Nape Amdonyoa Lowassa?

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,829
4,164
Akirejea kauli za Mwalimu Nyerere, Nape amesema (namnukuu)..........

"Wapo watu leo watahangaika sana lakini hawatafanikiwa kwa sababu tu Mwalimu (Nyerere) alisema HAPANA!"
 
Kimilidzo

JF-Expert Member
Jan 3, 2011
1,346
594
Mbona hata JK alisemewa hapana na Mwalimu lakini akapata kwa hila??

Magamba hawana tena nafasi ya kuongoza hii nchi after 2015, hii CANNIBALISM waliyoianza sasa ndo itawamaliza,,
 
CR wa PROB

Senior Member
Sep 21, 2011
170
29
Kwa mtzamo wangu mimi kama niwekewe Lipumba na Lowasa namchagua Lowasa, kwani ni jembe la ukweli!! Tuombe mola uchaguzi ujao watanzania wawe na uelewa mzuri wa kuchagua kiongozi bali sio chama!
 
Mghaka

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
320
126
Katika vita ya ushindani upande mwingine hupata nguvu kwa gharama ya upande mwingine kuwa dhaifu nahii napenda kumkumbusha kijana wangu Nape alitambue. Kama utaambiwa upime CHADEMA na CCM ni chama kipi kinazidi kujiimarisha na chama kipi kinadhoofika jibu ni wazi CCM inadhoofika na CHADEMA kinaimarika sana. Tuache unafiki na ushabiki wa kijinga ni kwamba Watanzania mnataka hamtaki Lowasa ni mtaji kwa Rais ajae iwe anatoka CHADEMA au CCM sababu unazo sihitaji kuzieleza hapa. Lakini naweza kuyasema haya makubwa mawili. Moja CCM imguse Lowasa kama wanapinga, RA amekuwa chuma sembuse itakuwa Lowasa, na huo ndio utakuwa mwisho wao. Kama wakimuacha na kwa joto walilolipata Igunga itabidi ama timu yake imnadi mgombea wa CCM au watengwe waende Chama chochote wakaweke changamoto. Siku zote sheria inatukataza kuwahukumu watu bila kuwasikiliza, Lowasa aliwahi kupata nafasi Bungeni kujitakasa kuhusu madhambi yake lakini kwa kuzingatia uswaiba wake alikubali kubeba msalaba, kwamba na yeye angebebwa lakini inaonekana sasa anataka kutoswa hasa, jaribio hilo litamleta kwenye jukwaa na itabidi ajitetee mbele ya watanzania hapo moto ndipo utawaka na miale itaenda juu ya moshi tunaouona sasa na kuleta nuru ya kweli katika siasa za Tanzania.

Lowasa ni mchapa kazi, anadiriki kutoa maamuzi magumu wakati ukilazimu, lakini pia wakati anafanya hivyo husukumwa na mahitaji yake binafsi. Kama ni kwa gharama ya kumbeba Lowasa ili nchi hii ipate ukombozi wa kweli mimi sijali, nipo tayari kupanda mgongo wa nyoka nivuke mto, hatutafuti ukombozi wa mtu tunatafuta ukombozi wa nchi, tutapokea sadaka na msaada wa aina yoyote na kwa mtu yeyote maadamu mwisho wa siku anakuwa katika mfumo tuliouweka sisi. CDM tusijadili nani tunamhitaji, tujadili tunahitaji nini ili kuikomboa nchi hii. muovu mmoja Lowasa ni afadhali kuishi nae na kufanya nae kazi kuikomboa nchi hii kuliko kuiacha mikononi mwa CCM. Lowasa, muovu mmoja ni rahisi kusafishika kuliko CCM kwa sababu ndani yake kuna mamillioni ya wanachama wake na familia zao na marafiki zao wote ambao wanawaza kuifisadi nchi hii kila kukicha.
 
mharakati

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,271
391
tatizo huyu Lowassa ataweka ma yes man kibao na wana maslahi binafsi wenzanke ambao hawezi kuwadhibiti kwa umakini..fikiiria miaka 10 ya kufukuza watumishi wadogo wadogo kwenye tv, kufukia mjadala wa katiba mpya, kutofanya mabadiliko yeyote ya maana katika sekta ya madini, kilimo, elimu ya juu, n.k kwa kifupi sioni maajabu ya rais Lowassa zaidi ya kuendeleza haya ya Kikwete toa labda hatakua na uswahili mwingi lakini msitegemee mabadilko ya kiutendaji seriakli zote za CCM zimekua hivyo hivyo.
 
