambo haya machache kama mifano utagundua kuwa sehemu kubwa ya ahadi za CHADEMA kwa wananchi ni ulaghai na uongo usio na mfano, hivyo wananchi wanapaswa kuutambua mti kwa matunda yake si majani yanayoonekana na kutamanisha machoni.

Ukiifahamu kweli itakuweka huru, ni muhimu kuitafuta na kuifahamu kweli.

Imetolewa na;

Nape Moses Nnauye,
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
15.06.2011

Mkuu Nape
Nina imani kwamba Tanzania kama tukiamua yote yana wezekana. Tatizo kubwa tulilo nalo bado hakuna (UTASHI WA KISIASA/POLITICAL WILL). Kwani nchi yetu inaendeshwa kisiasa zaidi, kama wanasiasa wataiachilia nchi iendeshwe kwa mjibu wa sheria/utawala wa sheria(Rule of Law) Tanzania si nchi masikini kama tunavyoambiwa.

Umejitahidi kuzungmzia swala la bajeti mbadala jinsi ambavyo haitekelezeki, lakini kitu ulichokisahau ni ahadi ambazo mwenyekiti wa ccm na rais wa jamhuri alizozitoa je kwa kiwango gani amezitekeleza? hapo ndipo wanasiasa mnapo yumbisha nchi. Tunapokuwa na wanasiasa wanao piga propaganda zaidi na bila kujali uhalisia wa mambo ndipo tatizo linapojitokeza.

Ushauri wangu, wewe ni kijana uko pontential au una future kubwa huko mbele, kisaidie chama chako. Wapo watu ccm wamelewa madaraka
hawasomi nyakati, hawaoni majira haya siyo yaliyopita, hao mkiwaelimisha mapinduzi ya kifikra yatapatikana ya dhati. Waambieni watanzania wazamani si waleo.

Mwambieni Rais ukweli, msimsome uso anataka asikie nini kisha ndo mumwambie anayoyataka, hapo hammsaidii. Mwambieni akatae kusikia ushauri hapo mtakuwa mmenawa mikono kama Pilato, la sivyo tunakoelekea mnatupeleka kwenye machafuko ambayo hayana sababu.
Msidharau wapinzani, yapo mambo yakujifunza kwao ondoeni jeuri ya chama, ni ukweli usipingika kwamba hivi sasa vyombo vya dola ndo nguvu ya chama badala ya nguvu ya wananchi. Nguvu halisi ya wananchi itakapo amua nguvu ya vyombo vya dola haitaweza kuizima.

Kisaidieni chama acha propaganda za mzee Kingunge za Bulgaria, hizo zilifaa wakati wa vita baridi. Sasa hivi hakuna wananchi wanao taka kubaki nyuma hali nchi nyingine zinaendelea. Wabunge wa ccm wasitumike kama rubber stamp huko bungeni, wananchi wanayaona hata kama dola itawasaidia kwa kutumiwa na chama kuingia bungeni iko siku wananchi watawahukumu.

Haya ni mawazo yangu, kwani kama tutakuwa wakweli na wazalendo matatizo makubwa yanatokana na jeuri,dharau ambayo chama tawala na dola inayo kwa wananchi wake. Hebu tufike mahala tuijenge nchi mnawafahamu wazalendo kati yenu na wale ambao ni wachumia tumbo pia.
Kwenye jamvi humu kuna ushauri ambao unaweza kuwasaidia pitieni humu chukua kile kinachoweza kukusaidia. Usitumie propaganda ya kizamani watu wanauelewa kwa sasa.( WATANZANIA WALEO SIYO WAJANA).
 
Ushauri wangu ni kwamba from now acheni kumjibu Nape just ignore him na okoa muda wako kwa kusoma mada endelevu na zenye mashiko kuliko kumuongelea huyu dogo si mwelewa . Alisoma India sijui alisoma nini huko .Maana yeye hajui kwamba hata faini zile za mahakamani ni vyanzo vya mapato . Faini za barabarani ni vyanzo vya mapato . Yeyey na CCM wanajua kuomba wazungu tu na si zaidi .
ndugu yangu vyuo vya pale india unazania vina kitu si unasomea nyumbani ukiwa pale muda mwingi nikunywa bia zinaitwa kingfisher yani nape pale india alikwenda kuweka recod kuwa naye alifika india kusoma lakini navyojua mimi kwa vyuo vya pale akuna kitu nape alikwenda kuzuga tu
 
Nape,
Mkuu wangu nadhani wewe ni mwanasiasa wa itikadi na hujui kabisa mantiki ya bajeti ya upinzani hua inasimamia misingi ipi.

Haiwezekani kabisa Chadema wakaleta bajeti inayozungumzia ilani na ahadi zao zitumike ktk bajeti ambayo inatolewa na chama tawala, isipokuwa Chadema wanachoweza kufanya ni kuonyesha mapungufu ktk bajeti hiyo ya chama tawala kulingana na sera, iilani za chama tawala na mgombea ama kupinga bajeti inayowakandamiza wananchi pamoja na bajeti inayodhoofisha uchumi ktk ukusanyaji wa fedha za pato la Taifa kinyume cha matarajio ya wananchi waliokipa chama hicho dhamana ya uongozi.

