Nape: Bajeti Mbadala ya Kambi ya Upinzani inadhihirisha uongo wa CHADEMA

72.kununua bajaj nchi nzima kwa ajili ya kusaidia akina mama waja wazito
73.kuifanya kigoma kuwa kama dubai
74.kulipa deni la chama cha ushirika mwanza tzs 3bn
75.kutopenda kusafirisafiri maana nawaudhi wananchi

ushauri wa bure kwa nape, humu ukiingia sifu chadema mwanzo mwisho nakuapia hakiaamungu huta guswa na mtu kwa matusi wala kejeli na soon utaanza kuitwa shujaa, mpiganaji nk. Lakini kwa mwendo huu wa kusema ukweli hakika humu hapakufai
 
Ndugu mh.Nape,kama mmekuwa viongozi kwa bahati mbaya sisi watanzania tumegundua. Haingii akilini kwa mtu timamu akae afikirie Nape amekuwa mpinzani dhidi ya wapinzani,ikumbukwe nia ya upinzani ni kumkosoa mtawala, sasa ni upotokaji mtawala badala ya kuonesha kuwa haiwezekani anaanza kuponda.

Umeeleza kuhusu mshahara wa dr Slaa,unasema alipi kodi kwani anajikata kodi au mamlaka ndo inapaswa kuikusanya kutoka kwake?unasema watawala waoneshe mfano,je kiongozi wa nchi analipa kodi kwa mshahara anaoupata?au sheria za kibaguzi kuwa private company ndo walipe kodi alaf no to govt.? govt.yenyewe inatoa ajira mia , mia50 kati ya zaidi ya lak4 wahitimu wa kozi mbali mbali,je iyo ni govt au NGO?

Unasema bajet ya cdm haijaonesha elimu bure waliyohaidi wakati wakichukua dola,je japo nec ilichakachua,mmekubali kuwapa dola?alaf mnaitaka bajeti ya elimu bure. Mh.Zitto kawaambia achaneni na kuweka mirija ya kutunyonya, bado mnammaliza mtanzania, mlitangaza umeme mgao umeisha lakini njoo kinondoni kuanzia sa12-sa5 usiku umeme kila siku alaf mnataka raia tuwashabikie? Kwa lipi?

Mkae mkijua leo cdm imepinga kuchangia elimu kama kenya,nyie mnagoma. Pia hata zanzibar,kuanzia cheti mpaka doctrate,govt inawasomesha,bahati yenu mmekutana nasi wabara wapole,elimu yetu mmeifanyia siasa! Mnagawa mikopo pale HESLB ktk %kama mnatoa maksi ya test vile?unategemea nini?apa mnaandaa wapiga kura wa 2015 wenye chuki kali kwa govt.

Nyie mnaenda mikoani,bungeni na ktk tbc yenu mkiwaponda wapinzani hamjui kuwa mnaponda mawazo ya watanzania wachovu. Ninayo mengi ila naishia apa maana nasikia hasira dhidi ya uchambuzi wako.

Wakati tunasoma primari,mwl wetu alikuwa akitoa maksi na zawadi,zawadi ktk madaraja: vema,vizuri sana,vizuri,hafifu. Hapa mi nakupa Hafifu. Mkuu si kila kitu ufanye siasa pinzani,kadi yangu ya ccm itaendelea kukaa kwenye briefcase mpaka chama kitakaporudi ulingoni.

Kikifa sina hasara maana wapinzani wameonesha nia ya dhati ya kuondoa ukandamizaji. Siku njema.
 
Nimependa kuona jinsi mheshimiwa Nape Moses Nnauye alivyojaribu kujenga hoja na kujibu (kukosoa) bajeti mbadala ya kambi ya upinzani kwa haraka (yaani ndani ya muda mfupi). Hata hivyo nimeshangaa kuona akiwa amejikita zaidi katika kuichambua CHADEMA huku akihusianisha na ahadi walizozitoa kipindi cha kampeni na ili kupata makosa hayo, nasikitika kuona Nape amesahau kuwa hivi sasa wananchi wanataka kuona utekelezaji wa mikakati itakayoboresha maisha yao na kuwaondoa katika lindi zito la umasikini na siyo mijadala ya mabishano kama vile kipindi cha kampeni.

Mapungufu aliyoyaainisha Nape ni dhahiri kuwa amejikita kuyazungumzia na kuyachambua ili kuonyesha ni kwa jinsi gani anatafuta nafasi ya kujibu hoja nzito kisiasa,kwa mfano. Je, ni kweli suala la elimu bure linaweza kutekelezwa ndani ya mwaka mmoja pasipo kuathiri mfumo uliopo?

Katika bajeti ya serikali wanazungumzia kutokatwa kodi katika posho. CHADEMA wanaeleza kuwa Dr Slaa analipwa posho za kumsaidia kuendesha shughuli zake. kwa maelezo ya Nape ni dhahiri kuwa posho inapaswa kukatwa kodi..

Ushauri wangu ni kuwa Nape kama kiongozi wa chama kilichopo madarakani anapaswa kuchukua ushauri mzuri kutoka upinzani na kuufanyia kazi ili kukifanya chama chake kiendelee kuongoza nchi na siyo kukosoa tu hata pale panapostahili pongezi!!!!!

".....Nichukue nafasi hii kumpongeza kijana mwenzangu kwa uwasilishaji wa bajeti na kwa baadhi ya mambo ya msingi yaliyomo ndani ya bajeti husika.Hata hivyo bajeti imeacha maswali kadhaa bila majibu........."

HAPA NAAMINI HAJAPONGEZA WALA KUTAMBUA CHOHCOTE CHEMA KWENYE BAJETI HIYO...KAZI KWELIKWELI....
 
ushauri wa bure kwa nape, humu ukiingia sifu chadema mwanzo mwisho nakuapia hakiaamungu huta guswa na mtu kwa matusi wala kejeli na soon utaanza kuitwa shujaa, mpiganaji nk. Lakini kwa mwendo huu wa kusema ukweli hakika humu hapakufai

Sio kweli, ila kwa hoja alizoweka Nape huhitaji kuwa chadema, cuf wala tpt-maendeleo kuona ni pumba!! Kubali kwamba Nape HANA uwezo wa kujenga hoja zaidi ya MIPASHO tu..
 
There are currently 144 users browsing this thread. (54 members and 90 guests)
Narubongo Rev Fr Masanilo Edson Z. M RINGO EDMUND Edson Kitila Mkumbo soft Mathias palalisote kiyeyeu kaburunye Mpaka Kieleweke Advicer ACHEBE mjogoro Gsana brazakaka mwakichi Mshindo makoye2009 Tympa kukumdogo mfereji maringo Mlangaja Kibanga Ampiga MKoloni Mzee Wa Rubisi tumwe273us Eshacky Kiby FUSO gmosha48 Ados STREET SMART Vonix Henge Dr.W.Slaa The dirt paka Madago forty Ledio Buswelu Yericko mkute M-mbabe Mwiburi jogi Lunyungu Edmond maandamano Buchanan sailor1 ibange Sangara

nakuona Dr kwa mbali unamsoma nape, nadhani ccm sasa wanajuta kwanini walimtoa chiligati, nasubiri ccm kuja na ya kujivua ngozi kabla ya october 2011
 
Nape nape mdogo wangu,mbona unakurupuka dogo.afadhali ccj ilinyimwa usajili kwani ungesababisha upinzani uonekane kituko.
Naomba uniambie ni meli ngapi zipo kwenye bajeti ya ccm mwaka huu.
Kama huna jibu rudi kanisani hapa singida tuendelee kimba injili kama zamani,na usingekimbia tungekuta tuna albam ngapi sasa hivi?
 
