Jiwe aliifirisi TTCLRipoti ya mwaka 2023 lakini waziri anazungumza ya 2018.
Debe tupu
Nape ane elimu ya kuungaunga aliyoipatia huko IndiaNape ana Elimu gani?
Nape akiwa kama waziri mwenye dhamana anapaswa kujikita zaidi katika kuzungumzia suluhu ya tatizo, zaidi ya kutumia muda mwingi kuelezea historia ya tatizo.Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ametaja sababu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kupata hati chafu mfululizo kuwa ni urithi wa matatizo ya hesabu za kifedha yaliyoanza wakiwa na mbia wao kabla Serikali haijarudishiwa umiliki wa shirika hilo.
Nape alisema hayo jana jijini Dodoma katika hafla ya utiaji saini mkataba wa upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika wilaya 23 nchini, ikiwa ni takribani wiki moja imepita tangu Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2021/22 kuwasilishwa bungeni na kuonyesha dosari kadhaa kwa T'TCL.
Miongoni mwa kasoro alizozibaini CAG, Charles Kichere ni TTCL lilikuwa na madeni ya Sh21 bilioni ambayo uongozi haukuweza kutambua wadaiwa husika. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, TTCL ni kati ya mashirika yaliyo na deni kubwa kuliko mtaji walionao, kwani ripotibilieleza shirika lina jumla ya deni la Sh349.9 bilioni huku likiwa na mtaji wa Sh227.8.
Katika hafla hiyo,Waziri Nape alisema hoja ya madeni vasiyo na vielelezo iliyoibuka ilianza katika ukaguzi wa mwaka 2017/18 ikiwa na deni la Sh91.43 bilioni.
Alisema shirika hilo lilirithi kutoka kwa iliyokuwa kampuni ya simu Tanzania
iliyoanzishwa mwaka 1994 na mwaka 2016 mbia alitolewa kwenye kampuni hiyo na kuwa shirika la simu Tanzania mwaka 2017 kisha shirika la mawasiliano Tanzania.
"Shirika limepitia mambo mengi ambayo yamekuwa na matokeo hasi na chanya, limekumbana na changamoto zinazotokana na historia.
Mfano wakati wa ukaguzi 2017/18 kuna tofauti kubwa kati ya hesabu zilizoonekana kwenye mfuko wa anka-ra na mfumo wa hesabu.
Awali, akizungumza utiaji saini mkataba wa upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa kilomita 1520 katika wilaya 23 kati ya shirika hilo na Kampuni ya Huawei, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la mawasiliano Tanzania, Peter Ulanga alisema mradi huo utakamilika kipindi cha miezi sita.
Alisema mradi huo utakaogharimu Sh37.4 bilioni, utakwenda kumaliza changamoto katika maeneo yaliyokuwa hayana mawasiliano, ili kuongeza matumizi ya Tehama, mitandao na kuboresha uchumi. "Kupitia upanuzi huu, kampuni za mawasiliano zitapata fursa za kibiashara ukizingatia tunaelekea katika mkakati wa kuunganisha mkongo na nchi jirani na hii itatusaidia kukuza uchumi na biashara nchini" alisema Ulanga. Ulanga alizitaja wilaya hizo
Kuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Mbogwe, (Shinyanga), Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Muheza, Kilindi, Mombo, Lushoto (Tanga), Ngara (Kagera), Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga na Hai (Kilimanjaro), Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Longido, Mbulu (Arusha).
Pia Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti (Pwani), Halmashauri ya Wilaya ya Mtama, Ruangwa, Nachingwea (Lindi), Halmashauri ya Wilaya ya Newala (Mtwara), Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga (Ruvuma), Wilaya ya Ludewa (Njombe) na Halmashauri ya Wilaya ya Vwawa, Ileje mkoani Mbeya.
Tanzania tumelaaniwa. Huyu Hata ubalozi wa nyumba kumi hayoshi anapewa uwaziriNape ane elimu ya kuungaunga aliyoipatia huko India
sidhani kama nape anajua lolote kuhusu mambo ya finance.kwani ukirithi hesabu za nyuma ambazo tayari zilikaguliwa ndo inapelekea kuleta hayo madudu?inawezekanaje kuwe na deni halafu usimjue anayekudai.hiki ni kichekesho cha mwaka. hapa ni issue ya debit na credi tu kitu ambacho hata book keeper anajua sasa iweje watu wenye CPT (T) washinde kuikamilisha hiyo transactin ndogo tu?hapa napata shida na inawezekana ndo matatizo ya kuajiri vyeti na si ujuzi.haya mabodi sijui ya uhasibu,ugavi,ufamasia nk ni miradi tu si chochote wala lolote.tukubali kurudi tulikotoka.si vibaya kupiga U- Turn.Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ametaja sababu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kupata hati chafu mfululizo kuwa ni urithi wa matatizo ya hesabu za kifedha yaliyoanza wakiwa na mbia wao kabla Serikali haijarudishiwa umiliki wa shirika hilo.