Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
ILE kauli kwamba ‘muosha huoshwa’ imedhihiri bungeni baada ya wabunge kumkalia kooni Nape Nauye, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, anaandika Faki Sosi
Jana wabunge hao wamesema kwamba, Nape ambaye kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana, alikuwa akinadi baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Tano kuwa mizigo na kwamba, kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya bunge kutazuia wananchi kumpima kama yeye ni mzigo ama rumbesa.
Miongoni mwa waliomng’ang’ania Nape ni Mwita Waitara, Mbunge wa Ukonga, Dar es Salaam (Chadema) ambapo wakati akichangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2016/17 amesema, matangazo hayo yangeonesha wazi kwamba Nape ni mzigo ama rumbesa.
Amesema, Serekali ya Rais John Magufuli inawasukuma wananchi kuomba stakabadi lakini haitaki wajue namna gani fedha wanazolipia kodi zinavyotumika.
“Nilipoona amepewa Wizara ya Habari nikajua ataruhusu mojadala ya wazi ili tumuone yeye kwamba hatokuwa mzigo lakini yeye amekuwa rumbesa,” amesema Waitara.
Kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana, Nape akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa na Abdurahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM walitembea nchi nzima wakinadi baadhi ya mawaziri wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete jambo ambalo lilisababisha Nape kuitwa Vuvuzela.
Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini amelieleza bunge kwamba, wabunge wote wanaounga mkono bunge kutooneshwa moja kwa moja na hata kusababisha mtafaruku bungeni wanahojiwa na Kamati ya Maadili ya Bunge.
Nape amesema kuwa, wabunge kwa pamoja walisomama na kupinga hatua ya serikali kuzuia matangazo hayo lakini cha kushangaza wengine wamegeuka.