Nape kakurupuka na akili zake chache sana anafikir watz ni wakupotoshwa tu na propaganda za magamba, hajasikiliza bajeti vizur na hivyo asubir kesho aisome kwnye magazeti asikimbilie kutoa matamko bila kufanya tafiti.

Atakuwa amedanganywa na wabunge wa magamba walioshiriki party caucus yao jana usiku ukumbi wa msekwa akakimbilia kutoa tamko.

Suala la elimu limeelezewa vizur pamoja na rural growth na vyanzo mbadala na mwonekano wa bajeno wa bajeti upo vizur, sasa sijui anacholalamikia ni kipi?

Haoni jinsi wabunge wake walivyokuwa wametulia wakati bajeti ya kambi inawasilishwa? Nan pia wamepigia kelele suala la posho kumbe hata kusoma hawakusoma kwnye mpango wao wa maendeleo ambao walikuwa wanaushabikia , ambapo suala la posho lipo.

Kweli Nape Kilaza.
 
Acheni ushabiki usiokua na maana.Mafisadi hata CDM wapo.Si kwamba huyo Dk silaa au Dk mabunduki ni safi ni fisadi tu hospitali yake CCBRT imejaa gharama kubwa wakati huo huo anapokea mabilioni kibao kutoka serekalini.
 
Wakuu hizo ahadi ukizipitia zinafurahisha sana - jamaa ni kiboko. hebu cheki ile ya 3 aisee atakuwa ametusaidia hasa sisi wa sikonge kupata maji safi na salama toka ziwa victoria, tunausubiri mradi huu ingawa sijaona dalili zozote kwenye bajeti ya mwaka huu.

Na ile ya 39, kujenga barabara ya Lami Manyoni - Tabora - Kigoma road project, hii inapitia Tabora yaani tutafaidika sana sisi wanyamwezi, naisubiri hii project kwa hamu kuu - kweli mtani ameamua kutuendeleza - lol

Nitamuuliza ndugu yangu Sikonge may be ana updates ya hizi project.
 
Sidhani kama Nape alikuwa serious. Labda anafanya utani, baadae ndio atakuja na uchambuzi halisi. Siwezi amini kabisa mtu unaweza kusimama mbele wa waandishi wa habari kisha utoe uchambuzi kama huo. Nasikitika kwamba kesho atachukua Headlines kwenye gazeti la Uhuru!
 
Hoja yake kwamba alitegemea kuona ahadi za CDM kwenye bajeti mbadala kama ambavyo tunategemea kuona bajeti za meli, barabara za juu na reli mpya kwenye bajeti ya serikali si ya kubezwa. Labda kitu alichosahau NAPE ni kuwa Serikali ya CDM isingekuwa na ukubwa wa Serikali ya sasa hivyo kwa kupunguza hivyo vyeo pesa nyingi ingeokolewa na kwenda kwenye huduma za jamii ikiwemo elimu bure. Embu fikiri kupunguza baraza la mawaziri la sasa toka takribani 50 mpaka labda 25 ni pesa ngapi ingeokolewa kwa maana ya mishahara na posho, wasaidizi wa waziri, ofisi/vitendea kazi, magari na gharama za kuhudumia hayo magari. Vile vile ukifuta vyeo vya wakuu wa mikoa na wilaya ni pesa ngapi itaokelewa.

Kitu muhimu cha kufahamu ni kuwa bajeti mbadala ya CDM imeandaliwa kwa kufuata mfumo wa sasa wa serikali.
 
