Akiwa anahojiwa asubuhi na sauti ya Ujerumani Nape alizungumzia mambo mengi kuhusu utendaji wa serikali ya ccm. Kazungumzia kuhusu Bomu lililolipuka kanisani Olasiti na lile la kwenye mkutano wa CHADEMA Soweto pamoja na watu kupigwa risasi kwa kutumia boda boda.
Na akasema vyombo vya usalama havijachukua hatua stahili kwa ajili ya matukio hayo. Pia akasema Tume iliyoundwa ikiongozwa na Paul Chagonja haijawahi kuleta taarifa yoyote ya maana isipokuwa ni kama kupoteza muda na fedha za umma.
Kuhusu mawaziri mizigo Nape amesema wao kama chama wamewahoji mawaziri hao na sasa wanachosubiri ni utekelezaji kwa upande wa serikali.
CCM kichekesho kweli, kama nina kumbukumbu sahihi huyo Chagonja ni kama juzi tu hapa amepandishwa cheo, sasa mtu ameshindwa kufanya kazi aliyopewa ya uchunguzi alafu serikali ya CCM inampandisha cheo, vituko Tanzania
ukifuatilia matendo ya watu wa ccm na serikali yao ni kama vile wameshakubali kushindwa kazi na wanakiri ila kilichokosekana ni wa kuwaambia 'ondokeni' kwa kutumia mfumo wa kisiasa uliopo.
Kiukweli sijapendezwa na mauaji ya Kisesa, Mwanza lakini ni wazi kuwa huenda ikawa njia mpya au 'plan B' ya wanaoamini kuwa wamiliki wa nchi hii.