Naombeni ushauri wenu, nataka kujiunga na siasa

Mc Samo

Member
Oct 26, 2016
13
9
Kwanza kabla ya yote napenda kuwasalim ndugu zangu wote wa JamiiForums wakubwa kwa wadogo,

Nasema itifaki imezingatiwa, shida yangu ni kwamba nataka kujiunga rasmi na siasa kwa maana naipenda sana toka moyoni.

Sasa basi naomba unishauri nini cha kufanya na je unapenda nijiunge na chama gani cha siasa?
 
Vuguvugu kubwa la siasa mwaka 20005-2015 haujui muelekeo wako kisiasa upo chama gani? Kama uliyoyandika yapo moyoni basi wewe kichwani ni mweupe pee labda kama ndio kwanza unatimiza miaka 18
 
Kwanza kabla ya yote napenda kuwasalim ndugu zangu wote wa JamiiForums wakubwa kwa wadogo,

Nasema itifaki imezingatiwa, shida yangu ni kwamba nataka kujiunga rasmi na siasa kwa maana naipenda sana toka moyoni.

Sasa basi naomba unishauri nini cha kufanya na je unapenda nijiunge na chama gani cha siasa?
Ni kitu cha kiasili hutokea automatically hasa ukiwa na viasili ama viashiria vya tabia hizi
Kigeugeu
Unafiki
Uongo
Rohombaya
Ubinafsi/umimi
Kusema usichomaanisha na kumaanisha usichokisema nk
Kama una viashiria hivi fuata moyo wako utafanikiwa
 
mie nikupe maneno yaliyosemwa na mh samweli sitta alomwambia mwakyembe ''jijegee ngozi ngumu, ili ukipanda juu usiungue na joto na siku ukishuka chini usidhurike na baridi''.

ni hayo tu na nakutakia kila la kheri.
 
Mi ushauri wangu,achana na siasa mkuu,inaumiza kichwa tu,ili kujua hilo nenda kapekue makablasha ya mbowe kuhusu lowasa enzi hizo,na leo wapo wapi.au kumbuka lowasa alisemaje wakat yupo ccm(asiyenitaka ccm atahama yeye ila mi sihami). Kifupi siasa ni uongouongo tu,
 
Nitakua wa mwisho kuondoka chadema-zitto kabwe
 
Ukiwa mwanasiasa na Mihemko yako uichunge! La sivyo.....Unapoteza Dira kabisa ya maisha yako.
 
Kwanza kabla ya yote napenda kuwasalim ndugu zangu wote wa JamiiForums wakubwa kwa wadogo,

Nasema itifaki imezingatiwa, shida yangu ni kwamba nataka kujiunga rasmi na siasa kwa maana naipenda sana toka moyoni.

Sasa basi naomba unishauri nini cha kufanya na je unapenda nijiunge na chama gani cha siasa?
Fuata moyo wako halafu kuwa na maamuzi binafsi... Ishi maisha yako

Jr
 
Back
Top Bottom