Nape apendekeza Msajili wa vyama kufuta CHADEMA

Nape apendekeza Msajili wa vyama kufuta CHADEMA

Nape na ccm ni kama Ng'ombe na Kupe:

Ng'ombe anachinjwa, Kupe hana habari!

Ng'ombe anachunwa, Kupe hana habari!

Ngozi inawambwa, Kupe hana habari!

Ngozi ikianza kukauka, kupe ndo anastuka!

Alaa! Huyu ngo’mbe kumbe keshachinjwa!

mkuu nimecheka saaaana baada ya kusoma hiyo! hii sms nzito!
 
Yaani ni kama mashabiki wa man utd walilie kufukuzwa kwa kocha wa Arsenal...hahahaaa na mimi nilihisi muda mrefu haya mambo ya uchaguzi ni CCM wanalilia...hivi Nape umeshawahi kusikia uchaguzi wa TLP...? Chadema inawakosesha usingizi magamba..
 
Nape na ccm ni kama Ng'ombe na Kupe:

Ng'ombe anachinjwa, Kupe hana habari!

Ng'ombe anachunwa, Kupe hana habari!

Ngozi inawambwa, Kupe hana habari!

Ngozi ikianza kukauka, kupe ndo anastuka!

Alaa! Huyu ngo’mbe kumbe keshachinjwa!
Kwali mkuu hapo umelenga penyewe kabisa!
 
Kuna mtu anapigiwa chapuo awe mwenyekiti wa CHADEMA kwa gharama na mbinu za CCM.

Kuna kipindi Mwakyembe alilalamika na kuandika hadi barua kwa IGP kuwa anataka kuuliwa na akaambatanisha na ushahidi kabla ya saga la sumu na kupewa uwaziri,lakini hakupewa ulinzi!!


Kuna kipindi Magufuli alitishiwa kuuawa kutokana na operation bomoabomoa na akaomba apewe ulinzi,lakini hakupewa. Na wapo wakina Slaa na mbowe pia lakini hawajawahi kupewa ila cha ajabu anatokea mtu mwenye makashifa lukuki anaitwa na polisi na kupewa ulinzi,tukisema huyu mtu wenu mmemnunua na mnampa mapesa na madaraka aue upinzani mnaleta upu.mbavu,haitoshi mnalazimisha apewe na chama kwa ghiliba za demokrasia, maza fanta!!!
 
Ni kama kocha wa timu pinzani anakwambia umechelewa kufanya SUBSTITUTE

Hii ni ajabu na kweli na wakati mwingine ni vigumu kuamini kuwa imetolewa na kiongozi mkubwa na alieingia darasani !!?ama kweli kuwa uyaone !!! Au huyu jamaa ndiye anasoma magazeti na kusiliza redio naTv peke yake !!? Kilichofanywa na CDM mwaka 2009 kilikuwa nini kama si uchaguzi ni nini??!! Na 2014 imeshapita. Nakubaliana na kauli ya Dr Mengi watu wengine inabidi wapelekwe milembe kwa nguvu.
 
Hii ni ajabu sana, Nape anashindwa kuwaeleza wananchi ni nn watanzania wamefanyiwa na chama chake kwa zaidi ya miaka hamsini sasa wakati matatizo yaliyokuwepo kipindi cha miaka hamsini tangu uhuru ndio yale yale
Nape kufanya CDM sehemu ya hotuba yake ni aibu kubwa sana na ni ishara mbaya kwa chama tawala
 
Kwani alipendekeza kuanzishwa kwa CDM. Muwasho mwingine mubaya mpaka mtu anaropoka bila kujua. Nawaambia huu ----- utawandama mpaka 2015.
 
Hahaaaaaaaaaaaaaaa!

Asante CHADEMA chama changu,

Watu wanaweweseka kila wanapojaribu kukuwaza.

Hahahahaaaa Nape anataka kugombea nafasi gani mbona analilia uchaguzi wa Chadema, wakati muda wake bado.. Tulifanya uchaguzi 2009 na awamu nyingine ni mwakani 2014.. wanalialia nini sasa CCM..
 
