Naombeni ushauri nimemfumania shemeji yangu

Chukuwa ushauri huu.
 
Mmh usije ukawa chanzo cha ugomvi wao mkuu , ingekua mimi ningekausha tu.
Kabisa ni kuchuna tu,atakuja kujua mwenyewe ,
Nilimfumania mke wa bro live kabisa anapapaswa na njemba buguruni huko.
Nimeshuka kituoni pale sokoni kuna bar na lodge pembeni.
Nikaona ngoja nikapige supu humo,
Hamad shemu huyu hapa tena anapapaswa kabisa kakumbatiwa anachekacheka tu.
Aliponiona alishtuka sana,kama aje anisalimie,
Nilipita nikatokea mlango mwingine huyo nikatimka.
Nilishika cm km mara 3 nimpigie bro
Badae nikaona achana nao hao wameoana na wana mtoto mdogo.
Sikuwai kumwambia bro mpk anakufa.
Maana nae namjua,angembatua mtu leo yuko jela.
 
Kwahiyo bora kimya kimya eti eeeh?
 
Unajua ndgu zangu kuna namna mnazoeana na rafiki yako.
Ndio hapa wadau wengine wanasema mwambie wengine wanasema kausha iyo ni vile wao wanawachukilia rafiki zao wao na sio urafiki wako na jamaa.
Je kwenye upande wa mahusiano wewe na rafiki yako mko vipi??,Huwa mnashirikiana au ni kibiashara na mambo mengine tu??

Mzebaba akili kumkichwa mapenzi kushaurika huwa ni kazi sana hasa kwa mtu aliewekeza kama rafiki yako.
Mi ushauri wangu kwako ni kumwambia tu jamaa amchunguze mke wake basi , izo info nyingine atafute mwenyewe.

Ama lah kama vipi unaweza kuweka rehani urafiki wenu, ukimpasukia iyo ishu basi jua urafiki uko mashakani.
 
Kwa uandishi huu si ajabu ni ww maana umeandika kwa uchungu saana
Na huyo mke ni wako unashindwa ufanye nn
huna uwezo wa kuachana na huyo mwanamke japo evidence zipo za kutosha
 
Hiyo mwanamke sijui shemeji yako yuko desperate Sana alafu either ni Malaya au hana mapenzi na mskaji wako pia huyo mskaji wako naye zuzu anapenda kiboya lakini na wewe inaonekana unamtaka huyo demu ndio maana unamfuatilia so kikawaida ushauri wa mahusiano ya kimapenzi ni utata Cha msingi angalia wao wanamsimamo gani Kama wanafuraha na maisha yao achana nao utaonekana mnoko
 
Aisee ulifanya jambo la busara mkuu, japo inauma yaani unashuhudia Kaka yako akisalitiwa😪, ila sasa ukifikiria consequences baada ya kumwambia mmh, labda tu siku ungemchana huyo shemeji kwamba siku ile hukupenda alichokifanya na asirudie otherwise utamwambia Bro nadhani angeogopa na asingerudia.
 
Na je ukikaa kimya rafiki yako aje afe na ukimwi utakuwa umemsaidia?
 
Na je ukikaa kimya rafiki yako aje afe na ukimwi utakuwa umemsaidia?
Dah sawa ila labda umwambie indirectly amchunguze mkewe ila si kumwambia nimeona picha na videos mkeo anakusaliti, ama umface huyo mwanamke umwambie umeuona huo upuuzi anaoufanya na muoneshe na hizo picha then mchimbe mkwara kwamba unampelekea mumewe aone. Hapo ataogopa na atajirekebisha
 
Usiri ni chanzo cha maambukizi ya ukimwi , na unafiki ni dhambi na ni chanzo cha mauti
Ni kweli kabisa mkuu, ila sasa what if ukimwambia kwa hasira akamchoma mkewe na gunia 2 wewe utajisikiaje huku?

Mtengenezee mazingira afumanie mwenyewe, ila usimwambie directly
 
Yeah at least ufanye kitu kuliko kujifanya rafik afu unamficha rafik yako jambo kama hilo. Mimi kama mimi ningependa rafik yangu aniambie tu direct ntamthamin sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…