Naombeni ushauri

Naombeni ushauri

Katika maisha yangu haya ya miongo minne kasoro niliyoishi, na muongo mmj na nusu hv katika kuwajua wanawake, kuna mambo mengi sana niliyojifunza. Lakini kubwa kuliko nililojifunza na kulielewa vyema ni kuhusu mwanamke kutokuwa na ustahamilivu/Subra/Uvumilivu pindi mume/bwana wake anapokuwa amepata changamoto ya kipesa.

Wengi wanasema kuwa katika mahusiano/ndoa , isije ikatokea hata kwa bahati mbaya mwanamke akamzidi mwanamume kipato, hasa wanawake wetu wa ngozi nyeusi (African ladies to be precisely). Mara nyingi imekuwa ikileta shida sana.

Kwa asili wanasema mwanamke mi mtu wa kuhudumiwa/kupewa (don't get me wrong), na mwanamme ni mtu wa kutoa.
Sasa inapotokea circumstances mambo yakawa vice versa, basi mambo huwa kama alivyosema mtoa mada au hata pengine zaidi.

Ukitaka uthibitishe kauli niliyotoa hapo juu, angalia mfano huu: unakuta mwanaume anakazi au biashara nzr, wkt huo mwanamke anakaa home au ana kazi ya kawaida na kipato cha kawaida tu. Mwanaume atahudumia na kuitunza familia, atajenga nyumba ya kuishi, atanunua gari, atalipia watoto ada, ataitoa familia out, n.k (yote haya yakifanyika huku mke/mwanamke akipata special treatment klk pengine hata watoto au mama mzazi wa mwanaume).

Sasa itokee siku mwanaume kafukuzwa kazi au biashara imebuma, na mwanamke anaendelea na kijikazi chake cha mshahara wa laki 7, aisee dharau zitaanzia hapo, kukasirika kusikokuwa na sababu, maneno kibao kuwa majukumu ameachiwa yeye tu, manun'guniko kuwa mwanaume hafanyi chochote, unakuta hata mzigo hakupi, na mmb mengine kama hayo. Hii siyo kwa kila mwanamke lkn wengi wao, hasa hawa wa mjini ndy wako hvy.

Sasa tukirudi kwenye mada mezani, mtoa mada unatakiwa uelewe kuwa mwanaume asipokuwa na pesa mfukoni anakosa confidence, hajiamini, anachanyikiwa, n.k!
Lakini la muhimu kujua ni kuwa mwanaume ni ngumu na inaleta sana ukakasi kumuomba mwanamke pesa mara kwa mara hata kama ni mkeo, kwa asili iko hvy. Ukiona mwaname yuko comfortable kuomba omba pesa kwa mwanamke huyo ni Marioo na ma Marioo wengi huwa wanafanywa michezo mibaya.

NINI CHA KUFANYA?
Kaa chini na mwenzako, mjadili suala hili na mengine kama yapo, zungumza nae, ikiwezekana uwe unampa mwanaume/mume wako mamlaka na pesa zako, hii itasaidia sana kumrudisha mchezoni na kuleta amani ndani. Mpe yeye ashike awe anatoa kulingana na mahitaji yenu. Ikiwezekana pangeni bajeti kbs kisha awe anatoa yeye hy pesa. Kama unaona ni ngumu, basi mpe kiasi fln akae nacho mfukoni kilinde mfuko wake, usisubiri akuombe. Najua kwa wanawake wengi hili itakuwa ni ngumu, lkn niamini nacholwambia, itasaidia sana kuokoa ndoa yenu.

Pia jaribu, kuwa na kauli nzr kwa mumeo, kaeni chini na mlijadili hili kwa unyenyekevu mkubwa, naamini mtafikia muafaka kuwa karibu na Muumba wako, mshirikishe kwa kila kitu chako, appreciate, vile vyote vzr alivyokufanyia wewe personally km mke. Mwisho pesa muhimu kwenye mahusiano/ndoa lkn haijawahi kuwa kila kitu, kuna muda wanandoa wanahitaji Amani na upendo zaidi kuliko masuala ya kipesa.

