Naombeni ushauri mpenzi wangu amepotea hewani

Naombeni ushauri mpenzi wangu amepotea hewani

Joined
Aug 27, 2013
Posts
26
Reaction score
11
Habari za majukumu wana-MMU.

Kwa ufupi nipo kwenye mahusiano na binti takribani miezi 5 sasa. Mwanzo mapenzi yalikua mazuri na tulipendana sana na nilijitahidi kutimiza kile alichohitaji kadri ya uwezo wangu. Japo kuna kipindi mawasiliano yalipungua kwake ikawa nisipo mtafuta mimi yeye hanitafuti hata tukikubaliana Jambo fulani yeye hatimizi mpaka ikafika kipindi tukawa na mgogoro. Ila nilijaribu kukaa naye chini na kuzungumza hatimaye tukawa sawa.

Sasa wiki iliyopita alikua hapatikani hewani takribani siku 3 mfululizo siku alipo nipigia tukaongea na kumuuliza akasema simu yake kioo kilivunjika na akawa ameniomba pesa ya matengenezo na kiukweli sikuwa nayo na ikumbukwe siku 4 nyuma kuna pesa nilikua nimempa kwa ajili ya kujikimu mahitaji yake madogo madogo.

Mpaka naandika hapa sasa ni zaidi ya wiki sina mawasiliano naye ikiwa na maana simu yake haipo hewani mpaka leo hadi nashindwa kuelewa maana hata alipokua anakaa aliondoka Kwa muda akaenda Kwa shangazi yake ili nilikua nalijua. Hivi ina maana mpaka leo simu yake haijatengemaa? Na inawezekana Kwa mtu unayempenda kukaa bila mawasiliano Kwa zaidi ya wiki kweli?

Hapa hata sielewi maana hata marafiki zake hawana mawasiliano naye kwa muda. Hivi kuna mapenzi kweli hapa? Maana sijui Hali yake na nini kimemsibu mbali na tatizo la simu.

Naombeni ushauri wenu wadau. Asante
 
unataka mpaka Yesu aje akwambie hutakiwi ndo uelewe ?

tambua kama hana muda na wewe ujuwe kuna mtu ana muda nae

labda kafungua tawi jipya kwa shangazi
 
Wewe Huyo achana nae haraka sana, ati Siku 4 bila mawasiliano? Kwani huko kwa Shangazi yake aliko nenda cha wana simu aazime akujulishe kinachoendelea?

Yupo kwa Shangazi yake ( Mme mwenzio), shenzi zake asizibie wenzie nafasi, embu Fanya kumpigia ireen yule ulomwombaga no, lakini roho ulikuwa inakusuta kumsalit mpenzi wako.

Trust me mpenzi wako yupo kwa mpenzi wake.
 
Back
Top Bottom