Naombeni ushauri, natafuta namna ya kujilipia masomo ya Ualimu

David Daudi

Member
May 8, 2019
23
9
Nimemaliza O-level 2013 na matokeo yakawa mazuri hadi kupelekea kuchaguliwa PCM Yalikuwa ni Math B+, BIO B, CHEM B, PHY D, HIST B, GEO B, CIV C, ENG C, LIT D, KISW B Ila advance nmetoka na SSE.

Mpaka naandika, nmekaa mtaani miaka 3. Nimejitahidi kahela kidogo natamani nisome hata ualimu, lakini je naweza pata ualimu wa secondari? au nifanyeje kwa kipato changu cha kuweza kujilipia laki 7 kwa mwaka?

Tafadhali jamani nisaidieni mawazo yenu.
 
Majina yako yanamaanisha UFALME

kwanini umewaza kusomea ualimu na sio kurudia pepa la Six ufight Mkopo ukasome Bach
Kiukweli kuna umri 30yrs,uoga wa pepa,wengine wanasema Pc hapati mkopo,bila tuition pcm naogopa,maisha yangu ni magum mno mpaka nkawaza ivyo
 
Diploma ya Elimu(Sekondari) huwezi kusoma kwasababu sifa ni Division I-III na kuanzia Principal Pass mbili hapo wewe una Principal moja.

Jaribu Diploma zingine zote wanadahili bila kuangalia Division ilmradi uwe na Principal moja pia Subsidiary moja.
 
Ingia kozi ya ufundi stadi itakayokuwezesha kujiajiri mwenyewe baada ya kumaliza masomo na kujikusanyia mtaji.

Haya masomo yanayokujenga fikra za kuja kuajiriwa yatakuchelewesha na kukutia fikra za utumwa wa ajira.

Rejea kigezo cha umri ulichosema umesogea
 
Diploma ya Elimu(Sekondari) huwezi kusoma kwasababu sifa ni Division I-III na kuanzia Principal Pass mbili hapo wewe una Principal moja.

Jaribu Diploma zingine zote wanadahili bila kuangalia Division ilmradi uwe na Principal moja pia Subsidiary moja.
Kama zipi ndugu yangu unazoona zinaweza kuniokoa angalau kwa hiki kipato changu
 
Kasome diploma ya Land and Mine Surveying pale chuo cha Madini Dodoma
Au
Diploma ya Geomatics pale chuo cha Ardhi Morogoro
 
Nimemaliza O-level 2013 na matokeo yakawa mazuri hadi kupelekea kuchaguliwa PCM Yalikuwa ni Math B+, BIO B, CHEM B, PHY D, HIST B, GEO B, CIV C, ENG C, LIT D, KISW B Ila advance nmetoka na SSE.

Mpaka naandika, nmekaa mtaani miaka 3. Nimejitahidi kahela kidogo natamani nisome hata ualimu, lakini je naweza pata ualimu wa secondari? au nifanyeje kwa kipato changu cha kuweza kujilipia laki 7 kwa mwaka?

Tafadhali jamani nisaidieni mawazo yenu.

Dogo nenda veta kasome electrical installation
Na ukitaka ualimu utaupata baada yakihitimu veta
Unaweza enda chuo cha ualimu wa veta ukasomea na kuwa mwl wa veta
 
Nimemaliza O-level 2013 na matokeo yakawa mazuri hadi kupelekea kuchaguliwa PCM Yalikuwa ni Math B+, BIO B, CHEM B, PHY D, HIST B, GEO B, CIV C, ENG C, LIT D, KISW B Ila advance nmetoka na SSE.

Mpaka naandika, nmekaa mtaani miaka 3. Nimejitahidi kahela kidogo natamani nisome hata ualimu, lakini je naweza pata ualimu wa secondari? au nifanyeje kwa kipato changu cha kuweza kujilipia laki 7 kwa mwaka?

Tafadhali jamani nisaidieni mawazo yenu.
Jaribu kuomba diploma ya ualimu miaka mitatu ambayo kiufupi inatolewa na vyuo vya ualimu mfano; korogwe ttc,mpwapwa ttc,songea ttc n.k

Sifa za kujiunga ni matokeo ya kidato cha nne ambapo unaweza kusoma half combination ya credit ulizopata mfano wewe umefaulu chemistry na math inafaa pia chemistry na biology inafaa.

Na uombaji wake ni kupitia tovute ya nacte.

N.B hata baadhi ya vyuo vya private wanatoa kozi hii, ila kwa vyuo vya serikali unasomeshwa na serikali.
 
Wengi wamekushauri bila kuzingatia hoja yako hapo juu..!Umesema huna uwezo wa kujilipia hiyo diploma ya ualimu.Mwingine akasema kwa matokeo yako ya kidato cha sita,huwezi kusoma ualimu.Yupo mwingine mmoja amekushauri jambo la mcngi sana la ku reseat mtihani wa kidato cha sita.Ushauri huo ni wa msingi sana kwa hali yako ya kiuchumi.Unaweza kutafuta kidogo kidogo ukapata pesa ya kulipia mitihani pamoja na kituo alafu ukawa unajikusanya taratibu ukasoma mtahani na tarehe ya mtihani ukapiga kawaida.Mungu akikujari ukapata principle pass mbili zinazohitajika uka join chuo kikuu na mkopo ukapata.Maana kwa sheria ya bodi ya mikopo umri ni mpaka miaka 33 unakuwa na sifa ya kupata mkopo,kwa vigezo vyao 2019/2020.Kusoma hakuna umri ndg yng,asikudanganye mtu.Hayo maswala ya umri umekwenda ni maneno kwa watu wasiyo na malengo.
 
Asante bro
 
Nimemaliza O-level 2013 na matokeo yakawa mazuri hadi kupelekea kuchaguliwa PCM Yalikuwa ni Math B+, BIO B, CHEM B, PHY D, HIST B, GEO B, CIV C, ENG C, LIT D, KISW B Ila advance nmetoka na SSE.

Mpaka naandika, nmekaa mtaani miaka 3. Nimejitahidi kahela kidogo natamani nisome hata ualimu, lakini je naweza pata ualimu wa secondari? au nifanyeje kwa kipato changu cha kuweza kujilipia laki 7 kwa mwaka?

Tafadhali jamani nisaidieni mawazo yenu.
Msaada wenu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom