Naombeni ushauri

Naombeni ushauri

Tafuteni mtu wa kumtongoza huyo demu halafu mnatengeneza fumanizi moja matata sana the rest mwachieni baba yenu
 
Wote walioshauri hapo juu wanasahau /kupitiwa kuwa kuna LAANA

Mali ni zake japo kachuma na mama yako huna haki kuzikatalia
Pia huwezi jua baba na mama yako mahusiano yana changamoto gani au mama nae anamapungufu huwezi yasema hapa au huyajui..

Ushauri wangu usithubutu kumtishia maisha mzazi wako kamwe hata kama anamapungufu
vinginevyo utavuna LAANA na km ipo kwenye ukoo wenu basi ndio hivyo inakutafuteni nyie watoto sasa JIHADHARI NYOTE KUIKWEPA KWA GHARAMA YEYOTE vinginevyo na nyie mtakuja kuyafanya vivyo hivyo.

USHAURI WANGU:
1. Tafuteni mzee mmoja mwenye busara amseme kistaarabu ,ikishindikana
2. Kama kuna ukoo wenu nendeni huko kuomba msaada/ushauri hasa mama yenu
3. Huo uchungu uwatume mjitafutie mali zenu na kumtunza mama yenu na yeye pia
4.Yawezekana ni mgomjwa kwani magomjwa ya akili ni mengi msogeleeni muongeze mapenzi, puuzieni hayo yake nyote hasa mama dheni kwa taratibu mnaweza kumtibu na kuokoa hizo mali, hata huyo bidada kaeni nae mkiwa na lenu jambo.

5. Mwisho mama aende ustawi wa jamii kwa ushauri zaidi ahakikishe hawezi kuharibu mahusiano. wivu na hasira NYOTE MNAWEZI VUNA HASARA
 
Mimi ni kijana nina umri wa miaka 23 katika familia yetu tumezaliwa watoto 5 na kwa bahati nzuri sisi wote ni wanaume na mimi ndiyo wa kwanza ndani ya familia yetu. Sisi tuna baba yetu ni mhuni, naweza kusema hivyo, maana anapenda wanawake kinoma.

Sasa baba yetu tabia yake ni hiyo ya kupenda wanawake sana, leo unaweza kusikia yupo na huyu kesho yupo na mwingine, yaani hatulii. Na tabia hiyo alianza kitambo sana, kipindi nina umri wa miaka 7 nilikuwa naona anavyomtesa mama yangu, kumpiga kama mtoto wake vile.

Sasa baba yangu pamoja na tabia zake hizo ni mtu ambaye anatafuta pesa sana na ana biashara zake, ana maduka na biashara nyingine. Na biashara zote hizo ameziweka nyumbani kwetu yaani kwa mama yangu, lakini kwa mara hii amedumbukia kwenye penzi la kadada kamoja hivi.

Mpaka sasa anataka kuamisha vitu vyake kwa mwanadada huyo, eti kwa huyo dada ndiyo kuna sehemu nzuri ya kufanyia biashara, lakini sisi tunaona anadanganya. Anataka kuamisha biashara vyake kutoka kwa mama na kuvipeleka kwa huyo mwanadada na hana mtoto naye.

Hapo ndipo kuna vurugo mpaka tunaona ni ajabu sasa, maana pamoja na tabia zake hizo hakuna siku ambayo aliwahi kuhamisha vitu kutoka kwa mama na kuvipeleka sehemu nyingine. Na kwa bahati mbaya hakuna mwanafamilia yeyote anayemshauri tena, wote wameshachoka na tabia zake na hata sisi watoto wake hatusikilizi.

Ila nataka nijue kitu kimoja,

Je, kisheria sisi kama watoto tuna haki ya kukataa au kuzuia mali hizo?
Kwa kuwa ni pesa zake alizitafuta kwa jasho lake mwache atapanye mali zake. Nyie msubirini zikiisha atakavyojuta

Yeye anadhani pesa itaendelea kuwepo hivyo hivyo. May be awe mtu wa kulamba asali pesa atazeeka nazo ila kama ni za kuvuja jasho then afanyie huo ujinga yatamkuta yaliyomkuta Baba yangu na wazee wengine
 
Ushauri wangu usithubutu kumtishia maisha mzazi wako kamwe hata kama anamapungufu
vinginevyo utavuna LAANA na km ipo kwenye ukoo wenu basi ndio hivyo inakutafuteni nyie watoto sasa JIHADHARI NYOTE KUIKWEPA KWA GHARAMA YEYOTE vinginevyo na nyie mtakuja kuyafanya vivyo hivyo.
Hii issue ya laana ni uongo
 
Moja ya hatar ya tabia hizi za uasherati ni kwamba utazunguka wakikijua ipo siku utafanyiwa ulozi utanasa kwa mwanamke wa mjini hapo utaflisiwa ...kwa hapo muombeni tu mzee wenu.

Anyway Kuna kijana wa ovyo nae kauza Figo kumnunulia mpenzi wake iphone 14
Screenshot_20221013-194811.png
 
Mwingine kaondoka juzi, kamnyanyasa mkewe mpaka basi kamterekeza hapo, na watoto wamesoma kwa shida, na mali zote katafuta na mkewe, hata nyumba aliokuwa akiishi na mkewe aliiweka bond kidogo iondoke, pesa katumbua na kamdada wamekula zilivyopungua kama si kuisha kamdada kakamkimbia, kurudi kwa mkewe kaona aibu, stress mpaka kafariki, wajane wanazidi kuongezeka.
 
Back
Top Bottom