Nape apendekeza Msajili wa vyama kufuta CHADEMA

Nape apendekeza Msajili wa vyama kufuta CHADEMA

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
KITAIFA
[h=1]Na Joyce Joliga, Mwananchi[/h]Posted Jumanne,Novemba19 2013 saa 24:0 AM
KWA UFUPI
Nape licha ya kukiandama Chadama alisikitika hakuna waziri wa kilimo aliyewahi kwenda mkoani Ruvuma.



Songea.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kukifuta Chadema kwa madai kuwa, kimeshindwa kusimamia katiba yake kwa kutofanya uchaguzi wa ndani zaidi ya miaka zaidi ya kumi.



Nape alisema chama hicho kimejaa viongozi waongo, wapenda vurugu na wanaotaka kuvuruga amani ya nchi kwa kisingizio cha Katiba Mpya na kwamba, wamesahau katiba iliyopo imedumu kwa miaka 50 na haijawahi kuwagombanisha wananchi wala kuwavuruga.



Hata hivyo, jitihada za kumpata Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika kuzungumzia tuhuma hizo jana jioni kwa simu yake haikufanikiwa.



Akihutubia wakazi wa Manispaa ya Songea jana, Nape alimtaka Msajili wa Vyama vya Siasa kukiagiza chama hicho kufanya mkutano wa uchaguzi haraka kikigoma akifute na kwamba, asipofanya hivyo wao wataendelea kumsema na kumchukulia hatua.



Aliongeza CCM kilifanya uchaguzi wake 2012 na kupata viongozi wapya, lakini Chadema imeshindwa kusimamia katiba yake ambayo ilipeleka kwa msajili wa vyama na kuisajili kwa kuivunja wao wenyewe kwa kuendesha chama isivyo.



Nape alisema chama hicho hakifai kuongoza nchi, kwani kimeshindwa kusimamia katiba yake na kuifuata hakiwezi kuongoza wananchi.



“Kwa sababu Msajili wa Siasa ni mlezi wa vyama vyote vya siasa ikiwamo Chadema, namuomba akiagize chama hicho kifanye uchaguzi kwani wao wanajiita wanademokrasia wakati wanashindwa kufuata demokrasia kwa vitendo,” alisema Nape.



Kuhusu malalamiko ya wananchi, Nape alisema wananchi wamekuwa wakilalamikia utendaji mbovu wa viongozi wa Serikali na kwamba, yana msingi kwani inasikitisha licha ya Ruvuma kuwa ni mkoa unaolisha nchi, hakuna mawazili wa kilimo ambao wamefika mkoani hapa.


 
Na kweli huo Uchaguzi unakihusu chama Tawala??? Mbona CUF haijawahi kufanya uchaguzi zaidi ya Miaka hiyo hiyo??

Hapo ndipo unapoona woote wanaolilia uchaguzi ndani ya CHADEMA NI CCM kutaka kuweka VIBARAKA; VIBEBERU; just for the sake of killing CHADEMA softly...

Chadema wanabadilisha wagombea urais zaidi hata ya CUF. Wanajua fika viongozi walioko sasa sio ndumila kuwili hauwezi kuwapa pesa; cheo; karanga ili tu wakidhalilishe chama chao labda waende kwa wenye njaa

Kwahiyo in a maana maongezi yooote hayo hapa jukwaani kwa miezi 10 ilikuwa ni wana CCM wanataka huo uchaguzi wa CHADEMA?

Nape… hakuna chama chochote duniani kinachochagua viongozi wake kama CCM Tanzania na CCCP CHINA
 
Only in CCM jamani!!! Eti adui wako anakushauri ubadilishe siraha za kumpigia coz unazotumia zimedumu kwa muda mrefu....nazidi kuamini intelligence is nothing to do with education,niliwahi kusikia eti nape ana masters,wakuu niambieni ali master vitu gani maana siielewi akili yake!
 
Aaah!! Kumbe wanasiasa hamnazo kabisa....!!

Inawezekana vipi ukadai haki itendeke kwa jirani yako wakati mwenyewe unakandamiza familia yako kila siku?


Sasa naamini kabisa watu wengi wanaotaka uchaguzi ndani ya CDM ni mamluki wa CCM...this is circumstantial evidence, and all persons in CDM who guns support from outside the party are squarely being used, with no doubt, by akina NAPE.
 
Nape na CCM yake wameshindwa kufanya kazi waliyotumwa na mwenyekiti wao ya kuzunguka nchi nzima kueleza kile kilichofanywa na CCM.Wameshindwa kueleza mafanikio yao wanamtaka msajili aifute CHADEMA.Nape ana zidi kutoa picha kuwa migogoro yote inayotokea CHADEMA inapangwa na CCM.
 
Nape na ccm ni kama Ng'ombe na Kupe:

Ng'ombe anachinjwa, Kupe hana habari!

Ng'ombe anachunwa, Kupe hana habari!

Ngozi inawambwa, Kupe hana habari!

Ngozi ikianza kukauka, kupe ndo anastuka!

Alaa! Huyu ngo’mbe kumbe keshachinjwa!

You are Highness kamanda Hiroshima
 
CDM haiongozwi kwa remote ya CCM! CDM ni chama makini kuliko anavyofikiria Nepi! Na uchaguzi ndani ya chama chetu tutafanya baada ya 2015

Mbona hawasikitiki CCM kuendelea kuongoza nchi???!
 
nape upo sahihi
tatizo chadema imeshindwa kutekeleza matakwa ya wanachama walio wengi.
maamuzi ya chama yameshakuwa ni ya viongozi wa ukanda flani.na waliobaki wanaogopa kudai uchaguzi kwa kuwa wataitwa wasaliti.
 
Only in CCM jamani!!! Eti adui wako anakushauri ubadilishe siraha za kumpigia coz unazotumia zimedumu kwa muda mrefu....nazidi kuamini intelligence is nothing to do with education,niliwahi kusikia eti nape ana masters,wakuu niambieni ali master vitu gani maana siielewi akili yake!
Ni kama kocha wa timu pinzani anakwambia umechelewa kufanya SUBSTITUTE
 
nape upo sahihi
tatizo chadema imeshindwa kutekeleza matakwa ya wanachama walio wengi.
maamuzi ya chama yameshakuwa ni ya viongozi wa ukanda flani.na waliobaki wanaogopa kudai uchaguzi kwa kuwa wataitwa wasaliti.

Kwani kazi ya viongozi ni nini?
Hap wanachama ni wa CCM si CDM!
MwanaCDM hawezi kupeleka malalamiko yake CCM....
 
Chadema isifutwe ila wafutwe viongozi wanaominya democracy ndani ya chama.
 
Waliokua wamewaandaa kugombea uongozi ndani ya cdm hawana nafasi. Kesho huyo kubwa jinga Nape atakuja na hoja kwamba Zitto lazima agombee uenyekiti nakama sivyo CDM IFUTWE.

Ila hasemi wanafunzi wakifeli CCM ifutwe!
Wala hasemi watu wakikosa maji CCM ifutwe!
Nape bwana!
 
Back
Top Bottom