Nape a.ka. ACHEBE ,

Unaonyesha dhahiri kuwa hujasoma hoja za bajeti mbadala , na unafanya propaganda za kitoto kwani ukisoma utaona mambo yafuatayo;
  1. kuhusu Elimu- CHADEMA imesema kuwa;
  • itaondoa ada kwa shule za kutwa ....hiyo maana yake ni elimu bure
  • kuwa wasichana wote shule za Bweni wataondolewa ada , hiyo maana yake ni elimu bure kwa wanafunzi wote wa kike sekondari.
  • kuhusu vyuo vikuu ....wamesema kuwa skills levy ipelekwe bodi ya mokopo .....ni kwa ajili ya kugharimia elimu bure na hizo ni zaidi ya 90 bilioni kwa mwaka changanya na zile 132 bilioni ..... elimu bure .
  • kuhusu shule za msingi inaonekana Nape hajui hata mfumo wa elimu wa Nchi hii kwani mpaka sasa anahoji mbona elimu ya msingi hakijazungumzwa kitu , anataka CHADEMA iseme nini ? kwani shule zote za umma anajua ada ya shule ni kiasi gani? hajui kuwa UPE imeondolewa siku nyingi? ni zuzu huyu.
  • asubiri hotuba ya waziri wa elimu ataona jinsi ya kuweza kufikia malengo hayo na aache kupotosha kama walivyopzoea.
2. Kuhusu vifaa vya ujenzi .
  • anangangania kuwa viongozi wengi wa CHADEMA wanapinga hoja ya nguvu kazi .....hajui mfumo wa nchi hii na hata hajasoma hotuba ya waziri wake kwani walianisha kuwa watahakikisha kuwa wananchi hawachangishwi kwani michango ni mingi kutokana na kila mfadhili kuacha kiasi fulani kichangiwe na ndio maana Mkullo akasema sasa wanarudisha ada za leseni za biashara kwenye vijiji na Halimashauri ili kuondoa michango. Kuhusu viongozi wengi wa CDM aseme ni yupi mmoja anayepinga michango halali , kwani mar zote ni kuwa CDM inapinga michango ya uongo na ambayo haina sheria yeyote inayosimamia michnagi hiyo na hivyo kuwa miradi ya watu na ndio maana mpaka leo hakuna mahesabiu popote kuwa mchango wa wananchi ni kiasi gani katika kujenga shule za kata.
3.Suala la kukwepa kodi.
huyu bado ni zuzu kwani anasema kuwa Dr.Slaa , kuwa yeye anakwepa kodi kwenye posho anayopewa ,..... inaonyesha hajasoma hata hotuba ya waziri Mkullo kwani anakuwa kama wale wabunge wa CCM ambao mara zote wamekuwa wakipinga suala la posho kuondolewa huku wakisema kuwa mpango ni mzuri na upitishwe bila kuusoma na kujua kuwa mpango umependekeza kufuta posho.

4.Kuhusu kima cha chini cha mshahara ...
anasema kuwa CHADEMA ni waongo kwani hawajasema hizo fedha zitatoka wapi .... asahau kuwa CDM wameongeza mapato ya ndani kutoka 6.9 trilion na kufikia 8.4 trilioni haoni kuwa hapo ni kupata fedha za kulipa wafanyakazi? Hajaona kuwa CDM wanasema kuwa PAYEE kodi ipungue kutoka 14% na kuwa 9% kwa wanaolipwa kiwango cha chini? na kiwango cha juu ipungue kutoka 30% na kuwa 27% na hiyo yote mapato yatapungua only kwa 20bilioni na hajaona vyanzo vipya vya mapato vya 1.905 trilioni vya nyongeza?

Nape .... unapaswa sasa uanze kujitegemea maisha yako na uhame nyumbani kwa baba Mkwe wako Brigedia Hemed pale jesus village CHANGANYIKENI ili uweze kuwa na maoni yanayojitegemea kwani uchambuzi wako ni wa ajabu na inaonyesha kuwa umeambiwa na wewe mbio mbio ukaenda kutoa tamko bila kujipanga na kusoma kilichomo .

Achebe , njoo ukijibu ntarejea maana kwa sasa nafanya kazi nyingine ......

Nawatakia uchambuzi mwema wadau.
 
