Napauka mno kipindi hiki, nitumie nini?

Napauka mno kipindi hiki, nitumie nini?

Inkotanyi 94

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2013
Posts
2,244
Reaction score
4,030
Amani iwe pamoja nasi sote!
Tukiachilia matatizo yanayoendelea; cambodia, pakistan, gaza, yemen, drc, ukraine, sahel, gen z, brics, iran, Lisu, Pole Pole, gwajima, mchujo CCM na bilion ya Taifa stars.... hebu tuangazie pia la ngozi yangu.
Wajuvi wa ngozi za kiume.
Nipo dar.
Kipindi hiki napauka kila idara ya mwili.
Nakunywa maji sana lakini wapi.
Huwa natumia lotion ya Cocoa butter for men lakin ndo kabsa napauka zaid.
Na hivi wanaume hatujirembi sana nimetelekeza makalio yakapauka kama pembe ya faru Joni.
Nipake nini?
Au ndo nafukuzwa dunian kistaarab!
 
mwanaume unataka uwe softy. Ndio maana wengi wanavunjwa.
20250506_162748.jpg
 
Tafuta Bio oil, mkuu hiki kipindi ni body oil na futa la mgando tu ndo utatoboa.
 
Na nyie wanaume humu mmezidi bana....yani kila mwanaume mwenzenu akiuliza kitu kuhusu mafuta au ngozi yake ni kum attack na maneno ya mwanaume hivi mwanaume vile..so watu watembee kama mizimu? Yani wapauke kama wako mashineni wanasaga unga..
Kuhusu yule mwingine mnasemsema kila siku ni special case ila wengine wanataka kujua kwa sbb ya hali ya hewa...kuna muda mnajidefend sana kwny uanaume wenu kumbe ndo wala viboga wenyewe...msyuuuu😏😏
 
Hii changamoto ndo nakutana nayo mimi kipindi hiki. Mafuta natumia ni oil ya nazi lakini ngozi inapauka sio poa wakati mwingine mwili unakuwa na shoti ya umeme yaani unagusana na mtu mkono una hisi anashtuka au ukishika kitasa cha mlango wewe mwenyewe unahisi electric short kabisa.
 
Back
Top Bottom