COLOR=#000080 said:

Kuhusu malalamiko ya wananchi, Nape alisema wananchi wamekuwa wakilalamikia utendaji mbovu wa viongozi wa Serikali na kwamba, yana msingi kwani inasikitisha licha ya Ruvuma kuwa ni mkoa unaolisha nchi, hakuna mawazili wa kilimo ambao wamefika mkoani hapa.
[/COLOR]

[/FONT][/COLOR]

Nimependa sana hii statement ya mwisho baadae ya Pirijo nyiiiiingi mwisho anashindwa kujitetea Chama chair kwa wana nchi kwani hoja ya naingia ni uwajibikaji wa serikali ya ccm and poor nape ana ischia kuku bail kuwa mawaziri hawajawahi fika huko!! Sa Sonora asingeenda hata kwenye hiyo ziara jaman!!! Unajua inaishia Nepi
 
tatizo Nape anataka uchaguzi wa Chadema utafikili yeye ni mwanachama, sisi wanachama tumesema mpaka chaguzi kuu zipite sasa yeye anataka kutulazimisha sijui amepanga kufanya nini hapo
 
nepi mjinga sana yeye chadema inamuumiza sana akili ccm ndo inatakiwa kufutwa wabakaji wakubwa
 
Ila hasemi wanafunzi wakifeli CCM ifutwe!
Wala hasemi watu wakikosa maji CCM ifutwe!
Nape bwana!

Ndugu yangu huyo Nape hamnazo wala hawasemi Mwingulu akiua tena ccm ifutwe wala Kapuya mbakaji wakishindwa kumkabiki ccm ifutwe wala hasemi waking'oa watu kucha na meno ccm ifutwe.
 
CDM haiwezi kufanya uchaguzi sasa kwani kilichotokea kwa shibuda kuchukua uwenyekiti kina weza kutokea kwa zito kuchukua uwenyekiti Taifa .wanajua kabisa sasa Dr slaa na Mbowe hawezi kupona.Mbowe hayupo tayari kuona maslahi yake na watu wake moshi yanachezewa . Kwani mbowe bado hadi leo amajilipa gharama zake za uchaguzi .

MAZOMBI YATAENDELEA KUCHANGISHWA PESA KWA OPERATION ZISIZO KUA NA KICHWA WALA MIGUU MFANO ,M4C,MASANGARA,SATO,KIBUA,PEREGE,DAGAAA HIZO ZOTE NI NJIA ZA KUKUSANYA PESA MWENYEKITI AKAMALIZIE KASINO ..
 
KITAIFA
[h=1]Na Joyce Joliga, Mwananchi[/h]Posted Jumanne,Novemba19 2013 saa 24:0 AM
KWA UFUPI
Nape licha ya kukiandama Chadama alisikitika hakuna waziri wa kilimo aliyewahi kwenda mkoani Ruvuma.



Songea.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kukifuta Chadema kwa madai kuwa, kimeshindwa kusimamia katiba yake kwa kutofanya uchaguzi wa ndani zaidi ya miaka zaidi ya kumi.



Nape alisema chama hicho kimejaa viongozi waongo, wapenda vurugu na wanaotaka kuvuruga amani ya nchi kwa kisingizio cha Katiba Mpya na kwamba, wamesahau katiba iliyopo imedumu kwa miaka 50 na haijawahi kuwagombanisha wananchi wala kuwavuruga.



Hata hivyo, jitihada za kumpata Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika kuzungumzia tuhuma hizo jana jioni kwa simu yake haikufanikiwa.



Akihutubia wakazi wa Manispaa ya Songea jana, Nape alimtaka Msajili wa Vyama vya Siasa kukiagiza chama hicho kufanya mkutano wa uchaguzi haraka kikigoma akifute na kwamba, asipofanya hivyo wao wataendelea kumsema na kumchukulia hatua.



Aliongeza CCM kilifanya uchaguzi wake 2012 na kupata viongozi wapya, lakini Chadema imeshindwa kusimamia katiba yake ambayo ilipeleka kwa msajili wa vyama na kuisajili kwa kuivunja wao wenyewe kwa kuendesha chama isivyo.



Nape alisema chama hicho hakifai kuongoza nchi, kwani kimeshindwa kusimamia katiba yake na kuifuata hakiwezi kuongoza wananchi.



“Kwa sababu Msajili wa Siasa ni mlezi wa vyama vyote vya siasa ikiwamo Chadema, namuomba akiagize chama hicho kifanye uchaguzi kwani wao wanajiita wanademokrasia wakati wanashindwa kufuata demokrasia kwa vitendo,” alisema Nape.



Kuhusu malalamiko ya wananchi, Nape alisema wananchi wamekuwa wakilalamikia utendaji mbovu wa viongozi wa Serikali na kwamba, yana msingi kwani inasikitisha licha ya Ruvuma kuwa ni mkoa unaolisha nchi, hakuna mawazili wa kilimo ambao wamefika mkoani hapa.



wala hakuna haja ya msajili kutia mikono yake CHADEMA. hiki chama kinajifia chenyewe ni suala la muda tu.
 
wala hakuna haja ya msajili kutia mikono yake CHADEMA. hiki chama kinajifia chenyewe ni suala la muda tu.

Masikini MSALANI bado unatumia noti za zamani angali noti mpya zipo.......Hebu njoo na tungo ingine bana....Unajua 2014 mtakosa tungo kabisa......Wekeni na kiporo bana..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom