Naombeni ushauri ndugu zangu

wakwetu_tz

Senior Member
Feb 21, 2017
122
169
Kuna mwanamke nilimpa mimba alikuwa anafanya shughuli zake na anakaa kwake japo amepangisha. Mimba ilipofikisha miezi 6 akaniomba aje tuishi wote nikakubali, tuliishi wote mpaka alipojifungua.

Na kwakua mama yangu yupo arusha na mimi nipo moshi kikazi Nilimpa taarifa mama na mama alikuja kumchukua ili akamlee kwenye uzazi. Nikiwasiliana na mke wangu ananiambia wanaishi kwa furaha sana na mama, tunachat kila muda halipiti lisaa hatujawasiliana.

Nachoshangaa ghafla huyo mwanamke anataka kutoroka nyumbani eti aje tuishi wote. Na anachokisema eti amenimis sana na hazijapita hata wiki tatu tokea aende kwa mama.

Naombeni ushauri nifanyeje juu ya hili...
 
Kuna mwanamke nilimpa mimba alikuwa anafanya shughuli zake na anakaa kwake japo amepangisha.Mimba ilipofikisha miezi 6 akaniomba aje tuishi wote nikakubali,tuliishi wote mpaka alipojifungua.
Na kwakua mama yangu yupo arusha na mimi nipo moshi kikazi Nilimpa taarifa mama na mama alikuja kumchukua ili akamlee kwenye uzazi.
Nikiwasiliana na mke wangu ananiambia wanaishi kwa furaha sana na mama,tunachat kila muda halipiti lisaa hatujawasiliana.
Nachoshangaa ghafla huyo mwanamke anataka kutoroka nyumbani eti aje tuishi wote.Na anachokisema eti amenimis sana na hazijapita hata wiki tatu tokea aende kwa mama.

Naombeni ushauri nifanyeje juu ya hili...
Sawa ni haki yake kukimisi hata ingekuwa imepita siku mojaa kwani tatizo liko wapi??? Km nafasi inaruhusu kuwa nae karibu we kuwa nae
 
Nenda mpaka kituo kikuu cha mabasi pale town, wahi asubuhi panda mabasi yanayoelrkea mikoani via arusha ,
Ni kilomita 80 tu toka moshi mjini mpaka arusha muda ni masaa mawili tu ,

Msalimie shemeji ,mama ,wadogo zako na wengineo ,
Kisha jioni nenda hadi kwa sadala pale njia kuu kwea usafiri kurudi job,

Kama unapesa nyingi pia unaweza kupanda ndege hadi pale kisongo kisha panda boda boda mpaka home kwenu.
 
Wavulana huwa mna matatizo jamani,mwanzoni umesema ni mwanamke tu,mbeleni ushageuza kawa mke.

Sasa unaomba ushauri gani kwamba arudi au asirudi kwani sie ndio tunamhudumia? Huna hela mwambie avumilie au aende kwao
 
Kama huyo mke wangu atakuwa na mimi mpaka anajifungua mtoto na tutamlea pamoja nyumbani. Mambo ya kwenda kwao sijui kwetu hayo mambo ya kizamani. Mwanamke mwenye mimba mara nyingi hufanya kitu bila ya kukusudia, sasa akija mkwaza mama mkwe ndio ugomvi unapoanza na ndoa kuiona chungu.
 
Mmh hata hilo nalo unataka ushauri? mapenzi siku hizi hakuna, kila kitu mpaka kiletwe huku? kumpeleka huyo bint kwenu unaona ushatimiza wajibu wako. kijana gangamala ulee mwanao usipeleke mpira kwa wazazi wako
 
Kwani huyo mwanamke uliomuolea mama yako au ulioa kwa sababu yako mwenyewe? Usitake kumtesa mama yetu kukulelea mkeo ulijitutumua mwenyewe kuoa. Kila abiria afe na zigo lake! Fanya haraka kachukue mkeo ulee mwanao. Acha kutapatapa
 
Mtori umempatia joto, mwache akuje ana minyege huyo... Au nenda basi akikuona ataridhika jamani!!!!
 
Ulimuwahisha kwa mama mkwe wake ilibidi abaki kwa mda ili muendelee na mchezo wa kifamilia, kwa mama hakuna shida ila yy anamahitaji na ww, rekebisha antena yako
 
Back
Top Bottom