cheusimangala
JF-Expert Member
- Feb 27, 2010
- 2,585
- 500
MmmmmhKanitambulishe kwa huyo mama tatizo litaisha akijuwa una mtu,halafu mbona hunielezi haya mambo nyumbani ?
Mama anawasiwasi na ukaribu wenu!
Cha muhimu we mkwepe mumewe tu!
asante sana umegusa point muhimu,umeongea kama mwanamke,umeongea yenye busara.Cheusimangala najua kabisa na nakubaliana nawewe kua personally huna nia mbaya.
Naomba uiangalie kwa upande wa huyo mama... kwa maelezo ulotoa hapo juu ningekua huyo mama amaini usiami naamini ningehisi kama wewe ila ninge ku tackle kwa njia tofauti sio obvious hivyo.. Unaweza ukaona sawa but it seems huyo baba kisha kupenda kimapenzi tokana na attention yoote anayo kupa na ile hali ya kusema hi is son in to you mpaka hata mbele ya mkewe anashindwa kujizuia. Huyo ni mke wake ilipaswa aoneshe heshima kua mkiwa wote watatu mko eneo moja awe considerate na feelings za mumewe....
Cheusi mangala hebu angalia kwa umakini yafuatayo na wewe kama mwanamke mwenzangu jiweke nafasi kidogo ya huyo mkewe...
- Yeye mwanaume ndo alikutafuta mkawasiliana mpaka mkakubaliana wewe uwe member - na kisha kukutambulisha kwa mkwewe; Ni common knowledge kua mumeo akikutambulisha msichana (tena nahisi wewe ni mrembo saana) - m/ke yeyote unakua makini na kuanza ku pick up signs...
- Yeye huyo mama yupo toka mda hivyo ina maana anajua dedication ya mumewe iko vipi hapo club - huwezi jua; labda kuja kwa ndo kumemfanya kuongeza bidii zaidi....
- Anakwambia mbele ya mkewe kua ukiwa na shida yoyote sema na atakusaidia.. mwanaume hata kama si mume ni boyfriend akisema hivyo kwa m/ke mwingine na hali wewe upo ni kwamba he is not considerate of her feelings... mimi mwenyewe siwezi penda.
Ushauri wangu mimi ni kua hilo tatizo kulimaliza ni rahisi... mwambie huyo baba awe considerate to the wife na kwamba mkewe anaumia.. kueni more formal (mana sidhani kama huyo mama mjinga tu - labda kama katika hio club wewe ndo mdada pekee).. ukifanya hivyo na ukikwepa the husband eventually with time the wife will get to know you and understand.
Wish you all the best.
Mh jamani club gani hizo ni hapa bongo au huko nje?
Kanitambulishe kwa huyo mama tatizo litaisha akijuwa una mtu,halafu mbona hunielezi haya mambo nyumbani ?
cheusi,kwa style hii mwana mke yeyote lazima angehisi
ana karibia kuibiwa!
either,...
1.kua karibu sana na huyo mama,mfanye rafiki yako na mshirikishe mambo
mengi sana ili awe huru na wewe kama mtoto/mdogo wake,..
au
2.ondoka kabisa,ili kutunza ndoa ya hao watu,hii ni option ya mwisho
baada ya ya kwanza kushindikana!
Please,usi mdokolee mwenzio mme wake!
Kama umeolewa unaweza kumtambulisha mmeo kwa wote wawili
huyo boss na mke wake (au hata mchumba kama unae ni vizuri pia)!!!
sorry shantel siwezi kutaja,
naomba usinielewe vibaya,
ila ni SOCIAL CLUB,sio club za madisco au pombe,activities tunafanya hata mchungaji au sheikh anaweza kufanya,mradi awe anapenda uwezo na vigezo.
ni activities tu zakuongeza ladha ktk maisha.
asante sana umegusa point muhimu,umeongea kama mwanamke,umeongea yenye busara.
kweli hata mim angekua ni mume wangu nisingefura
mm ni mtu mzima naelewa dalili za mwanaume anayenipenda kimapenzi,lkn huyu ananijali sbb anaona umuhimu wangu kwa club yake,chukulia mfano ni club ya mpira si lazima coach atapendelea wale wachezaji anaoona wananyanyua timu.
Huyo kunambia mbele ya mkewe kuwa mtu akiniudhi nimweleze sioni kama ni tatizo sbb pia alinambia kama yeye hayupo kama kuna jambo nisisite kumshirikisha mkewe.
Hata mim siku moja nilipanga nimweleze kuwa naona mkewe hafurahii huu ukaribu lkn nikashindwa sbb namuheshimu sana na kama nilivyosema hajanitongoza.
Kuhusu kama ana tabia ya kutongoza tongoza sijui na wala siwezi kumtetea lkn mm hajanitongoza na wapo wadada wenzangu lkn sijahisi kama anawatongoza sbb yuko serious sana.
mim sina urembo wowote kama unavyofikiri kua ndo sbb ya huyo baba kupagawa,kinachomvutia kwangu ni uzoefu na mambo ninayocontribute kwa club yake.
Tena mm naona anampenda sana mkewe sema ndo hivyo tena naona haelewi.
Basi kazi unayo dear... All the best katika kufika solution..