Nape akutwa na majanga Iringa

Nape akutwa na majanga Iringa

Earthmover

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2012
Posts
25,975
Reaction score
25,289
....

katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) Taifa Nape Nnauye apatwa na majanga mkoani Iringa baada ya kuanguka na kuteguka mkono wake wa kulia wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya timu ya msafara wa Kinana na Veteran mjini Iringa.

Tukio hilo limetokea mapema asubuhi ya leo na hivyo kulazimika kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi.


3.%2BNape%2BIringa%2Bmjini.jpg

4.jpg

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa
Mwembetogwa mjini hapa Nape ambae alikuwa amefungwa mkono wake alisema amepatwa na tatizo hilo leo asubuhi baada ya kuanguka uwanjani japo mbali ya kuanguka alisema hajaweza kuacha kupanda jukwaani kuwaeleza wananchi wa Iringa mjini juu ya mbunge wao mchungaji Peter Msigwa( Chadema)

Kwani alisema ni lazima mbunge Msigwa aondoke katika jimbo hilo baada ya kushindwa kuwatumikia vema wananchi wa jimbo hilo na kuendelea kuwaletea mabalaa mbali mbali .

Nape pia ametumia nafasi hiyo kutaja ahadi lukuki za mbunge Msigwa ambazo alipata kuwaahidi wananchi pasipo kuzitekeleza katika jimbo hilo.


note: Ukipambana na Chadema unapambana na Mungu !!!
 
Kinana hajamzungumzia Msigwa,hasimu wake wa masuala ya UJANGILI???NA ILE MELI???

Msigwa Ukimtajia Jina la Nyalandu anaishia kukenua kenua! anatoa 3M kulipia Press Conference ya kumsifia Nyalandu wakati chama chake Mkoani hakina walau Printer ya laki 3!
 
Huyu bwana sidhani kama anafikiria sawasawa, hawajui umuhimu wa competitive politics?
 
Katibu Mwenezi gani wa chama tawala asiyeweza kufanya ziara mikoani peke yake mpaka apate mbeleko ya Kinana? Hicho cheo hakiwezi, na siku JK akitoka Ikulu nayeye akatafute kibarua kingine.
 
Kwani kodi anakusanya Mchungaji Msigwa? au mmbunge anafanya nini zaidi ya kueleza shida za wananchi wake bungeni?

Nape anafikiria kwa kutumi ma-ka-lio ndiyo maana anasema wananchi hawana haja ya katiba kwani katiba haiwezi kuwajengea barabara wala kuwaletea wananchi maji. Huyu ni msomi wa Masters pale mzumbe....Sijui kwanini ameamua kukiabisha chuo alichosoma hivyo? kana kwamba hakufundishwa kitu chuoni.
 
...

....ukipambana na Chadema unapambana na Mungu !!!

Mungu gani huyo kwenye Masanduku ya kura kila Uchaguzi kura hazitoshi, Mungu gani anaedai kuibiwa kura baada ya kushindwa " kuzilinda" aliepa kuandamana mpaka Bunge liahirishwe lakini akashindwa, Acheni kufananisha washerati wa akina Mukya na jina la Muumba wako na wangu
 
kuna taarifa zisizothibitishwa kuwa hayo yamemkuta kwenye fumanizi na mke wa mtu.ritz na wenzio tupeni taaruifa sahihi.
 
Mungu gani huyo kwenye Masanduku ya kura kila Uchaguzi kura hazitoshi, Mungu gani anaedai kuibiwa kura baada ya kushindwa " kuzilinda" aliepa kuandamana mpaka Bunge liahirishwe lakini akashindwa, Acheni kufananisha washerati wa akina Mukya na jina la Muumba wako na wangu

...Siku zote Mungu husimamia ukweli !!!


mara.jpg
 
Wanachama wake wanaamini na kumtegemea Mungu hivyo Mungu hapo Chadema lazima awepo tu .
hata CCM wapo pia. Nadhani tusifanye siasa na Mungu. Huko ni kumkosea adabu kwa nafasi yake. CHADEMA na vyama vingine yawezekana kuna wachamungu wala sina tatizo na hili. Ila kukifanya chama cha siasa ni representative wa Mungu au Mungu.mwenyewe ni utovu wa nidhamu na ni dhambi!
 
hata CCM wapo pia. Nadhani tusifanye siasa na Mungu. Huko ni kumkosea adabu kwa nafasi yake. CHADEMA na vyama vingine yawezekana kuna wachamungu wala sina tatizo na hili. Ila kukifanya chama cha siasa ni representative wa Mungu au Mungu.mwenyewe ni utovu wa nidhamu na ni dhambi!

...ccm mlengo wa shetani
 
Back
Top Bottom