Naombeni ushauri, nikishalala na mwanamke napoteza mzuka naye

Sputnik_1

Member
Jul 16, 2018
47
60
Habari zenu.

Mie ni kijana wa kiume. Kama nilivyoandika ktk kichwa cha habari, ni kwamba nikimtongoza mwanamke akakubali, na kuwa mpenzi wangi, nikifanya nae ngono mara moja au mbili au tatu baada ya hapo nakua sina hamu nae kabisa. Naanza tafuta mpya nae nikifanya nae hivyo hivyo.

Na saa zingine naona siwatendei haki maana unakuta mdada katokea kunipenda sana na nampigisha shoo kali. Ila nina hii tabia nikisha fanya nae sex mara kadhaa namkinai kabisa.

Kuna muda naweza sema huyu ndiye mwanamke nitakayeenda ishi nae ila nikishapiga shoo tu, naanza kumkinai.

Mie ni mkimya na wanawake ninayekua nae kwa wakati huo wanatokea kunipenda sana. Sijawahi kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Ila udhaifu wangu ndio huu, nina hamu kuwa na mwanamke mmoja tu nije nimuoe ila ndio hivyo.

Ushauri, nafanyaje!
 
Habari zenu.

Mie ni kijana wa kiume. Kama nilivyoandika ktk kichwa cha habari, ni kwamba nikimtongoza mwanamke akakubali, na kuwa mpenzi wangi, nikifanya nae ngono mara moja au mbili au tatu baada ya hapo nakua sina hamu nae kabisa. Naanza tafuta mpya nae nikifanya nae hivyo hivyo.

Na saa zingine naona siwatendei haki maana unakuta mdada katokea kunipenda sana na nampigisha shoo kali. Ila nina hii tabia nikisha fanya nae sex mara kadhaa namkinai kabisa.

Kuna muda naweza sema huyu ndiye mwanamke nitakayeenda ishi nae ila nikishapiga shoo tu, naanza kumkinai.

Mie ni mkimya na wanawake ninayekua nae kwa wakati huo wanatokea kunipenda sana. Sijawahi kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Ila udhaifu wangu ndio huu, nina hamu kuwa na mwanamke mmoja tu nije nimuoe ila ndio hivyo. Ushauri, nafanyaje!
Wewe ushawahi kuona konda anawapigia debe abiria ambao wako ndan ya gari tayari??
 
Hilo tatizo linaitwa testorane propagation, yaani mbupu kujaa hewa. Nenda hospital kitengo cha RCH wakupime, kama una ilo tatizo utawekewa bleda
 
Unachukua madem low quality ambao hawajakiz vigezo vyako ndo maana after sex una wakinai tafuta pisi kaliiiiiiiiiii mjuba vepee
 
Back
Top Bottom