Naombeni ushauri,nimfanyeje huyu binti

Naombeni ushauri,nimfanyeje huyu binti

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,151
Reaction score
20,068
Ilikua jumatatu, tarehe 10 mwezi wa 6 mwaka 2013,niko kwenye msiba wa kaka angu(RIP BRO).. Ilikua kama sa 2 hivi usiku niko kwenye kikao tukijadili na kupanga taratibu za mazishi,kuhifadhi mpendwa wetu.

Nikiwa kikaoni nikasikia mtetemo kwenye sim yangu ikiashiria ujumbe mfupi umeingia,sikua na haraka ya kuusoma,nikijua baada ya kikao ntausoma,ndio ntakua na muda mzuri wa kusoma ujumbe huo,hata hivyo mimi ndie nilikua katibu wa kikao,nikakipa kikao uzito zaidi.

Ilipofika sa 4 kama na nusu hivi kikao kimeisha, nikasikia mlio wa sim,ilikua ni sim yangu ikiita,nikaitoa mfukoni kuipokea,kusoma jina ni la kipenzi cha moyo wangu,nikatabasam kwa mbali nikijua mpenzi wangu kanipigia kujua naendeleaje,ile napokea tu sim ikakata.

Nikajua mamaa kaishiwa pesa,nikaenda hewani,simu ikaita kidogo kisha nikasikia"simu ya mteja uliepiga inatumika" ikiashiria sim imekatwa,nikakata sim,mara kidogo nikapokea ujumbe kutoka mpenzi wangu

"nilitaka kujua kama meseji umeipata,sitaki mapenzi na wewe,futa namba yangu" nikashtuka kidogo,nikajua ni utani,kisha nikataka kujua ni ujumbe gani huo

Nikaenda inbox nikakuta ujumbe uliokua umetumwa haujasomwa ni wake akinijulisha mimi na yeye basi. Nikampigia sim hapokei,nikatuma ujumbe hakujibu. Msiba wa ndugu yangu ukawa mchungu zaidi

Siku zikaenda hivyo nikiwa siamini kilichotokea,bila ugomvi,bila sababu ya msingi nikawa nimeachwa. Nikatumia kila mbinu kumbembeleza na kumshawishi,kupitia kwa ndugu zake,marafiki zangu na ndugu zangu akagoma.

Ratiba zetu ilikua mwezi wa kumi mwaka jana nikajitambulishe rasmi,mwezi wa pili mwaka huu tufunge ndoa . Mipango hiyo ikawa imekufa. Niliyumba sana baada ya hilo tukio,nimejikaza nikasimama kiume ila kwa maumivu makali sana.

Kituko cha mwaka ni kua binti huyo kamwambia rafiki yangu kua bado ananipenda na anatamani turudiane, hadi naandika ujumbe huu huyo binti toka juzi anapiga sim(sijapokea simu yake hata moja) na kutuma ujumbe akiniomba nimsamehe

Wadau,nimrudie kisha nimtende kama alivyonifanya au nimuache aendelee na maisha yake(sina hisia nae tena na wala simpendi,,namchukia sana,natamani kisasi juu yake),ebu nishaurini wandugu.
 
Kuna watu wanapenda kutingisha kibiriti!
 
Nafikiri binti alikuwa na kwikwi hajielewi. Kama unahisi kumpenda bado basi mchunguze kwanza hapo kati kama alichepuka au la kisha usonge mbele. You will never know until you try.
 
Msamehe kwa kosa alilokufanyia la kuuvunjavunja moyo wako ila kama huna hisia nae mwambie hilo, huna hisia nae aendelee na maisha ila imemsamehe
 
"nilisafiri kwa siku kadhaa kwa viatu vya jirani.sikujua kama kiatu changu ni kizuri kiasi hiki.najuta kwanini niliacha kiatu changu." alienda kuangalia upepo huyo kakuta joto tupu.if your heart is already meng'emeng'e kubali tu but jua kuna jamaa kakumegea
 
huwa sielewagi watu kama nyie mtu alikwambia live kuwa hakupendi na akaamua kukuacha saizi anajirudi kukuomba msamaha mwanamme kuwa na msimamo usikuwa kupimwa akili mwambie staki na staki kuona ukinisumbua tena songa mbele tafuta hela kwa uchungu kuna siku mungu atakupa atakayetunza moyo wako na kuuhifadhi ukimkubalia anakuwa anakuona wewe zuzu na kuwa huwezi muacha na kuna siku utatukanwa ili upimwe akili maisha ya kupimana akili si maisha mbali ni kuumizana moyo
 
Usikilize moyo wako nini unataka, mie sitaki kuusemea. Lakini kaa ukijua calender siku zote huenda mbele.
 
Hakuna haja ya kumfanyia kisasi....mwache kwa amani tu endelea na maisha yako na kama unaikumbuka sms aliyokutumia wakati wa msiba wa kaka yako nawe mwandikie sms hyohyo.......tafuta mpz mpya uanze nae upya lakini si kumrudia ex
 
haya mambo ndo maana mi huwa siyapi percent kuubwa kiasi hicho.. kaka pole sana kwa matatizo...

mimi kuna mbebez mmoja tulizinguana hivyo hivyo majuzi tu hapa kama february hivi, basi katuma sms kanambia excel kuanzia leo mimi na wewe basi,... nikamuuliza are you serious? akasema for sure sikutaki, kisa tu tumekorofishana kwa jambo dogo tu..

ok, mi nikamwambia sawa, nikaendelea na mambo yangu, lakini namba yake sikuifuta, ikabaki tu kwenye phone memory,
sasa nimeshangaa mwishoni mwa mwezi wa tatu, nimepokea text yake.. baby I miss you!.. surely nikatabasam tu ila sikujibu text on time....

katuma tena nyingine, baby are you there?... basi na mimi nikaijibu baada ya masaa ma3 hiviiii!!

mwisho wa siku kajirudi, kaomba msamaha, ila sikumuacha bure!! nilimtukana sana tu japo si matusi ya nguoni.. nilimuonya sana kuhusu vitabia vya kutingisha kiberiti na kuleta swaga za kutishiana kumwagana...

actually mi sijawahi kupewa presha na mapenzi mapenzi haya, kupenda najua, ila ukizingua, nikakubembeleza mara moja ukagoma, mara ya pili nako ukatia ngumu, basi na mimi nakumwaga kama pishi tu la ubwabwa wa juzi....

mkuu, kwa jinsi ulivyosema huna love nae, no way..... take the other way! mwambie ushapata mashine gun nyingine..

mwambie kabisa kwamba wa sasa ana application nyingi kuliko yeye...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom