Napata shida na Nia ya Serikali ya Viwanda

FredKavishe

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,090
318
Wakati wa kampeni Raisi Magufuli alijinasibu na kauli ya Serikali yake itakua ya viwanda mpaka sasa mwaka na miezi kadhaa toka awe raisi bado anaendelea na kauli yake inawezekana wanayo nia nzuri lakini itashindwa kutekelezwa.

Kuna operation inaendelea ya kukamata Viroba kwa hoja vinachafua mazingira ukiangalia kwa idadi kampuni za bia ndio zinaongoza kulipa kodi,inawezekana kabisa Viroba zinasababisha madhara ya afya haswa nguvu kazi,madhara ya mazingira pia nk.

Hata Viwanda vikubwa pia vinasababisha madhara haswa hewa chafu angani hata maji machafu yanayomwaga kwa jamii,kwa kua tunaona kila viwanda kina madhara yake kwa jamii tena vingine madhara makubwa zaidi.

Zoezi hili la viroba limesababisha umasikini kwa baadhi ya wafanyabiashara ukizingatia wengi walikua na mzigo na tamko limewapa siku 10 tu kumaliza stock tu ya mzigo wote unauzaje viroba hata tani 400 zilikamatwa kwa wiki moja,je wafanyabiashara watarudishiwa pesa zao za kununulia mzigo ambao sasa unakamatwa.

Viwanda vina mitambo ambayo inafungasha hivi vifungashio vinavyochafua mazingira kubadilisha hivyo vifungashio huwa inachukua muda,tuseme leo Konyagi waweke oda ya mashine ambayo vifungashio vitakua rafiki kwa mazingira,mpaka mashine ifike ni miezi hadi 4-5 bado ifungwe tuchukulie mwezi 1 haraka ilikua ya nini?

Ajira imekua ngumu je serikali imejuuliza madhara ya ajira kwa watu kwenye haya makampuni kwa kusitisha uzalishaji wa viroba kwa maana kwa kusitisha hivi ina maana makampuni mengi watapunguza ajira kwa wafanyakazi wao.

Kwanini wasingewapa hata miezi 6 huku viwanda zikukatazwa kuzalisha viroba kwa mifuko inayo haribu mazingira,lakini hawa wafanya biashara wamalize stock zao zote,Lakini vilevile wakati huo kampuni wakinunua mitambo yenye vifungashio vya mazingira.

Ndio maana tunajiuliza nia ya dhati ya Serikali kuhusu Viwanda je ni dhamira ya dhati ama tunakurupuka viwanda havijengwi kama kichuguu lazima tuandae mazingira rafiki kwa kurupuka hii imetisha hata wawekezaji wapya yaani leo kuna Mungu mtu anaweza akaamka kiwanda cha Cement kisiwepo kinarusha hewa chafu Angani pia kuangalia effect kwa jamii husika.

Sote tunatamani Tanzania ya viwanda lakini hatuoni nia njema kuifikia mathalani kiwanda kama cha Dangote kilichukua miaka 4 mpaka kufunguliwa ina maana viwanda vikubwa vitachukua muda kujengwa mpaka kuanza uzalishaji kipindi hiki cha serikali kuwekeza kwenye uchumi wa viwanda wajenge misingi imara ya upatikanaji wa malighafi za viwanda hapa hapa nchini haitakua na maana kiwanda cha Nguo halafu pamba itoke kwingine.

Sekta ya Viwanda inategemea na sekta ya Miundominu,Nishati,Kilimo ambapo hatufanyi vizuri hakuna sera bora...

Nimalize kwa kusema ni ndoto kuikaribia Tanzania ya Viwanda kama wawekezaji wanakatishwa tamaa kwa sheria za kiongozi akiamka anaamua jambo fulani.
 
Back
Top Bottom