Nape alaaniwe kwa kutuita Boko Haram

Nape alaaniwe kwa kutuita Boko Haram

BrigGen+NnauyeKisw.jpg


Hivi Nape ni mtoto wa Mnauye kweli ?.Nina mashaka sana haiwezekani watoto waandikwe,wakwe waandikwe,wajukuu waandikwe mtoto kubwa kama Nape asaulike.
Awe mtoto wa Nnauye au asiwe mtoto wa Nnauye wewe inakuhusu nini? Au unaathirika na nini Nape akiwa na ubini tofauti na Nnauye?
 
BrigGen+NnauyeKisw.jpg


Hivi Nape ni mtoto wa Mnauye kweli ?.Nina mashaka sana haiwezekani watoto waandikwe,wakwe waandikwe,wajukuu waandikwe mtoto kubwa kama Nape asaulike.
hili siyo swala la bahati mbaya, familia inaujuwa ukweli ku-adapt jina si swala la kukupa legitimacy ya DNA.

Hata rais Joseph kabila si mtoto wa marehemu Laurent kabisa. kwahiyo hao siyo wajinga na isitoshe Nape ni mkristo na Moses mnauye alikuwa mwislamu.
 
Msitokwe na mishipa ya Shingo kubishana juu ya chombeza za Kisiasa hayo majina nisawa na chachandu ktk mlo.
Iwepo isiwepo mlo utalika (Siasa itaendelea kuwepo).

Lakini, kama hoja ni wapinzani kutokuvutiwa na neno ama jina la 'BOKOHARAM'
Mbona tulishabikia sana pale Ma-CCM yalipoitwa 'INTARAHAMWE'???

Mi naomba tukubali tu; Sisi ni Ma-Bokoharam na wao ni Ma-Intarahamwe, Ama kinyume chake.

MNYONGE MNYONGENI LAKINI, HAKI YAKE MPENI,
Vinginevyo tuache tabia ya kuitana majina ya ajabuajabu na mwishowe wengine kushabikia Kushabikia.
 
Mi naona tz kuna baadhi ya watu wanatamani kuwe na vikundi vya kigaidi! aliwazalo mjinga ndio litakalomtokea!
 
Mimi nakubaliana na Nape kuwa hao jamaa hawana tofauti na Boko Haram,ingawaje siwaungi mkono CCm lakini nashangazwa na wanasiasa wa Tz walivyo malofa wa akili,wote tu hao ukawa na ccm ni majitu ya hovyo tu. Nilikuwa naangalia ITV siku za karibuni,Pro. Lipumba anatembea na kibabu kimoja chenye balaghashia ambacho kwa mujibu wa ITV wanamuandika muwakilishi kutoka Taasisi ya Kiislam. jambo la kushangaza Taasisi hiyo haina jina maana taasisi za Kiislam zipo nyingi tu na kila moja ina jina lake,sasa huyo BOKO HARAM anayetembea na hao jamaa wa UKAWA anatoka taasisi gani,hao ndio wachumia tumbo katika siasa za Tz,mtu kama huyo babu anatumika kuonekana kama vile taasisi za Kiislam zinawaunga mkono,kila taasisi iliishatoa maoni yake hicho kibabu cha BOKO HARAM hakijitambui. Jambo lingine nimemsikia Profesa eti akisema wanataka katiba ya meno ya kungata,jambo hili linashangaza,je Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na kina Warioba haina meno? maana mpaka sasa ni sehemu moja tu imejadiliwa nayo ni kuhusu Muungano,na hapa ndipo wanasiasa walipopata mwanya wa kutimiza malengo yao ya kuihujumu rasimu,nasema wote tu hata hao UKAWA hawakufurahia hiyo rasimu kwani ilipunguza sana utawala wa kiimla kwenye vyama vya siasa na ikwawaweka wananchi na wanachama huru ndani ya vyama vya siasa. hata sasa wanasiasa wote tu wanapita kwa wananchi kupiga blabla baada ya kulikimbia bunge la katiba,huko mlitakiwa muende mwisho wa siku kwani wananchi ndio watasema YES/NO. nakubaliana kabisa na Nape hao ni BOKO HARAM
 
Ugaidi haupo mbali sana Africa-mashariki, waulizeni Kenya wana hali gani saaizi! Badala ya kuconctrate ktk kutangaza amani, watu mnatangaza na kutukuza vikundi vinavyomwaga damu kila siku!?
 
BrigGen+NnauyeKisw.jpg


Hivi Nape ni mtoto wa Mnauye kweli ?.Nina mashaka sana haiwezekani watoto waandikwe,wakwe waandikwe,wajukuu waandikwe mtoto kubwa kama Nape asaulike.

Nape hoja ajue kuwa utete hakuna lami ,kisarawe hakuna lami,elimu dv 5, machinga wanafukuzwa aende kushughulikia hao kwanza ndipo tujadili maana ys bokoharamu na incidence yake
 


Dodoma. Mbunge wa viti maalumu kwa tiketi ya CUF, Amina Abdallah Amour amemjia juu katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwa kuufananisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kundi la Boko Haramu na kutaka alaaniwe.

Ukawa iliundwa wakati wa Bunge Maalumu la Katiba na unahusisha wajumbe kutoka vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema na CUF.(Martha Mageesa)

Akizungumza bungeni mjini Dodoma juzi, mbunge huyo alisema kauli ya Nnauye ni ya uchochezi na inapaswa kulaaniwa.

Mbunge huyo alikuwa akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto kwa mwaka 2014/2015 iliyowasilishwa na waziri wake, Sophia Simba.

"Gazeti la Uhuru (jana) lilimnukuu Nape Nnauye akisema Ukawa ni sawa na Boko Haramu... Hii ni kauli chafu na ya uchochezi. Haikubaliki na ninailaani kwa nguvu zangu zote," alisema.

Mbunge huyo alihoji "wazazi wao hawajui watoto wao wanaishije, wanakula nini wala wanalala vipi.... Leo hii Nape Nnauye amethubutu kusema Ukawa ni sawa na Boko Haramu?"

Hata hivyo, wakati akihoji hivyo, baadhi ya Wabunge wa CCM nao walisikika wakihoji "na Intarahamwe Je?".

Ukawa ilitumia jina hilo la Interahamwe wakati mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akitangaza uamuzi wa kundi hilo kujitoa kwenye Bunge la Katiba, akiifananisha CCM na kundi hilo la nchini Rwanda.

Katika gazeti hilo, Nnauye amenukuliwa akisema Ukawa ni kundi hatari linaloeneza chuki na kusambaza uongo kwa Wananchi kwa nia ya kuwagawa na kusema silaha wanazotumia ni zaidi ya Boko Haramu.

Nnauye anadaiwa kutoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mkoani Tabora, akisema silaha za uongo wanazotumia viongozi wa Ukawa ni hatari zaidi kuliko silaha za moto zinazotumiwa na Boko Haramu.

Viongozi wa CCM na wale wa Ukawa wamekuwa wakizunguka nchi nzima kufanya mikutano ya hadhara kufafanua kile kilichojitokeza ndani ya Bunge la Katiba na kusababisha Ukawa kususia Bunge hilo.

Source: Mwananchi

Simtetei Nape,lakini ili kuwa fair,mtu wa kwanza kulaaniwa anapaswa mwenyekiti wake huyu mama,yaani prof mapumba, wa CUF kwaani alikuwa mtu wa kwanza kuwaita CCM,INTARAHAMWE.
Lakini CCM hawakuhamaki,Sasa imekuwa mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu.
Nini tofauti ya INTARAHAMWE NA BOKO HARAMU,yote ni makundi ya mauaji,ya watu wasionahatia.
Mama muombe prof afute kauli,ili Nape nae AFUTE.
 
Awe mtoto wa Nnauye au asiwe mtoto wa Nnauye wewe inakuhusu nini? Au unaathirika na nini Nape akiwa na ubini tofauti na Nnauye?

Naona MSALANI Boss wako Kanangwa
 
Last edited by a moderator:
Huyu mbunge naye kilaza kweli kweli yaani Lipumba alivyowaita wenzake Intarahamwe alimlaani??
 
Ok tumewapata wengine intarahamwe wengine boko haram! Shame on you mnaotukuza haya majina
 
sasa ninaweza kusema nimechoshwa na siasa za Tanzania, kila leo kuna jipya yaani imekuwa kama vile mipasho ya hadija kopa na nasma kadogo.

huyu akiita intarahamiwe huyu anaita boko haramu alaf wananchi wanabaki kwenye lindi la umaskini, wasiokuwa na mwelekeo zaid ya kuona pesa zao za jasho lao zikitumbuliwa ndani ya jumba lenye kiyoyonzi, na watu wenye kauli chafu, za kashfa na za kibaguzi.

sijui ni kwanini sisi raia tumeacha hali ifike hapa makosa ni yetu wala sio ya awanasiasa wetu tumekaa kimya, tukisubiri huruma yao ilihali hakuna mwenye huruma na sisi raia c'mon let raise our voices together tumechoshwa na siasa za mipasho.
 
ukawa ni sawa na boko haram tu...ukawa ni ugaidi


nape ni mwiba mchungu kwa ukawa.mtajibeba

huyu mwanamke si ndio yule ambaye hana mume aliyegombea umakam mwenyekiti wa bunge la katiba akaambulia pa tupu??

kwani kuna tofauti gani kati ya ukawa na boko haram.......ukiacha hii ya kwamba boko haram ni ya nigeria na ukawa ni ya tz

BrigGen+NnauyeKisw.jpg
 
Back
Top Bottom