Naombeni ushauri wenu

Diwani

JF-Expert Member
Oct 25, 2014
2,672
2,696
Bila shaka mu wazima na shughuli za maendeleo wana jamvi.

Ni takribani miaka mitatu sasa tangu nimekabidhiwa nyumba ya urithi, nyumba iliyokuwa chini ya uangalizi wa walezi wangu kwa muda mrefu.

Jengo la nyumba ni chakavu, nina lengo la kuikarabati ili niipandishe thamani ya ukaazi kwa wapangaji, mimi sikai hapo. Fursa niliyoona ni kwamba, nyumba ipo karibu na makazi ya daharia (hostels) za wanafunzi, kwa utafiti wangu, hitaji la vyumba kwa wanafunzi ni mkubwa aidha baada ya kukosa vyumba, ama baada ya muda wa kukaa kufika.

Mzunguko wangu wa kipato bado mdogo, kwa tathmini ya haraka, marekebisho yanaweza kufika kiasi cha 10 Milioni mpaka 12 Milioni; pesa ambayo sitaweza kuipata kwa shughuli nifanyayo.

Sina mpango wa kuiuza (kama lingekuwa shauri) nina mpango wa ukarabati, naomba msaada wa namna gani, naweza pata kiasi hiko nilichokadiria, na wapi (kwa maana ya taasisi ipi ya fedha). Asanteni

Karibu
 
Nenda bank ukachukue mkopo wa ukarabati.. Dhamana itakuwa hati ya nyumba na marejesho yatatokana na kodi za upangaji.. Pata mtu akuandalie andiko mradi zuri utapata pesa
 
Nenda bank ukachukue mkopo wa ukarabati.. Dhamana itakuwa hati ya nyumba na marejesho yatatokana na kodi za upangaji.. Pata mtu akuandalie andiko mradi zuri utapata pesa

Mungu akubariki kaka; ntashughulikia
 
Back
Top Bottom