Naombeni Ushauri. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naombeni Ushauri.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtoto wa Mkulima, Dec 14, 2007.

 1. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Ee bwana wazee naombani ushauri.
  Miaka miwili hivi nilikutana na demu mmoja kutoka Kenya ukambani. Demu kiaina tukawa kweny uhusiano. Tumeendelea kuwa na uhusiano toka mwaka jana hadi juzi kama week 3 hivi. Demu tunaishi nae karibu sana ni mwendo wa kama dk 5 kutoka kwangu hadi kwa kwa hiyo tunaonana kila siku na demu alikuwa anapika ndio tunakula wote.

  katikati ya mwaka huu demu alidai anataka kupata mtoto maana umri umeenda kidogo kama 30 years hivi ambapo tunaumri sawa ila nimemtangulia kwa mwezi mmoja tuu.

  Juzi mwezi wa kumi demu akaanza kubadilika akawa anachart sana na mara nyingi nikimkuta anachart anakuwa kama anahide compter. Nikahisi kuna kitu. Siku moja demu akaniambia anaomba break kidogo kwa sababu kuna mambo ya kifamilia anatakiwa kuwasaidia wadogo zake shule etc etc so tusitishe uhusiano ili apate muda wa kufanya mambo yake.

  Siku moja niko chumbani kwake yeye akatoka kwenda bafuni nikaingia kwenye komputer yake nikakuta kuna picha ya kijana nikagundua kuwa amepata BF. Sasa nikawa namwambia kuwa kama amepata jamaa yeye akawa ananiambia nisichunguze mambo yake. Nikiwa nae jamaa akapiga simu nikasikia maongezi yake nikagundua sasa yuko kwa mapenzi na jamaa ambaye ni Mganda Bwana M.F ambaye naye yuko huku ugaibuni anafundisha kiingeraza.

  Sasa demu nikamuuliza akasema kweli kwa sababu jamaa anataka kumuoa. Ila demu still akaendelea kulala na mimi. Kweli nilimpenda sana huyu demu juzi ananiuliza kama nampenda na yeye anasema anajifeel guilty lakini sasa anahitaji kuolewa na anajua kuwa ameniumiza so sitomtrust tena.

  Wakuu hali kama hiyo inakuwa je? ujue kwamba tunakaa kwenye flat moja na just one floor. Huwa nikimuona roho inaniuma sana wakuu.

  Sasa najiuliza maswali mengi sana maana huyu demu tulipo fahamiana naye kwa week moja tuu tukalala wote na huyu jamaa nae wamefahamiana muda mfupi wamelala wote. Demu ni msomi na ana masters mbili ila sasa sijui wazee inakuwa je hapo. Nipeni ushauri.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,814
  Likes Received: 83,210
  Trophy Points: 280
  Ni bora ukajikata kisabuni mapema kuliko kuendelea kuumiza roho yako. Huyu demu inaelekea anataka kote kote, lakini moyoni mwake keshakutoa na kumuweka huyo mganda. Inawezekana kabisa anaendelea kupata nyeti zako kwa sababu mapigo yako si ya kawaida ukilinganisha na huyo mganda

  Kama wewe ni 'muungwana' basi achana naye kabisa, lakini kama ni 'mtoto wa mjini' unaweza kuendelea 'kula uroda' huku ukijua kwamba mali zina mwenyewe.

  Kwa usalama wako ni bora ukaachana naye maana hujui huyo mganda ni mtu wa aina gani, lolote linaweza kutokea na kukuacha wewe kwenye majuto makubwa.
   
 3. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0

  Babu nashukuru sana kwa ushauri mzee I real apreciate. Tuko wote Ugaibuni huku na huyu mganda naye anaishi kwenye hili jiji. Nina jamaa yangu mganda anamjua na anasema jamaa yupo na anaishi hapa hapa. Kama jana demu alikuja kwangu kunitembelea sas jamaa akapiga simu demu akakimbia kusikiliza nnje. Tatizo nipe strategy za namna ya kumwacha sasa. Hii ni kweli wazee sio story za kwenye magazeti.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,814
  Likes Received: 83,210
  Trophy Points: 280
  Hiyo noma ndugu yangu, uko na demu mnapiga story inakuja simu inabidi akimbie nje ili akaongee kwa kuhofia wewe utasikia mazungumzo yao. Achana naye, maana kishaonyesha chaguo lake kati yenu ni lipi, kuendelea kuwa naye ni kuumiza roho yako.
   