naninibaraka

JF-Expert Member
Oct 13, 2011
912
667
Naamini Lowassa kwa uchapakazi hawezi kuchagua ma yes man kama Jk,jamaa mfuatiliaji sana hataki uzembe kama unaondelea sasa hv serikalini
 
Majala Kimolo

JF-Expert Member
Aug 3, 2007
342
39
Kwani kampeni za Urais 2015 zimeshaanza??
Ndyo! tena si urais tu, ni pamoja na Ubunge, udiwani na Uspika pia. Amini nakwambia kuna magamba mengi ndani ya sisiem yamesubiri mpaka yanachoka yanatangaza wazi hata kwa kuhamia CDM tutagombea, tunatoswa hivihivi tunaona! Chama hakiwezi kupewa mtu kama Nope, sharobaro, hana hoja nzito, kazoea mipasho na kuropoka hajui kesho ataulizwa swali gani ambalo jibu lake lilitakiwa litoke leo. JK na jamaa zake wamechemsha. Nusra yao ni kuruhusu Mgombea binafsi, nasema hivi kwa sababu, mwisho wao watatiwa kitanzi na CDM. Wameona mziki ulivyokuwa mnene, mtu kama Nope haweza kufanya utafiti, yeye ni mic tu ya JK. Wanapata Ruzuku hawazipeleki kwenye utafiti. Siasa ni sayansi na sio urithi kutoka kwa baba. Utafiti niliofanya unaonyesha mabadiliko ya kasi kuelekea kuanguka kwa sisiem iliyoshindwa kupata viongozi thabiti (Angalia safu yao imejaa watu tepetepe)
 
Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
11,270
20,110
Lowassa anawanyima usingizi sana akina Nape. Wanajua kwamba kwa kuwa hatuna tume ya taifa ya uchaguzi (maana iliyopo ni taasisi ya CCM), kama Lowassa atapitishwa na CCM, basi atakuwa Raisi wetu come 2015.

Hivi kwa nini CHADEMA hawafanyi harakati za kuhakikisha inaundwa tume huru ay Uchaguzi? Kusubiri uchaguzi ufanyike harafu kuja kulalamika baada ya matokeo (kama Igunga..) si sawa kabisa.
 
mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,680
249
Katika vita ya ushindani upande mwingine hupata nguvu kwa gharama ya upande mwingine kuwa dhaifu nahii napenda kumkumbusha kijana wangu Nape alitambue. Kama utaambiwa upime CHADEMA na CCM ni chama kipi kinazidi kujiimarisha na chama kipi kinadhoofika jibu ni wazi CCM inadhoofika na CHADEMA kinaimarika sana. Tuache unafiki na ushabiki wa kijinga ni kwamba Watanzania mnataka hamtaki Lowasa ni mtaji kwa Rais ajae iwe anatoka CHADEMA au CCM sababu unazo sihitaji kuzieleza hapa. Lakini naweza kuyasema haya makubwa mawili. Moja CCM imguse Lowasa kama wanapinga, RA amekuwa chuma sembuse itakuwa Lowasa, na huo ndio utakuwa mwisho wao. Kama wakimuacha na kwa joto walilolipata Igunga itabidi ama timu yake imnadi mgombea wa CCM au watengwe waende Chama chochote wakaweke changamoto. Siku zote sheria inatukataza kuwahukumu watu bila kuwasikiliza, Lowasa aliwahi kupata nafasi Bungeni kujitakasa kuhusu madhambi yake lakini kwa kuzingatia uswaiba wake alikubali kubeba msalaba, kwamba na yeye angebebwa lakini inaonekana sasa anataka kutoswa hasa, jaribio hilo litamleta kwenye jukwaa na itabidi ajitetee mbele ya watanzania hapo moto ndipo utawaka na miale itaenda juu ya moshi tunaouona sasa na kuleta nuru ya kweli katika siasa za Tanzania.

