Naombeni Ushauri: Mke amenishtaki kuwa nimempiga

kibhojela

JF-Expert Member
Mar 7, 2018
1,004
1,094
Siku chache zilizopita tuligombana na wife wote tuliumia, lakini baadaye akaenda police kunishtaki kuwa nimempiga na jalada lipo Polisi.

Naombeni ushauri kukiepuka kikombe hiki.

Baada ya kugombana Mimi ndo nilimtibu na baadae wazazi wangu wakaja kumchukua ili atulie kidogo lakini akatoroka hom na kwenda kwao ndo karudi kisirisiri kukisanua, alitaka kunipoga shoka ndipo nikamtime nakumlaza kwa mtama.

Nilipigwa na ubao kichwani nikiwa nimetulia nachat kwenye simu. nilishonwa.

====

MREJESHO:

=====

Nilienda Jumatatu kujisalimisha kituo cha polisi na wife kumbe alikuwa kapangwa na ndugu ili kunikomoa ili wanifunge.

Lakini nilimbembeleza kwa muda mrefu afute lile shauri na badaye akalifuta na akasepa kwenda kwao akidai hawezi kurudi Nyumbani kwani anaona aibu kwa kumshitaki mume.

Nikamtakia maisha mema.

AHSANTENI KWA USHAURI WENU
 
Back
Top Bottom