 5. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mzee nimeshaamua kuachana naye kabisa
   
 6. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mtoto wa Mkulima, ni jambo la maana sana umefanya hilo, demu wa namna hiyo hata ukiposa kisha kuoa, baada ya miaka kadhaa tabia yake hiyo itarudi tu tena. Ni bora umefanya hilo mapema kabisaa kabla ya commitment ya muda mrefu.

  Kuhusu huyo jamaa yake, miye nakusihi usimfatilie maisha yake... kama yeye ni illigal immigrant hayo ni maisha yake acha kudadisi maisha ya mwanamme mwingine, hayo mambo waachie akina dada (si watukani), pia kama kuna jazba bado unalo naomba uliondoe kabisa maana tatizo ilikuwa demu na inawezekana hata kama huyo Mganda anamchukua hivi sasa, baada ya muda bado tu huyo demu atatafuta Mbogo mwingine (maana kesha onjeshwa asali tayari) wa kuweka pembeni ili kukidhi ka-urafi kake. Hivyo basi usije uka mtungua jamaa kule home office kwa ajili ya kulipiza kisasi tu katika maswala ya mapenzi, ukithubutu kufanya hilo, naamini lita kuwinda maishani. Ni hayo tu. Pole na mkasa huo na ni matumaini yangu chaguo lako lifuatalo litakuwa makini na linalofaa zaidi na la kudumu nalo maishani. Baadae.

  SteveD.
   
 7. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Steve nashuru kwa ushauri huo. Kusema kweli sina jaziba wala nini hayo maisha ya mademu tumecheza nayo sana na wala sina nia ya kumuatilia mshikaji wake. Maana mimi nilipo mkuta huyo demu alikuwa na jamaa yake huko Kenya kwa hiyo naona nikuwa ni trend tuu hiyo mkuu. I wish kuwa wawe na maisha mema I know kwamba sikuwa nimeweka malengo ya muda mrefu na nadhani ni Mungu alinisaidia kwa hilo.
   
 8. C

  Choveki JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2007
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mtoto wa Mkulima, Pole sana, ndiyo kukua na kukomaa huko.
  Kwa kiasi fulani naweza kusema una bahati kwani huyo demu amekuonyesha jinsi alivyo kabla hujafunga naye ndoa, hamjawa na mtoto au huja invenst roho yako kwake. Jihesbau una bahati, anza polepole kupunguza mawasilano naye, pia anza kutofuta mwenzio mwingine. Jifunze kutoka na hayo yaliyotokea, wewe bado kijana na move on.
   
 9. Ole

  Ole JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2007
  Joined: Dec 16, 2006
  Messages: 751
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  You're a very lucky man. The lady has shown you her true colours, she wasn't meant for you. Its time to look for someone else who will be committed to you and your life rather than wasting time any more with her. It will be difficult initially but rest and be assured it will be the best decision you have ever taken in your life.
   
 10. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #10
  Dec 15, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wakuu nashukuruni saana kwa ushauri wazee kweli first week ilikuwa ngumu sana kwangu. Nilikuwa stressed sana ila sasa nimeshaanza kuzoea na simwazi tena. Maisha huwa ni safari ya kujifunza siku zote.
   
 11. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #11
  Dec 15, 2007
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kabla ya yote kapime ngoma after 21days tangu mkutane mara ya Mwisho. Usiniambie huku umatumbini hakuna ngoma.

  Nakupa pole sana na kama ndio mara ya kwanza kukutana na hili jambo najua utakuwa umepata pigo kubwa but ni sehemu ya maisha.
   
 12. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2007
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  achana Naye Haraka Sana. Tafuta Mwingine!!
   
 13. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #13
  Dec 15, 2007
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..acha kumfuata,jiondoe taratibu kwenye hiyo ngome.

  ..go out,have fun,look for someone else!be careful though,usijeibukia ngoma nyingine kama hiyo!kumbuka easy come,easy go!

  ..ndio maisha hayo!leo machungu kesho matamu!
   
