Naombeni ushauri kwa mtoto anayesumbua kula!!

Naombeni ushauri kwa mtoto anayesumbua kula!!

Angekua mdogo ningekupa shortcut ila sasa naona kama haitasaidia

Mpe uji tunisha tumbo
Atapata njaa za mara kwa mara
Ila sasa umri huo ukimuanziashia uji hatataka
Ila mimi mwanangu wa la pili mpaka leo anakunywa uji maana najua faida moja wapo ni kutanua tumbo ili ale
Vinginevyo sijui ingekuaje maana anachagua chakula ila akipata kiepe yai anapiga sahan nzima
 
Wakuu nina mtoto wangu wa kiume ana miaka 9 lakini anasumbua kula sana.

Tunajitahidi kumpa kila anachotakiwa kula lakini wapi, ujanja wote wa kumbadilishia chakula umegonga mwamba!!

Nilidhani labda kwakua anasoma shule basi atachangamkia kula lakini hamna kitu.

Yupo darasa la 3 na shule anafanya vizuri tu changamoto ya kula ndo shida chakula kama ni ugali atakula matonge machache tu

Yaani anashindwa hata na mwingine mdogo wa miaka 4!

Mimi na wife tumepambana lakini wapi.

Naombeni mnishauri nifanyeje maana hata lishe tumenunua lakini hatujaona matokeo na huko shuleni kwao wanapikiwa lakini bado shuleni huwa anaskip muda wa kula.

Mpaka kuna mda natamani hata labda ningemuhamishia shule za serikali labda ingesaidia...Wenye watoto kama huyu wangu mmetumia mbinu gani?
Ana kilo ngapi ?

Ratiba yake ya shule ikoje anaenda muda gani anarudi muda gani ?

Je akiwa nyumbani kabla ya mlo mkubwa huwa mnampa kitu gani cha kutafunatafuna ?

Je mnakula milo mingapi kwa siku hapo nyumbani ?
 
Sana sana uwe unampatia vyakula vitamu! Halafu jua chakula anachopenda sana! Awe anapikiwa mara kwa mara! Mimi mwenyewe nilikuwa na tatizo la kutokula nilikuwa mwembamba mno hata sasa sio mnene! Hali huto ilifanya wazazi wasiwe wanasafiri na mimi! Mara nyingi wao na ndg zangu walisafiri likizo lin nlibaki nyumbani! Baadae waligundua chakula nlichokuwa nakipenda “wali maharage na ndizi mbivu” nlikuwa napikiwa daily! Hat boarding nlivyofaulu form one! Sikupelekwa nlisoma day! Mimi hiyo hali iliisha nlivyoenda boarding A level! Hats sasa nakula vizuri Ila msosi sio kitu cha kunibabaisha! Siwezi kukaa kwny sherehe eto nasubir msosi
 
Eti siwezi kukaa kwenye sherehe kusubiri msosi😄😄😄
 
Ngoja nimcheki Dr. Janabi ataniambia kati yako wewe unaekula mara 3 kwa siku na mwanao anaekula mara 1 nani ni tatizo.
Ukimuuliza Dr Janabi atakwambia huyo mtoto ndiye mwenye Afya nyingi kuliko mzazi wake anayekula mara 3,very confusing.
 
Fanya yote ila asije kukudanganya mtu yoyote eti anakutafutia dawa hizi za mitishamba ili mtoto apende kula,, ndio zinafanya kazi ila atakuwa mroho kama nguruwe
 
Wakuu nina mtoto wangu wa kiume ana miaka 9 lakini anasumbua kula sana.

Tunajitahidi kumpa kila anachotakiwa kula lakini wapi, ujanja wote wa kumbadilishia chakula umegonga mwamba!!

Nilidhani labda kwakua anasoma shule basi atachangamkia kula lakini hamna kitu.

Yupo darasa la 3 na shule anafanya vizuri tu changamoto ya kula ndo shida chakula kama ni ugali atakula matonge machache tu

Yaani anashindwa hata na mwingine mdogo wa miaka 4!

Mimi na wife tumepambana lakini wapi.

Naombeni mnishauri nifanyeje maana hata lishe tumenunua lakini hatujaona matokeo na huko shuleni kwao wanapikiwa lakini bado shuleni huwa anaskip muda wa kula.

Mpaka kuna mda natamani hata labda ningemuhamishia shule za serikali labda ingesaidia...Wenye watoto kama huyu wangu mmetumia mbinu gani?
Naomba nikusaidie, wala usiumize kichwa…. Kwa maelezo yako hiyo ni behavior ya huyo mtoto kwa kuwa umeshajaribu mbinu zote ikiwemo na kwenda Hospital kuchekiwa na kupewa hizo mebendazole na multivitamins…… so do not stress up

Hiyo ni character ya mtoto yaani Compatiment…. Anavyozid kukua atabadilika na atapenda kula
 
Hivi ni vidonge vya mafuta ya samaki lakini mbali na vidonge pia kuna mafuta ya samaki ambapo yanauzwa kwenye maduka ya dawa yana matokeo kwa asilimia mia
Vidonge vinarange kuanzia 120-160 gharama
Lakini mwanangu mimi nilimnunulia mafuta kwa elfu32
Utaulizia mafuta ya omega3
SISHAURI. Supplements are not so good as you might think.. the 9 old boy doe not need any of those

Let him get naturally….. as he grows atakuwa sawa
 
Back
Top Bottom