wakimataifa.
JF-Expert Member
- Jun 7, 2015
- 1,625
- 558
Jembe la CCM Nape Mnauye leo amenifurahisha zaidi kwa kuwaambia ukweli CHADEMA ni chama cha mafisadi CCM si chama cha mafisadi CHADEMA wakitaka wawe wasafi wamfukuze Lowassa na mimi nasema hawana ubavu wa kumfukuza.
Nape amenukuliwa na kituo cha television cha AZAM TWO, akimjibu Tundu Lissu kuhusiana na kauli aliyoitoa kuwa ufisadi ni ajenda ya CHADEMA ya kudumu, Nape ameanza kumshambulia LOWASA , na akisema kuwa kama CHADEMA kina ajenda ya ufisadi kimfukuze LOWASSA.
Nimeshangazwa na uwezo mdogo alionao NAPE katika kujenga hoja kwa sababu zifuatazo,
(1) Kwa nafasi aliyonayo serikalini kwa sasa hakupaswa kuanza kumshambulia mtu badala ya hoja
(2) Hakupaswa kumtaja Lowassa kwani ufisadi wa LOWASSA hajuathibitishwa na Tume yoyote na hata mahakama yoyote
(3) Lowassa alishatoka ndani ya Chama Tawala na sasa yupo upinzani kama kulikuwa na kikwazo kumpeleka mahakamani kushindwa kumfikisha mahakamani kwa sasa maelezo au madai ya Nape ni kichekesho
(4) Nyuma ya LOWASSA kuna watanzania zaidi ya millioni sita kwa kiongozi kama hakupaswa kuendeeleza madai yasiyothibitishwa
(5) Ukiwa ni muda mchache tuu toka tuingie toka uchaguzi, Nape kama kiongozi hakupaswa kuendeleza siasa za wakati wa uchaguzi.
Nafikiri Lowassa anapaswa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya NAPE, ili aweze kuthibitisha madai yake