Adios!
 
umejiunga leo au mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya......mwaanaume ukiwa huna kazi kichwa huwa moto balaa na ukiwa na familia.....ila msamehe tuu.....ongea nae kwa upendo......mpe dyudyu la kukusudia then ongea nae hilo....ni msongo wa mawazo....sio tabia nzuri but usimnyanyapae....mjadiliane what next,,,,anaweza zeeka bila kazi.....ujasiriamali ni bure....anza kumuamsha mmeo....watoto wanakua hao...
 
Wakati mnakula kiapo na ukakubali kwamba utakuwa naye katika shida na raha sasa hiki ndio moja ya kipimo chako sasa.
 
Fibanochi,
Kweli aisee. Kuna wafanyakazi wenzetu wawili waliachishwa kazi, iliwachukua miezi mitatu tu tukasikia wote wameachana na wake zao na sababu kubwa ni hizi ulizozisema.
 
mamibeibe, Kitu pekee ambacho unatakiwa ukielewe ni kwamba.. Tangu asili ya kuumbwa kwa ulimwengu huu Mungu aliweka Mwanaume ni Mlinzi wa familia na wala so mlindwa, Mtoaji ndani ya familia na wala si mpokeaji Na pia muombwaji si muombaji. Kwa maana ni muwajibikaji namba moja katika kutoa mahitaji ya familia yake bila kujali ana kipato cha aina gani.

Kama unamuamin kama baba wa familia yako na hua anasimamia vyema matumizi. Na kujua wajibu wake kipindi akiwa nacho na si mtu wa ufujaji wa pesa.
Unaweza ukajiwekea utaratibu wa kumtumia kile unaona kinafaa kua kama akiba ya familia. Na kumwambia kama baba mda wote anatakiwa kua imara na utayari wa jambo lolote lile lihusulo familia yake. Pesa iyo ni ya yeye kua na utayari mda wote kusimama kama baba hivyo asikuangushe katika hilo.

Embu vuta picha mtoto kaumwa gafla bahati mbaya wewe hupatikani yeye kama baba akiambiwa alipie matibabu? Je aseme ngoja tumsubirie mama yake.
 
Finances and sex.

Hizi ndio sababu kubwa za ugomvi sugu katika ndoa
 
Badili password.ya mpesa

Password ya benk

Acha kubeba mahela home

Ila.akichacha mtoe unajua mwanaume kuomba naayo aibu(kwa wanaojielewa tu)
 
Na wewe ni tezi jike.

Leave ili iweje, aje kwenu?
Ni mwizi , umeolewa na mwizi .Halafu Mimi personal siwezi kiwa na mwanaume wa namna hiyo .Mwanaume anaechukua or omba pesa kwa mwanamke huyo ni cancer kwenye society .leave
 
Ni mwizi , umeolewa na mwizi .Halafu Mimi personal siwezi kiwa na mwanaume wa namna hiyo .Mwanaume anaechukua or omba pesa kwa mwanamke huyo ni cancer kwenye society .leave
Utoto unakusumbua,naona bado boyfriends wanakutanganya na kukuaminisha upande mmoja wa maisha
 
sasa si ushukuru kachukua elfu 5 tu..what if angekomba zote?
nahisi jamaa kakosa hata nauli,na baadhi yetu sisi wanaume tunaona noma kuomba wanawake pesa.
 
Wanaume wenzake watatetea huu upuuzi lakn mumeo ni mwizi kama sio mdokozi, badilisha namba ya siri na Kuwa makini na utunzaji pesa za cash, Kama ni Mume mwema asingefuta meseji, Kama angeomba kusingekuwa na tatzo
 
Haha wanawake hatukuumbwa kuhudumia familia jamani, angekuwa mwanaume amefanyiwa haya na mkewe wala asingeanzisha uzi ila huyu kuna kitu kinamkaba rohoni ndio maana tunashuhudia haya
 
Tatizo ni kuchukua pesa bila kukuomba, hasa ndugu kama ishu ndogo kama hii umeshindwa kukaa nae chini uongee nae kweli???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom