Nape apokelewa kishujaa SAUT Mwanza

Nape apokelewa kishujaa SAUT Mwanza

security guard

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
799
Reaction score
603
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipokelewa na umati wa watu kwenye eneo la mkutano Nyamalango ambapo atahutubia wanachama wa CCM Tawi la SAUT pamoja na wakazi wa maeneo hayo , pamoja na kuhutubia pia Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi atawapokea wanachama zaidi ya 30 wanaotoka Upinzani na kujiunga na CCM

Wanachama wa CCM SAUT wakionyesha ujumbe kutoka kwenye mabango

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipeana mikono na wanachama wa CCM SAUT kwenye uwanja wa Nyamalango.

Nifuraha kwa kila Mwana CCM SAUT wakati wa mapokezi ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye.

Ujumbe kutoka kwa Tawi la CCM SAUT

=========================================



  • Zaidi ya Watu 420 wajiunga na CCM
  • Wanachuo SAUT waahidi kudumisha Umoja wao na Ushirikiano
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wanachama wa Tawi la CCM SAUT Kambarage na wananchi wa Nyamalango ,wilaya ya Nyamagana Mwanza ambapo aliwaambia kuwa CCM itaendelea kuongoza kwani ndio chama pekee chenye sera inayoeleweka kwa wananchi,mipango na ahadi zake zinatekelezwa kila kona ya nchi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipokea kadi ya CHADEMA kutoka kwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Agustine Ndugu Simon Philbert Macheyeki ambaye amejiunga rasmi na CCM,katika mkutano huo zaidi ya wanafunzi 86 wa chuo hiko wamejiunga na CCM na wanachama wapya 420 wamejiunga na CCM.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimkabidhi kadi ya CCM Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine Ndugu Simon Philbert Macheyeki ambaye amejiunga rasmi na CCM,katika mkutano huo zaidi ya wanafunzi 86 wa chuo hiko wamejiunga na CCM na wanachama wapya 420 wamejiunga na CCM.
Kadi za wanachama wapya waliojiunga na CCM kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine Mwanza.
Wanachama wapya 420 wajiunga na CCM kutoka Chuo Kikuu cha SAUT Wilaya ya Nyamagana.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Agustine Ndugu Simon Philbert Macheyeki akila kiapo cha kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Nyamalango wilayani Nyamagana.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na wananchi na wanachama wa Tawi la CCM SAUT Kambarage Mwanza.
Wanachama wa Tawi la CCM SAUT wakiburudisha kwa kucheza na kuimba nyimbo mbali mbali.

 
Mbona CDM walinyimwa uwanja huko?Kulikoni?
 
ina maana hawa wote ------------ au cdm jana mlituaminisha tofauti
 
kuna waliopewa 20000 hao ndo wale unaowaona na mabango,,,,

kuna wa 10000:hao ndo utawaona wanashangilia sana,,

wapo walioahidiwa wali,maharage,,,
mi nimevuta 10000,,,,,,
 
mbona kijani imetawala hapo? Nadhani lilikuwa kusanyiko la viongozi wote wa magamba .ccm ina wanachama kiduchuu sana hapa SAUT na ukiwachunguza karibu wote ni watoto wa mafisadi na jangili.
 
headline kuuubwa content dhaiiiiiiiiifu, hiyo idadi hailandani na ng'ombe na mbuzi waliotolewa kuwahonga wanachuo kuhudhuria mkutano, halafu naona kama mko wenyewe tu mliovalia sare, tunawahesabu hao kama misukule
 
Mnavyosema mnampokea Nape sielewi mnamaanisha mini haswa, pokeeni maendeleo, fikra mpya, fursa mpya salsa ninyi mnabzki kumshabikia mpiga domo am aye serikali take imechoka.
 
Hiki ndicho chama tawala Tanzania! Safi sana Nape.
 
mkutano ulidoda sana pamoja na kusomba maccm katika maeneo yote ya jiji na kugawa nyama hapa chuoni.Nimepata taarifa hizi kutoka kwa swahiba wangu aliyeamua kuhudhuria ili kufanya udukuzi.
 
Safi sana NAPE, Endelea kueneza sera madhubuti za Chama cha mapinduzi.
Watanzania wazalendo tutaendelea kuwasapoti kwa hali na mali.
 
CHASO SAUT fukuzeni wasaliti wote,pamoja na huyo ''rais'' mtoeni madarakani maana alishinda kwa kutumia mvuto wa cdm.
 
hivi yule demu alipiga picha za uchi wa hapo sauti mwanza (nsia swai) yupo? people graduated but still stupidy
 
Safi sana NAPE, Endelea kueneza sera madhubuti za Chama cha mapinduzi.
Watanzania wazalendo tutaendelea kuwasapoti kwa hali na mali.
Wahandishi wa habari yericho nyerere ben sanane na wengine wanne wapewa pikipiki.
 
mimi npo saut hapakuwa na shamrashamra zozote tofauti na alivyokuja slaa na halima mdee
 
Kuna ujinga mwingine kama siyo mjinga
huwezi kupost, utafikiri wako sendoff!
 
Nipo hapa saut Nape ana watu wachache sana kwa msiba wa jirani
 
magamba hamjielewi kweli cku ya leo nimesikia watu wanasema pesa tukipewa na ccm tunachukuwa 7bu ni kodi zetu ila kura hawapti hata mimi npo tayar kupokea money but kura ni ndoto 2015.
 
Back
Top Bottom