Peter Mwaihola
JF-Expert Member
- Jun 23, 2022
- 276
- 460
HISIA ZANGU, MAMBO HAYA KUMBEBA LISSU CHA
Baada ya chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA kutangaza mchakato wa uchaguzi wa viongozi wakuu wa chama umeibuka mjadala juu ya nani ataweza kushinda uenyekiti katika uchaguzi huo.
Mjadala unaendelea wakati ambapo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe na Tundu Lissu, makamu mwenyekiti wa chama hicho wote wakiwa wamechukua fomu kugombea nafasi ya uenyekiti.
Mengi yamezungumzwa sana na watu mbalimbali ndani na nje ya chama cha chadema juu ya kinyang'anyiro hicho.
Moja kwa moja katika mtazamo nayaona mambo hayacyanayoweza kumbeba Lissu dhidi ya Mbowe katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika januari hii 2025.
Mosi, Uthubutu wa Lissu kwenye muelekeo wa siasa za kiharakati unambeba kuelekea uchaguzi huo. Nimefanya utafiti mdogo kwa kuangalia maoni ya wadau wa siasa na wanachadema nchini kwa kipindi cha miaka kadhaa tangu uchaguzi mkuu wa 2020 wafuasi wengi wa chama cha chadema walionyesha kiu ya kuwa na chama chenye harakati zaidi kuliko siasa za maridhiano ambazo Mbowe anaamini.
Lissu alijitofautisha na mtazamo wa Mbowe kwa kujitenga na kukashifu maridhiano jambo ambalo linampa uungwaji mkono na wafuasi wengi wa chama pamoja na wanaharakati.
Pili, msukumo wa nje ya chama unamuweka mtegeoni Mbowe na kumpa njia Lissu. ukifuatilia kwa umakini katika fukuto hili la uchaguzi wanachama wengi wa chama cha Mapinduzi wanamuunga mkono Mbowe ili asalie kuwa mwenyekiti kwa faida ya kuwa Mbowe hana misimamo mikali kama Lissu.
Msukumo huu unawaamsha wanachadema wengi kujiuliza kuwa CCM haiwezi kuitakia mazuri chadema hivyo kumchagua Lissu ni vema zaidi ili akaichachafye CCM, chadema ishike dola.
Tatu, Ajenda za Lissu kuutaka uenyekiti zimenyooka na kukubalika zinakosa majibu sahihi kutoka kwa Mbowe na kambi ya wanaomuunga mkono.
Lissu ameahidi kuwa akipata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama atakijenga chama katika misingi ya uwazi, uwajibikaji, atakomesha rushwa na kubadilisha katiba ya chama ili kuweka ukomo wa madaraka na kukuza demokrasia ndani ya chama.
Hoja hizi hazijibiwi ipasavyo na upande wa Mbowe badala yake utetezi unaotolewa unamtaja Lissu kama msaliti na aliyekosa adabu kwa mwenyekiti hoja pekee inayomlinda Mbowe ni kuwa amekaa muda mrefu kukijenga chama ana nguvu ya kuendelea.
Jambo lingine ambalo moja kwa moja linampa nafasi Lissu dhidi ya Mbowe ni hisia za wanachadema baada ya uchaguzi kupita, wanachadema wengi wanaonyesha wasiwasi kwamba iwapo Mbowe ataendelea kushikilia nafasi ya uenyekiti, chama hicho kitakosa uhalali mbele ya umma katika kupigania mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi kwa sababu washindani wa chama hicho watatumia katiba ya Chadema isiyo na ukomo wanmadaraka kuhalalisha katiba ya jamhuri inayolalamikiwa.
Hivyo kumchagua Lissu inaonekana ndilo litakuwa suluhisho na safari mpya yenye matumaini katika madai ya mabadiliko ya kikatiba nchini.
Si hayo tu, ikumbukwe mwaka 2021 Mbowe alipokuwa anazungumza na wanachama wa chadema kanda ya magharibi alisema kwamba ikifika mwaka 2024 ataachia uenyekiti chadema, hii ilikua na maana kwamba ungekua mwisho wa uongozi wake wa miongo miwili ndani ya chadema.
Hisia zangu, mambo haya yanambeba Lissu uenyekiti chadema.