Sasa unapokuja hapa na kuzungumza kwamba Chadema walitakiwa kuonyesha dhamira yao ya kutoa elimu bure hali wananchi wamechagua mrengo wa CCM tena kwa maneno yako mwenyewe umeandika hivi :-

"Moja kati ya misingi mikuu ya kutengeneza bajeti katika mazingira ya siasa za kwetu na nyingine nyingi duniani ni ahadi ambazo chama kimeahidi kwa Wananchi wake aidha kwa kupitia Ilani ya Uchaguzi au ahadi binafsi za Mgombea Uraisi alizozitoa kipindi cha kampeni ya uchaguzi. Kwa maneno mengine bajeti ni zao la Ilani ya Uchaguzi ya Chama husika na sera mbalimbali zilizopo."

Kwa hiyo lazima ufahamu kwamba mbio za uchaguzi zimekwisha na wananchi wamechagua sera, ilani na ahadi za JK kupitia chama CCM kuwa dira ya mwongozo wa maendeleo ya miaka mitano ijayo na sii jukumu la Chadema kuendelea libeneke bungeni wakinadi sera na ilani za chama kama vile hawakubaliani na matakwa ya wananchi, isipokuwa Chadema watapinga pale itikadi inayopingana na imani ya chama itakapo tumika ktk kuunda sheria, zaidi ya hapo ni kupitia bajeti ya CCM na kutazama uwezekano wa hizo sera, ilani na ahadi mlizotoa kama kweli zitaweza kuleta maendeleo na kama haziwezi ni sehemu zipi Chadema imeyaona mapungufu na yanahitaji kufanyiwa marekebisho..

Swala la kodi halimhusu Dr.Slaa pekee ni sheria ambayo imepitishwa na chama tawala kiasi kwamba wabunge wote na watumishi wa Umma wamekuwa wakipokea fedha pasipo kulipia kodi. Haijalishi ni mbunge wa chama gani isipokuwa sheria yenyewe ndio dhaifu na Chadema wanataka sheria hiyo ibadilishwe.

Dr.Slaa halipi kodi kutokana na sheria hiyo, vivyo hivyo JK, Pinda, viongozi na wabunge wote hawalipi kodi hizi za posho iweje leo wewe umtazame Dr.Slaa ambaye anatumikia sheria mloitunga nyie.

Tumeona kwamba mshahara wa mbunge ni Tsh 2.4 millioni lakini kwa ujumla mbunge hupokea millioni 7 kwa mwezi kutokana na ongezeko la malupulupu na posho ambazo hakuna mbunge anayelipia kodi kutokana na sheria yenu.

Hili ndilo swala na Chama Chadema sio swala la nani anachukua anani hachukui bali kinachopingwa hapa ni sheria na sii mtu.

Kwa nini Chadema wameileta hoja hizi buingeni ktk bajeti yao? ni kwa sababu wamepitia vitu, wamepokea hizo fedha na hawaoni lazima wala umuhimu wake ktk ujenzi wa Taifa na ndio maana wanataka posho ziondolewe acha mbali kulipiwa kodi, hii haina maana kwamba walitakiwa watochukua posho hizi au kulipia kodi wakati sheria hairuhusu kukukusanya kodi kutoka posho za wabunge na watumishi wa serikali.

Kifupi mkuu wangu umeonyesha ufinyu mkubwa ktk kuelewa jinsi bunge au upinzani unavyoweza kuwakilisha bajeti yake na kama sikosei ulitaka kugombea Ubunge sijui ingekuwa vipi kuwa na wabunge kabuntas vs vivuli?
 
..CCM wanaingia ktk kupinga kila wazo linalotolewa na CDM hata kama litakuwa na manufaa kwa taifa letu.

..mimi nadhani kupunguza ada ya wanafunzi wa kivulana na kuondoa kabisa kwa wanafunzi wa kike ni hatua nzuri kuelekea kufutwa kabisa kwa ada hiyo.

..badala ya kuipinga hoja ya Chadema kiujumla-jumla kama alivyofanya Nape, bora CCM wangekuja na hoja mbadala na kupunguza ada ya shule ili waonekane wako more practical.

..pia kuhusu suala la posho, ingependeza kama wabunge wa CCM wangekubaliana na hoja hiyo, halafu baada ya kufanya hivyo wawa-challenge CDM kupunguza malipo wanayompatia Dr.Slaa.

..zaidi, ingependeza kama tungeweza kupata mchanganuo wa mishahara, posho, na mafao, ya viongozi wote wa umma. taarifa za mapato ya viongozi wote wa umma zinapaswa kuwa available in the public domain.
 
Back
Top Bottom