ANCHEBE ,naamini nikikujibu wewe,utampelekea majibu NAPE kama vile ulivyotuletea "hoja" zake hapa:
Naamini msingi wa "hoja" ya Nape ni Ilani ya uchaguzi ya CHADEMA ambayo kwa bahati nzuri inapatikana kwa urahisi kabisa na ningetegemea mtu kama yeye ni lazima alipaswa awe nayo. Sina uhakika kama anayo kweli (maana upungufu kama huo si jambo la ajabu sana kwa viongozi wa aina hii). Na kama anayo na ameisoma vizuri basi ameleta hili andiko lake kwa makusudi mazima ya UPOTOSHAJI na kuwafanya watanzania woote wapumbavu na vipofu. (Ndio maana nilisema kwenye post yangu mwanzo kuwa kwetu huko nilikotoka kosa kama hili halisameheki).

Ukisoma katika dibaji ya ilani ya CHADEMA 2010 utaona mistari hii:
"Ilani hii sio ahadi, ni mpango wa kazi ambao tutautekeleza kama CHADEMA itapatiwa na wananchi ridhaa na nafasi ya kuongoza. Kwa ufupi, Ilani hii itakayobeba mwelekeo wa CHADEMA kama chama tawala kuanzia 2010-2015 ina lengo la kuomba ridhaa ya wananchi ili tuweze kuanza tena ujenzi wa taifa letu jukumu ambalo CCM imeliacha kwa miaka zaidi ya ishirini sasa. Tunataka kurudia jukumu la kwanza kabisa la taifa letu baada ya Uhuru na Muungano yaani kujenga Taifa la kisasa. Kama Baba wa Taifa alivyosema "maendeleo ni ya watu siyo vitu" tunaamini kabisa kuwa tukirudisha maono yenye kulenga maendeleo ya watu basi maendeleo ya vitu yataenda sambasamba kabisa na maendeleo ya watu hao.
Ilani hii ni dira na ni maono yenye kuthubutu.
Ni dira ya kutupeleka tunakotaka kwenda kwa ufanisi mkubwa na kwa muda mfupi zaidi na ni maono ya Tanzania gani tunayoitaka kuanza kuijenga ndani ya miaka hii mitano. Hii ni Ilani ya Mabadiliko, ni Ilani ya Matumaini, ni Ilani ya kimapinduzi.

Pitia kwenye red kwanza halafu kama utakuwa na swali nitakuwa tayari kujibu kwa kirefu zaidi. Najaribu kuepusha e-wastes walau.

"
Alichouliza;
1. Elimu bure iliyoahidiwa iko wapi?
2. Mpango wa kushusha bidhaa za ujenzi uko wapi?
3. Kweli cdm wanachukia wakwepa kodi kama wanavyodai?
4. Pesa za kupandisha mshahara ziko wapi na chanzo nini?

HAYA KWA WAUNGWANA HAPA NI MATUSI MFULULIZO, PENGINE NDIO MAJIBU......
 
Na hajui kwanini nae anaiita bajet5i mbadala badala ya kuiita bajeti ya serikali.
Huyu inaelekea huwa anabishana na kivuli chake kwamba nani kavaa vizuri,na kukicheka kwa kuwa na kibiongo bila kujua hata yeye asingekuwa nakibiyongo hata kivuli kisingekuwa nacho.

Na kwa akili ya nape ukimwekea kioo mbele yake anakunja ngumi kama jogoo.
 
Nape tupambane na mafisadi wetu kwanza.
Siamini kama hii statement imetoka kwa malaria sugu. Duh, ndiyo maana huwa nasema huyu jamaa ni muelewa lakini huwa anatoa hoja za hovyo hovyo kwa ajili ya kupotosha tu.
 
