Naombeni ushauri nichague kozi ipi kati ya hizi?

Torquemada

JF-Expert Member
Oct 17, 2020
231
257
Habari humu.

Nipo njia panda , nahitaji Mawazo yenu kufanya maamuzi ya mwisho.

Ipo hivi nimechaguliwa UDSM ( BA in Psychology) na Tudarco ( LLB).

Kila MTU ana ndoto zake lakini pia siku hizi suala la kusoma ni maslahi.

Napenda sana sheria, preferably ningewish kusoma (UDSM & Mzumbe)

Bahati mbaya UDSM nimepata( BA in psychology) na Laws - Tudarco.

Je, una la kunishauri?

Karibuni sana ndugu.
 
Hv si anaweza fika chuo akabadilisha au
Kwa UDSM sijajua kama anaweza, ila mm mzumbe moro nakumbuka baadhi walihamia Llb nilikokuwa nasoma ila wachache hasa wale waliokidhi vigezo,ingekuwa mzumbe kidogo ningempa matumaini ila udsm sina uhakika
 
Kwa udsm sijajua kama anaweza,ila mm mzumbe moro nakumbuka baadhi walihamia Llb nilikokuwa nasoma ila wachache hasa wale waliokidhi vigezo,ingekuwa mzumbe kidogo ningempa matumaini ila udsm sina uhakika
Mimi namshauri awasiliane na udsm wampe information kama inawezekana au lah
 
Fata kile unachoona sahihi kwako Llb ya Udsm na Mzumbe imeshapeperuka sijui ufanyaje
Kuomba transfer nawaza nikitemwa mkuu?

Lakini Sheria ya udsm, mzumbe nk si ile ile tu ama kwenye ajira nitapa shida kutokana na jina la chuo?
 
Mkuu una ambition ya kusoma sheria nenda tu hata huko Tudarco, Mie naamini huko unaweza kuanza kama msingi tu, baadaye ukaja kujiendeleza huko Udsm au Mzumbe!

Kwenda kusoma Pyschology, huku roho inataka LLB, hutakuwa vizuri kisaikolojia! Kumbuka maslahi yako ya badaye yanategemea ni jinsi gani utatoka vizuri hapo na sio jina la chuo ulikosoma!

Hata hivyo mie sijasoma Tudarco, so mliosoma Tudarco mnaweza kuongezea hapa juu ya mazingira ya chuo na performance!
 
Mkuu una ambition ya kusoma sheria nenda tu hata huko Tudarco, Mie naamini huko unaweza kuanza kama msingi tu, baadaye ukaja kujiendeleza huko Udsm au Mzumbe!.
Ahsante sana mkuu!

Ni kweli passion yangu kuwa lawyer

Hofu ni jina la chuo tu.

Ulivyonushauri nimeona point hapo

Kwamba naweza kuanzia Tudarco bachelor then masters nikasoma udsm au mzumbe au hata nje kutegemea na matokeo yangu.
 
Ahsante sana mkuu!

Ni kweli passion yangu kuwa lawyer

Hofu ni jina la chuo tu.

Ulivyonushauri nimeona point hapo

Kwamba naweza kuanzia Tudarco bachelor then masters nikasoma udsm au mzumbe au hata nje kutegemea na matokeo yangu.
Kama unataka LLB kutoka moyoni nenda TURDACO. After all wote wa UDSM na TURDACO wakimaliza wanapitia Law School. Usiue ndoto yako kwa kuogopa jina la chuo. Wako vijana wengi wazuri tu wanasheria waliopitia hapo TURDACO. Tunaingia dakika za lala salama-amua.
 
Kama unataka LLB kutoka moyoni nenda TURDACO. After all wote wa UDSM na TURDACO wakimaliza wanapitia Law School. Usiue ndoto yako kwa kuogopa jina la chuo. Wako vijana wengi wazuri tu wanasheria waliopitia hapo TURDACO. Tunaingia dakika za lala salama-amua.
Ahsante sana mkuu Masiya

Unachosema kipo sahihi.

Nimepitia baadhi ya profile za Lawfirms kubwa

Nimeona kuna young lawyers from Udsm, mzumbe, Tumani, Sauti , Udom, Ruaha etc.

Nitafanya maamuzi mkuu!
 
Simponi and clear nenda udsm, ukifika pale unaama course unaenda pale school of law unaamia llb
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom