Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,702
- 36,143
Habari!
Mwezi wa pili alikuja mtoto wa dada yangu kutoka mkoa wa X kuja Dar kutembea.
Inavyoonyesha alikuwa na lengo la kuja kukaa kwa ndugu yetu (mama mdogo) ila maza mdogo alichomoa mkeka kwa kumwambia kuwa amesafiri na atamtafuta pindi atakaporudi.
Hajapokea tena simu mpaka leo.
Kwa scenario hiya binti akaja home kunitembelea akitokea kwa dada yake ambaye asingeweza kukaa naye kwa muda mrefu kwasabu ya kimazingira (dada yake kaolewa na wamepanga chumba kimoja).
Alikaa kwangu kama wiki hivi, kwakuwa wife alikuwa ana mwezi mmoja au miwili hivi ajifungue ikabidi nimuulize kuwa atabaki amsaidie shangazi yake kipindi cha kujifungua na baada ya kujifungua au nitafute mtu mwingine yeye anapita tu?
Akasema atakaa home asaidie kazi. Nikamwahidi kuwa wife akitengamaa nitampa mtaji asirudi mkoa kukaa tu au nitamtafutia kazi viwandani maana kwa elimu yake hakuna ofisi ya kumwajiri(std 7). OK maisha yakaendelea.
Issue iko hivi ; Binti kamaliza mwezi tu tayari kapigwa mimba na kijana wa jirani yangu. Kijana ni jobless anakula na kulala home.
Maza wake binti ambaye ni dada yangu nilipomweleza hakulipa uzito hili jambo.
Nilidhani ataungana na mimi tumpeleke binti nyumbani kwa kijana akaishi huko kama mwanzo wa ndoa lakini alitaka binti abaki kwangu mpaka ajifungue.
Hii May mimba ya binti ina miezi 2 .
Nawaza nichukue maamuzi magumu kumpeleka kwa kijana kama ndoa ya kimila au nimpe nauli arudi kwa wazazi wake.
Kijana na wazazi wake wamekubali kuwa mzigo ni wao .
Vipi wakuu nifanyeje hapo?
Asanteni