 14. M

  Mtu JF-Expert Member

  #14
  Feb 4, 2008
  Joined: Feb 10, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Usikubali kuacha demu kirahisi mkuu shikiria ngangangaa!! komaa ne huyo Mtoto wa M7
   
 15. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kaka kwanza naomba nikupe pole sana kwa hayo yaliyokusibu.

  Huyu demu kwa jinsi ninavyofikiri ni kwamba hakuwa muwazi kwako, na pia kwa ambavyo nawaelewa wanawake ni wasiri sana na ikifikia ukapata kujua ishu kama hiyo ujue mambo yaliharibika tangu zamani.
  Cha msingi hapa kaka ni kuamua kuachana na huyo binti tena bila ugomvi wowote mwambie awe free kufanya hayo mambo yake na wewe jitahidi usijihusishe na ishu zake hata kidogo. Pia kaka amini wewe ni kijana na bado utaweza kupata demu atakayekufaa kwa kila hali.

  Things happen tena ni bora hili umelijua mapema kabla hamjaingia katika ngazi nyingine ya mapenzi (NDOA).

  Nakuomba tu uchukulie hilo suala kama njia ya kukufanya uwe na experience katika maisha ya mapenzi.
   
 16. F

  FELISTER kulwijira Member

  #16
  Feb 5, 2008
  Joined: Mar 11, 2007
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inaumiza sana lakini naamini iko siku atakukumbuka tu nawe utakuwa umeshasahau na bila shaka utakuwa umepata mwingine itakuwa zamu yake kuumia na kujuta ,mara nyingi inatokea hivyo kwavile yeye kaanza we maliza kabisa yaani m delete kabisa katika kumbukumbu yako kila la kheri!
   
 17. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #17
  Feb 5, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Sasa wewe Mbona ulikuwa unamchezea tu bila kumwahidi utamwoa?
   
 18. mwanamama

  mwanamama Member

  #18
  Feb 8, 2008
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Eti mtoto wa mkulima ulikuwa unampenda huyu msichana kweli au wewe ulikuwa unataka tu mtu wa kukupikia na mapenzi, bila commitment yoyote.
  Simlaumu huyo msichana, yeye anataka kuolewa, na wewe wataka kucheza tu. Sasa ni kwa nini wewe utake yeye akusubiri tu mpaka mwisho wa dunia?
  Usidanganyike kutaka kumlaumu huyo dada, you have a responsibility to all of this too. In life what comes around, goes around, ulikuwa unamchezea sasa na yeye ameamka mapema before hajachelewa.
  Look at it this way, kama ingekuwa ni wewe umekutana na msichana mwingine mzuri ukampenda sana, si ungemuacha huyo msichana wa kikenya tu?
  Stop being selfish and take it as a man!!
   
 19. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #19
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mawazo yote mazuri, ila kwa maoni yangu Mwanamke hadi kafikia 30yrs bado hajaolewa si vyema, iwe alikupenda kwa dhati au la alikuwa tayari katika mipango ya kuolewa...na mtu aliye serious. mtot wa mkulima hapo hukuwa serious na issue ya kumuoa iwe kwa ndoa au vyovyote vile.

  Kuhusu utaifa hapana, hujakataliwa kwa sababu wewe ni mtanzania na ndio maana akaenda kwa mganda, la hasha,watu huoana hata kama mmoja ni wa taifa gani. Wanajamii tupo sehemu mbalimbali duniani, mahali nilipo sipo ulipo wewe, nchi niliyopo sio uliyopo wewe, AU NCHI MOJA SEHEMU TOFAUTI ,hata na lugha ninazozungumza huenda zikawa tofauti kabisa isipokuwa kiswahili ambacho ndio tumeanza kuwasiliana nacho hapa katika JF. NA NDIO MAPENZI YALIVYO.HAYACHAGUI WEWE NI NANI.

  Msamehe kwani ametii what so called "CALL OF NATURE" pia na wewe kama mwanajamii next time usiwe na tabia ya ubakaji wa DEMOCRACY kwani ikikugeuka itakuwa DEMO-CRAZY...Mpe nafasi na kama ni kweli huyo mwingine atamuoa..Mungu awabariki.
   
Loading...