Lowasa ni mchapa kazi, anadiriki kutoa maamuzi magumu wakati ukilazimu, lakini pia wakati anafanya hivyo husukumwa na mahitaji yake binafsi. Kama ni kwa gharama ya kumbeba Lowasa ili nchi hii ipate ukombozi wa kweli mimi sijali, nipo tayari kupanda mgongo wa nyoka nivuke mto, hatutafuti ukombozi wa mtu tunatafuta ukombozi wa nchi, tutapokea sadaka na msaada wa aina yoyote na kwa mtu yeyote maadamu mwisho wa siku anakuwa katika mfumo tuliouweka sisi. CDM tusijadili nani tunamhitaji, tujadili tunahitaji nini ili kuikomboa nchi hii. muovu mmoja Lowasa ni afadhali kuishi nae na kufanya nae kazi kuikomboa nchi hii kuliko kuiacha mikononi mwa CCM. Lowasa, muovu mmoja ni rahisi kusafishika kuliko CCM kwa sababu ndani yake kuna mamillioni ya wanachama wake na familia zao na marafiki zao wote ambao wanawaza kuifisadi nchi hii kila kukicha.

Mawazo haya ni mtu anayefiki kwa ya masaburi, ni sawa na mtukuza majini au mvukuza upepo.Kwa kuwa ni mbishi ngoja tumtose Lowassa wako uone CCM asilia itakapoimarika.
 
Mghaka

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
320
126
Mawazo haya ni mtu anayefiki kwa ya masaburi, ni sawa na mtukuza majini au mvukuza upepo.Kwa kuwa ni mbishi ngoja tumtose Lowassa wako uone CCM asilia itakapoimarika.

Huna hata chembe ya kuwa mmoja wa watu wanofikirisha kichwa, unaleta ubishani wa maneno ya kichangudoa badala ya kuja na hoja ambazo zinaonyesha Lowasa ni dhaifu anaweza kushughulikiwa kama unavyotaka wakati wowote na chama cha mafisadi. Wewe unaesema hivyo haupo hata kwenye orodha ya watoa maamuzi wa CCM ambao ndio wanaouona mlima mrefu kuupanda (kumshughulikia Lowasa). Time will tell who is right btn you and me. Si kwamba Lowasa ni chuma kiasi kwamba hakiwezi kuyeyuka katika joto kali, lakini kwa CCM kumchuna Lowasa gamba bila kuwachuna Kikwete na makada wengine katika chama na serikali kwa akili za kawaida ni ngumu kama kufa na kufufuka kwa mawanadamu wa kawaida. Sisi wenye kumbukumbu za kawaida tunakumbuka Rais kikwete alivyohangaika kumsafisha na kumtetea Lowasa kwa yale yaliyomsibu na Richmond bungeni. Swali alimtetea kwa nini na kwa sababu ipi? Tunakumbuka jinsi CCM ilivyokebei hoja ya ufisadi, hivi ni nini kimejili na kuiamsha CCM kutambua ukweli? Mimi nahisi mwisho wa mtu kuwa kafara ili wengine waendelee kuneemeka unakaribia mwishooo! Na atakaye tufikisha hapo mwisho ni Lowasa atakaposimama na kusema Richmond saga ilikusudia kurejesha fedha ambazo CCM ilikopa EPA na kutumia katika kampeni iliyompeleka Kikwete Ikulu, siku ile yaja na si mbali sana kama hali ya hoja ya kujivua gamba itaendelea.
 
mambo

JF-Expert Member
Jun 11, 2007
2,374
5,588
Lowasa ameokoka anasali sana kwa joshua kule nigeria.akirudi mtajikuta wote mnampa kura za ndio ,ameenda kuwaweka sawa mumkubali
 
Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,519
6,084
Katika vita ya ushindani upande mwingine hupata nguvu kwa gharama ya upande mwingine kuwa dhaifu nahii napenda kumkumbusha kijana wangu Nape alitambue. Kama utaambiwa upime CHADEMA na CCM ni chama kipi kinazidi kujiimarisha na chama kipi kinadhoofika jibu ni wazi CCM inadhoofika na CHADEMA kinaimarika sana. Tuache unafiki na ushabiki wa kijinga ni kwamba Watanzania mnataka hamtaki Lowasa ni mtaji kwa Rais ajae iwe anatoka CHADEMA au CCM sababu unazo sihitaji kuzieleza hapa. Lakini naweza kuyasema haya makubwa mawili. Moja CCM imguse Lowasa kama wanapinga, RA amekuwa chuma sembuse itakuwa Lowasa, na huo ndio utakuwa mwisho wao. Kama wakimuacha na kwa joto walilolipata Igunga itabidi ama timu yake imnadi mgombea wa CCM au watengwe waende Chama chochote wakaweke changamoto. Siku zote sheria inatukataza kuwahukumu watu bila kuwasikiliza, Lowasa aliwahi kupata nafasi Bungeni kujitakasa kuhusu madhambi yake lakini kwa kuzingatia uswaiba wake alikubali kubeba msalaba, kwamba na yeye angebebwa lakini inaonekana sasa anataka kutoswa hasa, jaribio hilo litamleta kwenye jukwaa na itabidi ajitetee mbele ya watanzania hapo moto ndipo utawaka na miale itaenda juu ya moshi tunaouona sasa na kuleta nuru ya kweli katika siasa za Tanzania.

Lowasa ni mchapa kazi, anadiriki kutoa maamuzi magumu wakati ukilazimu, lakini pia wakati anafanya hivyo husukumwa na mahitaji yake binafsi. Kama ni kwa gharama ya kumbeba Lowasa ili nchi hii ipate ukombozi wa kweli mimi sijali, nipo tayari kupanda mgongo wa nyoka nivuke mto, hatutafuti ukombozi wa mtu tunatafuta ukombozi wa nchi, tutapokea sadaka na msaada wa aina yoyote na kwa mtu yeyote maadamu mwisho wa siku anakuwa katika mfumo tuliouweka sisi. CDM tusijadili nani tunamhitaji, tujadili tunahitaji nini ili kuikomboa nchi hii. muovu mmoja Lowasa ni afadhali kuishi nae na kufanya nae kazi kuikomboa nchi hii kuliko kuiacha mikononi mwa CCM. Lowasa, muovu mmoja ni rahisi kusafishika kuliko CCM kwa sababu ndani yake kuna mamillioni ya wanachama wake na familia zao na marafiki zao wote ambao wanawaza kuifisadi nchi hii kila kukicha.

nzuri lakini ndefu kweli na wewe khaa
 
Bigirita

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
15,866
7,161
Lowasa kabla ya kuwa premier, kwa nafasi za kisiasa alizokuwa amezishika, amewahi kufanya nini?

Tusiweweseke na aliyoyafanya Lowasa akiwa premier.....kabla ya hapo kafanya nini huyu 'tajiri'?
 
Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
2,953
3,281
Huna hata chembe ya kuwa mmoja wa watu wanofikirisha kichwa, unaleta ubishani wa maneno ya kichangudoa badala ya kuja na hoja ambazo zinaonyesha Lowasa ni dhaifu anaweza kushughulikiwa kama unavyotaka wakati wowote na chama cha mafisadi. Wewe unaesema hivyo haupo hata kwenye orodha ya watoa maamuzi wa CCM ambao ndio wanaouona mlima mrefu kuupanda (kumshughulikia Lowasa). Time will tell who is right btn you and me. Si kwamba Lowasa ni chuma kiasi kwamba hakiwezi kuyeyuka katika joto kali, lakini kwa CCM kumchuna Lowasa gamba bila kuwachuna Kikwete na makada wengine katika chama na serikali kwa akili za kawaida ni ngumu kama kufa na kufufuka kwa mawanadamu wa kawaida. Sisi wenye kumbukumbu za kawaida tunakumbuka Rais kikwete alivyohangaika kumsafisha na kumtetea Lowasa kwa yale yaliyomsibu na Richmond bungeni. Swali alimtetea kwa nini na kwa sababu ipi? Tunakumbuka jinsi CCM ilivyokebei hoja ya ufisadi, hivi ni nini kimejili na kuiamsha CCM kutambua ukweli? Mimi nahisi mwisho wa mtu kuwa kafara ili wengine waendelee kuneemeka unakaribia mwishooo! Na atakaye tufikisha hapo mwisho ni Lowasa atakaposimama na kusema Richmond saga ilikusudia kurejesha fedha ambazo CCM ilikopa EPA na kutumia katika kampeni iliyompeleka Kikwete Ikulu, siku ile yaja na si mbali sana kama hali ya hoja ya kujivua gamba itaendelea.

...Hili likitokea CCM na Watawala wake Kwishney! nadhani hii ndo inampa shida sana JK.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom