Nape alaaniwe kwa kutuita Boko Haram

Nape alaaniwe kwa kutuita Boko Haram

lolip

Member
Joined
May 19, 2014
Posts
19
Reaction score
0


Dodoma. Mbunge wa viti maalumu kwa tiketi ya CUF, Amina Abdallah Amour amemjia juu katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwa kuufananisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kundi la Boko Haramu na kutaka alaaniwe.

Ukawa iliundwa wakati wa Bunge Maalumu la Katiba na unahusisha wajumbe kutoka vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema na CUF.(Martha Mageesa)

Akizungumza bungeni mjini Dodoma juzi, mbunge huyo alisema kauli ya Nnauye ni ya uchochezi na inapaswa kulaaniwa.

Mbunge huyo alikuwa akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto kwa mwaka 2014/2015 iliyowasilishwa na waziri wake, Sophia Simba.

"Gazeti la Uhuru (jana) lilimnukuu Nape Nnauye akisema Ukawa ni sawa na Boko Haramu... Hii ni kauli chafu na ya uchochezi. Haikubaliki na ninailaani kwa nguvu zangu zote," alisema.

Mbunge huyo alihoji "wazazi wao hawajui watoto wao wanaishije, wanakula nini wala wanalala vipi.... Leo hii Nape Nnauye amethubutu kusema Ukawa ni sawa na Boko Haramu?"

Hata hivyo, wakati akihoji hivyo, baadhi ya Wabunge wa CCM nao walisikika wakihoji "na Intarahamwe Je?".

Ukawa ilitumia jina hilo la Interahamwe wakati mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akitangaza uamuzi wa kundi hilo kujitoa kwenye Bunge la Katiba, akiifananisha CCM na kundi hilo la nchini Rwanda.

Katika gazeti hilo, Nnauye amenukuliwa akisema Ukawa ni kundi hatari linaloeneza chuki na kusambaza uongo kwa Wananchi kwa nia ya kuwagawa na kusema silaha wanazotumia ni zaidi ya Boko Haramu.

Nnauye anadaiwa kutoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mkoani Tabora, akisema silaha za uongo wanazotumia viongozi wa Ukawa ni hatari zaidi kuliko silaha za moto zinazotumiwa na Boko Haramu.

Viongozi wa CCM na wale wa Ukawa wamekuwa wakizunguka nchi nzima kufanya mikutano ya hadhara kufafanua kile kilichojitokeza ndani ya Bunge la Katiba na kusababisha Ukawa kususia Bunge hilo.

Source: Mwananchi
 
watu uwa hawafikirii cha kuzungumza, ila wangekuwa wapinzani ungesikia wakamatwe.
 
Kumulaani Nape ni sawa na kupoteza laana pasipo faida.Nape alishalaaniwa toka zamani ndiyo maana kinywa chake hakiwezi kusema lililo jema hata siku moja.
 
Na Lipumba naye hastahili kulaaniwa kwa kuwaita wabunge wazalendo waliochaguliwa na wananchi kwa kura nyingi, Intarahamwe.
 
Kumulaani Nape ni sawa na kupoteza laana pasipo faida.Nape alishalaaniwa toka zamani ndiyo maana kinywa chake hakiwezi kusema lililo jema hata siku moja.

Hata hapa hakutajwa.......

BrigGen+NnauyeKisw.jpg
 
Huyo Nepi alishalaaniwa kitambo na hata familia yake ilishamlaani ndio maana hata katika watoto wa Mzee Moses Nnauye hakutajwa.
 
ukawa ni sawa na boko haram tu...ukawa ni ugaidi
 
huyu mwanamke si ndio yule ambaye hana mume aliyegombea umakam mwenyekiti wa bunge la katiba akaambulia pa tupu??
 
kwani kuna tofauti gani kati ya ukawa na boko haram.......ukiacha hii ya kwamba boko haram ni ya nigeria na ukawa ni ya tz
 
Huyo Nepi alishalaaniwa kitambo na hata familia yake ilishamlaani ndio maana hata katika watoto wa Mzee Moses Nnauye hakutajwa.
akili yako iko sawa na ya huyu mwanamke ambaye hana mume....huyo hapo kwenye maelezo ya mleta mada
 
Jamani huyo ni baba wa kufikia wala sio baba mzazi wa Nape,
 
akili yako iko sawa na ya huyu mwanamke ambaye hana mume....huyo hapo kwenye maelezo ya mleta mada

Mbona unanishambulia mimi wakati mimi sihusiki kabisa katika affairs the familia ya Mzee Moses Nnauye, sikuhusika kabisa katika tangazo lililotaja majina ya watoto ya mzee Nnauye. Acha kushambulia personality kama mwenyekiti wenu "dhaifu" amabaye alimshambulia Tundu Lissu.
 
akili yako iko sawa na ya huyu mwanamke ambaye hana mume....huyo hapo kwenye maelezo ya mleta mada

with your statements inaonyesha how weak you are. defense mechanism ni kusema hana mume, you have to think between the lines to come up with the point. poor you.
 
ccm ni chama cha wahuni na washenzi wakubwa wameishiwa sera boko haramu ni nape pamoja wanafiki wenzake ccm
 
BrigGen+NnauyeKisw.jpg


Hivi Nape ni mtoto wa Mnauye kweli ?.Nina mashaka sana haiwezekani watoto waandikwe,wakwe waandikwe,wajukuu waandikwe mtoto kubwa kama Nape asaulike.
 
Back
Top Bottom