Nape a.ka. ACHEBE ,

Unaonyesha dhahiri kuwa hujasoma hoja za bajeti mbadala , na unafanya propaganda za kitoto kwani ukisoma utaona mambo yafuatayo;
  1. kuhusu Elimu- CHADEMA imesema kuwa;
  • itaondoa ada kwa shule za kutwa ....hiyo maana yake ni elimu bure
  • kuwa wasichana wote shule za Bweni wataondolewa ada , hiyo maana yake ni elimu bure kwa wanafunzi wote wa kike sekondari.
  • kuhusu vyuo vikuu ....wamesema kuwa skills levy ipelekwe bodi ya mokopo .....ni kwa ajili ya kugharimia elimu bure na hizo ni zaidi ya 90 bilioni kwa mwaka changanya na zile 132 bilioni ..... elimu bure .
  • kuhusu shule za msingi inaonekana Nape hajui hata mfumo wa elimu wa Nchi hii kwani mpaka sasa anahoji mbona elimu ya msingi hakijazungumzwa kitu , anataka CHADEMA iseme nini ? kwani shule zote za umma anajua ada ya shule ni kiasi gani? hajui kuwa UPE imeondolewa siku nyingi? ni zuzu huyu.
  • asubiri hotuba ya waziri wa elimu ataona jinsi ya kuweza kufikia malengo hayo na aache kupotosha kama walivyopzoea.
2. Kuhusu vifaa vya ujenzi .
  • anangangania kuwa viongozi wengi wa CHADEMA wanapinga hoja ya nguvu kazi .....hajui mfumo wa nchi hii na hata hajasoma hotuba ya waziri wake kwani walianisha kuwa watahakikisha kuwa wananchi hawachangishwi kwani michango ni mingi kutokana na kila mfadhili kuacha kiasi fulani kichangiwe na ndio maana Mkullo akasema sasa wanarudisha ada za leseni za biashara kwenye vijiji na Halimashauri ili kuondoa michango. Kuhusu viongozi wengi wa CDM aseme ni yupi mmoja anayepinga michango halali , kwani mar zote ni kuwa CDM inapinga michango ya uongo na ambayo haina sheria yeyote inayosimamia michnagi hiyo na hivyo kuwa miradi ya watu na ndio maana mpaka leo hakuna mahesabiu popote kuwa mchango wa wananchi ni kiasi gani katika kujenga shule za kata.
3.Suala la kukwepa kodi.
huyu bado ni zuzu kwani anasema kuwa Dr.Slaa , kuwa yeye anakwepa kodi kwenye posho anayopewa ,..... inaonyesha hajasoma hata hotuba ya waziri Mkullo kwani anakuwa kama wale wabunge wa CCM ambao mara zote wamekuwa wakipinga suala la posho kuondolewa huku wakisema kuwa mpango ni mzuri na upitishwe bila kuusoma na kujua kuwa mpango umependekeza kufuta posho.

4.Kuhusu kima cha chini cha mshahara ...
anasema kuwa CHADEMA ni waongo kwani hawajasema hizo fedha zitatoka wapi .... asahau kuwa CDM wameongeza mapato ya ndani kutoka 6.9 trilion na kufikia 8.4 trilioni haoni kuwa hapo ni kupata fedha za kulipa wafanyakazi? Hajaona kuwa CDM wanasema kuwa PAYEE kodi ipungue kutoka 14% na kuwa 9% kwa wanaolipwa kiwango cha chini? na kiwango cha juu ipungue kutoka 30% na kuwa 27% na hiyo yote mapato yatapungua only kwa 20bilioni na hajaona vyanzo vipya vya mapato vya 1.905 trilioni vya nyongeza?

Nape .... unapaswa sasa uanze kujitegemea maisha yako na uhame nyumbani kwa baba Mkwe wako Brigedia Hemed pale jesus village CHANGANYIKENI ili uweze kuwa na maoni yanayojitegemea kwani uchambuzi wako ni wa ajabu na inaonyesha kuwa umeambiwa na wewe mbio mbio ukaenda kutoa tamko bila kujipanga na kusoma kilichomo .

Achebe , njoo ukijibu ntarejea maana kwa sasa nafanya kazi nyingine ......

Nawatakia uchambuzi mwema wadau.
Nape = Achebe
 
Back
Top Bottom