Mtoto wa Mkulima
JF-Expert Member
- Apr 12, 2007
- 681
- 126
Ni bora ukajikata kisabuni mapema kuliko kuendelea kuumiza roho yako. Huyu demu inaelekea anataka kote kote wewe kwa kuwa uko hapo utamtimizia shida zake kwa kuwa huyo mganda yuko ughaibuni, lakini moyoni mwake keshakutoa na kumuweka huyo mganda. Inawezekana kabisa anaendelea kupata nyeti zako kwa sababu mapigo yako si ya kawaida ukilinganisha na huyo mganda
Kama wewe ni 'muungwana' basi achana naye kabisa, lakini kama ni 'mtoto wa mjini' unaweza kuendelea 'kula uroda' huku ukijua kwamba mali zina mwenyewe.
Kwa usalama wako ni bora ukaachana naye maana hujui huyo mganda ni mtu wa aina gani, lolote linaweza kutokea na kukuacha wewe kwenye majuto makubwa.
Hiyo noma ndugu yangu, uko na demu mnapiga story inakuja simu inabidi akimbie nje ili akaongee kwa kuhofia wewe utasikia mazungumzo yao. Achana naye, maana kishaonyesha chaguo lake kati yenu ni lipi, kuendelea kuwa naye ni kuumiza roho yako.
Mtoto wa Mkulima, ni jambo la maana sana umefanya hilo, demu wa namna hiyo hata ukiposa kisha kuoa, baada ya miaka kadhaa tabia yake hiyo itarudi tu tena. Ni bora umefanya hilo mapema kabisaa kabla ya commitment ya muda mrefu.
Kuhusu huyo jamaa yake, miye nakusihi usimfatilie maisha yake... kama yeye ni illigal immigrant hayo ni maisha yake acha kudadisi maisha ya mwanamme mwingine, hayo mambo waachie akina dada (si watukani), pia kama kuna jazba bado unalo naomba uliondoe kabisa maana tatizo ilikuwa demu na inawezekana hata kama huyo Mganda anamchukua hivi sasa, baada ya muda bado tu huyo demu atatafuta Mbogo mwingine (maana kesha onjeshwa asali tayari) wa kuweka pembeni ili kukidhi ka-urafi kake. Hivyo basi usije uka mtungua jamaa kule home office kwa ajili ya kulipiza kisasi tu katika maswala ya mapenzi, ukithubutu kufanya hilo, naamini lita kuwinda maishani. Ni hayo tu. Pole na mkasa huo na ni matumaini yangu chaguo lako lifuatalo litakuwa makini na linalofaa zaidi na la kudumu nalo maishani. Baadae.
SteveD.
Ee bwana wazee naombani ushauri.
Miaka miwili hivi nilikutana na demu mmoja kutoka Kenya ukambani. Demu kiaina tukawa kweny uhusiano. Tumeendelea kuwa na uhusiano toka mwaka jana hadi juzi kama week 3 hivi. Demu tunaishi nae karibu sana ni mwendo wa kama dk 5 kutoka kwangu hadi kwa kwa hiyo tunaonana kila siku na demu alikuwa anapika ndio tunakula wote.
katikati ya mwaka huu demu alidai anataka kupata mtoto maana umri umeenda kidogo kama 30 years hivi ambapo tunaumri sawa ila nimemtangulia kwa mwezi mmoja tuu.
Juzi mwezi wa kumi demu akaanza kubadilika akawa anachart sana na mara nyingi nikimkuta anachart anakuwa kama anahide compter. Nikahisi kuna kitu. Siku moja demu akaniambia anaomba break kidogo kwa sababu kuna mambo ya kifamilia anatakiwa kuwasaidia wadogo zake shule etc etc so tusitishe uhusiano ili apate muda wa kufanya mambo yake.
Siku moja niko chumbani kwake yeye akatoka kwenda bafuni nikaingia kwenye komputer yake nikakuta kuna picha ya kijana nikagundua kuwa amepata BF. Sasa nikawa namwambia kuwa kama amepata jamaa yeye akawa ananiambia nisichunguze mambo yake. Nikiwa nae jamaa akapiga simu nikasikia maongezi yake nikagundua sasa yuko kwa mapenzi na jamaa ambaye ni Mganda Bwana M.F ambaye naye yuko huku ugaibuni anafundisha kiingeraza.
Sasa demu nikamuuliza akasema kweli kwa sababu jamaa anataka kumuoa. Ila demu still akaendelea kulala na mimi. Kweli nilimpenda sana huyu demu juzi ananiuliza kama nampenda na yeye anasema anajifeel guilty lakini sasa anahitaji kuolewa na anajua kuwa ameniumiza so sitomtrust tena.
Wakuu hali kama hiyo inakuwa je? ujue kwamba tunakaa kwenye flat moja na just one floor. Huwa nikimuona roho inaniuma sana wakuu.
Sasa najiuliza maswali mengi sana maana huyu demu tulipo fahamiana naye kwa week moja tuu tukalala wote na huyu jamaa nae wamefahamiana muda mfupi wamelala wote. Demu ni msomi na ana masters mbili ila sasa sijui wazee inakuwa je hapo. Nipeni ushauri.
Wakuu nashukuruni saana kwa ushauri wazee kweli first week ilikuwa ngumu sana kwangu. Nilikuwa stressed sana ila sasa nimeshaanza kuzoea na simwazi tena. Maisha huwa ni safari ya kujifunza siku zote.