usikurupuke kaka vuta subira! Mara nyingi mtu anapoanza kazi huwa kwenye probation na ktk kipindi hiki kazi huwa si nyingi hivyo muda wa kutoka kazini huwa ni wa kawaida. Na kama ujuavyo new job siku zote huja na new people, new challenges and new environment. Kutokana na hilo, kuna uwezekano wakati wa kuadapt mazingira ndiyo kama hivyo lazima akusimulie kila kinachoendelea huko kwenye kazi mpya. Ni jambo la kawaida unapopata kazi upya kusimulia yale mazingira na watu wapya unaokutana nao huko kazini kwa mwenzi wako ukirudi nyumbani. Lakini ukishazoea, kila kitu unaona kawaida!
Cha msingi hapa brother ni kumpa muda na wakati huo hio kufanya uchunguzi wa kina. Unaweza kuanza kwa kujitahidi kuzoeana na watu wa ofcn kwake wale waaminifu na kupiga safari za kushtukiza hapo kazini pasipo yeye kujuwa na kusoma reaction yake thereafter. Kama kuna mambo anayoyafanya huko kazini kwake hatapenda kukuona maana moyo utakuwa unamsuta. Na pia kumbuka kuwa mara nyingi watu huwa hawapendi kumuona mwenzao anaibiwa wakakaa kimya, watakwambia tu hata kwa mafumbo.
Kama utapenda kufanya uchunguzi ni-PM nikupe ma-njia ya kufanya.
Pole sana mkuu