Nape afunguka na kusema serikali yake ni dhaifu

Sengeon

JF-Expert Member
Dec 29, 2011
529
0
Akiwa anahojiwa asubuhi na sauti ya Ujerumani Nape alizungumzia mambo mengi kuhusu utendaji wa serikali ya ccm. Kazungumzia kuhusu Bomu lililolipuka kanisani Olasiti na lile la kwenye mkutano wa CHADEMA Soweto pamoja na watu kupigwa risasi kwa kutumia boda boda.

Na akasema vyombo vya usalama havijachukua hatua stahili kwa ajili ya matukio hayo. Pia akasema Tume iliyoundwa ikiongozwa na Paul Chagonja haijawahi kuleta taarifa yoyote ya maana isipokuwa ni kama kupoteza muda na fedha za umma.

Kuhusu mawaziri mizigo Nape amesema wao kama chama wamewahoji mawaziri hao na sasa wanachosubiri ni utekelezaji kwa upande wa serikali.

Source- Sauti ya Ujeruman.
 

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,109
2,000
Naombeni tu-print au turekodi tuweke kumbukumbu vizuri maana hakawii kukataa na kuruka kimanga
 

jnuswe

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,270
1,195
CCM kichekesho kweli, kama nina kumbukumbu sahihi huyo Chagonja ni kama juzi tu hapa amepandishwa cheo, sasa mtu ameshindwa kufanya kazi aliyopewa ya uchunguzi alafu serikali ya CCM inampandisha cheo, vituko Tanzania
 

harakat

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
2,894
2,000
Nape anaweza kuwa muelewa ila mm napenda afikirie kwa mapana vizazi vijavyo vitaishi vipi kwaenye tz hii ambayo wanaitengeneza
 

omujubi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
4,162
2,000
ukifuatilia matendo ya watu wa ccm na serikali yao ni kama vile wameshakubali kushindwa kazi na wanakiri ila kilichokosekana ni wa kuwaambia 'ondokeni' kwa kutumia mfumo wa kisiasa uliopo.
Kiukweli sijapendezwa na mauaji ya Kisesa, Mwanza lakini ni wazi kuwa huenda ikawa njia mpya au 'plan B' ya wanaoamini kuwa wamiliki wa nchi hii.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom