Nape asema CHADEMA ni FISI

Nape asema CHADEMA ni FISI

Mie saiv simlaumu nepi, pata picha akili za nepi, nkamia, makonda, mhita, alaf niambie je aliyewachagua hawa watu atakua na akili gani sasa 😂😂😂
 
Nape acha ujinga mkuu anayetaka nchi isitawalike kwa taarifa yako ni EL ole wenu mwumpige chini patachimbika
 
Mie saiv simlaumu nepi, pata picha akili za nepi, nkamia, makonda, mhita, alaf niambie je aliyewachagua hawa watu atakua na akili gani sasa 😂😂😂

Umesema MHITA.....yupi huyo..?? Unataka kuniambia yule mbunge mjane wa Kondoa...(Allah ampe subra wakati huu akiwa eda)
 
Nape n pakapori! Au paka jizi! Hana hoja nawasikitikia wanaopoteza muda wao kumsikiliza polen sana
 
Waroho wa madaraka ni CCM, ambao kwao, kila mtu anataka Urais!
 
Hivi shirika la mali asili na utalii mpaka wapate ushahidi wa namna gani?.
KIJAZI amka usingizini,hawa jamaa wote wakamatwe watueleze wana mahusiano gani na hawa FISI.
 
Katibu wa Uenezi wa CCM Mheshimiwa Nape Nnauye amewaita wapinzani wao CHADEMA kuwa ni fisi waliovamia sherehe isiyowahusu. Nape alisema kuwa FISI wanataka nchi isitawalike, wanataka damu imwagike kwa kujawa na uroho wa madaraka walionao.

Nape amesema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa stendi Kata ya Izigo Wilayani Muleba ambapo vijana wa upinzani walikuwa wamesimama pembeni wakinung'unika.

Katika kumalizia hotuba yake jukwaani hapo, Nape amesema kuwa Ikulu hawatakwenda wapinzani abadani, na kwamba mwaka huu ushindi wa CCM utaongezeka kufikia zaidi ya asilimia 80%

Baada ya muda kidogo nitapandisha video.


Nape na scandals ndiyo kama oxygen na binadamu hai duh !!!!
 
Nape anahitaji intensive counselling ili kuamini CCM hawana chao tena,..
 
Tangu ilipokuwa imetolewa ratiba ya kutangaza nia ya urais nimekuwa nikimsikiliza kila mtangaza nia ya urais laikini kuna mambo kadhaa mimi binafsi sija ya elewa.Nitayaeleza machache kama ifuatavyo.

1.Wapo waliojinadi kukomesha RUSHWA na UFISADI, lakini hawajatuambia kama mafisadi Tanzania wapo au hawapo;kama ni wapo ni akina nani? na kwa nini mpaka leo hawajukuliwa hatua? kwa sababu baadhi ya hao watangaza nia mawaziri au nyadhifa nyingine serikalini au ni wastaafu ambapo walikuwa na nafasi ya kumsaidia rais kukomesha hiyo hali.

2.Kwa wale walioko kwenye nyazifa zao bado au wanafanya hivyo kumuhujumu rais wao aonekane ameshindwa? au wametunza hayo matatizo kwa makusudi ili iwe ndiyo gia ya kuomba urais?

3.Baadhi yao tunawaona kule bungeni kwa nguvu zote wakitetea UFISADI leo wanakuja na wimbo huo huo kuutaka urais;hivi wanatufanya watanzania ni watu tusiyo na fikra?

4.Baadhi ya wataka nia ni Mawaziri waandamizi na wastaafu ambapo mikataba yote mibovu inayolinyonya taifa imefanyika wao wakiwa madarakani;sisi tutawaaminije kuwapa nchi tena kwa mara ya pili?

5.Baadhi ya watia nia tunaona kabisa huku mikoani jinsi wanavyotumia fedha nyingi kukodi watu,lakini wanadai ni za marafiki zao,hao marafiki zao malipo yao ni nini baada ya kupata urais? je, hao marafiki ni wa ndani au wa nje?

6.Baadhi yao wamemshauri vibaya kabisa rais kiasi cha kutumia pesa nyingi katika katiba na katiba haijapatikana;je hao ndiyo wanafaa kupewa urais?

7.Wapo wanaojinadi watafanya maamuzi magumu wakipewa urais;lakini hawasemi ni aina gani ya uamuzi mgumu amabao wataufanya kama katika viwanda,elimu,ulinzi,kilimo,mi undombinu nk; na wengine bado wako kwenye nafasi hizo lakini hawawahi hata kushauri rais afanye hivyo; je leo ndiyo wataweza wakipewa urais?

MAONI YANGU:
Watanzania sasa wanataka rais anayeweza kushughulikia maswala yanayo mgusa mwananchi moja kwa moja siyo porojo.

1.Mfumo wa elimu ni mbaya kabisa hauandai mhitimu kujiajiri

2.Ardhi ni kilio cha watu kila kukicha,wanyonge wanaporwa ardhi viongozi wakok kimya

3.Mazao ya wakulima yanaoza majumbani

5.Afya mbaya.watu binafsi maduka yao yana dawa,serikali hakuna

6.Barabara za halmashauri zetu ni mbaya na kama zina jengwa ni kwa chini ya viwango

7.Kodi watu hawalipi,wameachiwa watumishi,serikali iko kimya

8.Maji safi na salama hakuna.maeneo mengine mto mkubwa upo chini ya km 50 na makazi ya watu lakini watu hawana maji ya bomba,

Haya ni machache tu lakini watia nia haya hata hawasemi.
Mungu ibariki TANZANIA
 
Mamburula wamejisahau!!!!!na asiwepo mtu wa kuwashtua hadi watakapo nyanyuliwa kuwapisha UKAWA Ikulu
 
ni mtazamo wake japo nadhani imetokana na hofu juu hali inavoonekana kuwakaba
 
Wawaulize meli mpya vipi au mwenyekiti wao alikuwa viroba wakati anaihaidi 2010? Hapo hawataropoka tena!!!
 
Waroho wa madaraka ni CCM, ambao kwao, kila mtu anataka Urais!

ausemayo yanaukweli.Tumeshatangaza NIA wanachana 24,ni mategemeo yetu sababu ya democrasia tuliyonayo ya kujilimibikizia mali za wizi watafuta kazI hawa muda wowote wanaweza kufika 30...Du hii lazima iingie kwenye kitabu cha guiness...
 
Sasa hivi amepanda Katibu Mkuu anaongea kuhusu kusambaza umeme vijijini...

Yaani wewe katika hotuba yake ya saa nzima, neno ulilolisikia ni FISI tu? Basi ndio maana ulifeli shule na umefeli maisha.
 
ole wao wakate jina la fisadi mwenzao lowassa,...
 
Back
Top Bottom