Naombeni ushauri kuhusu combination ya CBG

Chukua ushauri wa manager wa makapuni.

Sikujiui hunijui ila nakushauri nenda karipot shuleni ukifika badilisha combination soma PCB, ukimaliza utasoma kozi zote za afya utajichagulia mwenyewe.

CBG utakuja kulia lia tena kuwa ukasome nn chuoni mambo yamebadilika zamani walikuwa wanasoma hadi MD, ila saiv in Environmental health, Medical lab in molecular biology and technology
 
Unaweza fanya reference apo dogo
Hii ni 2020 ya ndalichako sio JK ambapo HKL, EGM walikuwa wanasoma MD
 
Hongera kwa kozi uliyochaguliwa, kifupi kama una mawazo ya kusoma kozi za ajira na ndo unaenda kidato cha tano basi mwisho wako utakuwa mbaya sana, ni vyema uhailishe kusoma kwanza ujitafakari,

Binafsi nimesoma CBG Karatu Boys pale baada ya matokeo kutoka nilishauriwa sana kusoma diploma ya afya maana tofauti na hapo yabidi niombe ualimu wa kemia na biology, niliamua mwenyewe kuomba kozi ya IT, nikafanikiwa kujiunga mzumbe university na mkopo wa bodi 100%, juhudi zangu zimeniwezesha niko mwaka wa tatu na hivi sasa napata deal za kutengeneza mifumo( tupo kundi), nasoma na bado napata connection, nakumbuka mzee baada ya kusikia nimechagua kusoma IT wakati ukoo wetu wote wakisoma basi ni kozi za afya, uhandisi na ualimu, alinigomea mwanzo kunipa sapoti, but mkopo niloupata umenisaidia kwa kiasi fulani mpaka akaja kuelewa,

Soma mkuu, fanya vyema, fursa zipo nyingi, kazi sio tu kwenye fani za afya, dunia imebadilika
 
Absolutely, Advance ni kama kubet vile.
 
Shukran sana
 
Wanasemaga ni combination of beautiful girls aka cabbage
 
Kwaiyo wataka kusema CBG asomi nursing?? Una uwakika na hilo au ndo unasema tuu
 
Acha kumdanganya dogo ,nani kakwambia alichukua CBG lazima aje kusomea unesi,akifauli vzr CBG anaweza kuja ku-opt kozi tofauti chuobi kama vile bachelor ya laboratory technology,Environmental science(EE), Environmental science Management(ESM) ,Bsc Pharmacy,na baadhi ya kozi nyingiz za kilimo SUA .ambazo ni very markertable
 
CBG hana vigezo vya kujiunga BSc Health Laboratory ile ya kupima wagonjwa hospitalini pia hana vigezo vya kujiunga BSc Pharmacy.

Ili ujiunge na hizo shahada mbili lazima uwe na pass ya PHYSICS, CHEMISTRY na BIOLOGY kwenye mtihani wa A Level.

Lakini pia hiyo nursing anajiunga kwa tochi.

Reference
Soma TCU Undergraduate Admission Guide Book 2020/2021 ukarasa wa 11 na 12.

Kwaiyo wataka kusema CBG asomi nursing?? Una uwakika na hilo au ndo unasema tuu
CBG hana vigezo vya kujiunga BSc Health Laboratory ile ya kupima wagonjwa hospitalini pia hana vigezo vya kujiunga BSc Pharmacy.

Ili ujiunge na hizo shahada mbili lazima uwe na pass ya PHYSICS, CHEMISTRY na BIOLOGY kwenye mtihani wa A Level.

Lakini pia hiyo nursing anajiunga kwa tochi.

Reference
Soma TCU Undergraduate Admission Guide Book 2020/2021 ukarasa wa 11 na 12.

Mkuu wakati unachagua combination hukufanya maamuzi sahihi.

Yanini kusoma biology, geography na chemistry advance alafu unatwambia uliamua kwenda kusomea IT kweli.

Sasa maarifa ya organic chemistry, inorganic chemistry, cytology, physical geography, Nutrition, Coordination, kupasua simbilisi na vyura unayatumia huko kwenye IT?

Yanini kujisumbua na ma BABA SALOME (BS) BIOLOGICAL SCIENCE advance. Mkuu ulikosea.

Mimi nadhani labda ungesema nilienda PCM au EGM au PGM hapo kwenye IT ningekusifu.

hayo ni makosa makubwa sana.

Tuache kumpa moyo huyu dogo. Mimi kwa ushauri wangu akasome kile anacho kipenda mapema kabisa. Lasivyo anatafuta stress zisizoisha maishani mwake.
 
HUu ni uongo!! CBG anasoma course kibao za afya ikiwemo na Nursing but some of courses hawezi kusoma kama Medical doctor na zingine hazizidi 4 hv.
So usimkatishe tamaa kabisa
Tatizo lako wewe mkuu ni moja tu. Utakua umesoma UDOM hivyo ni kilaza wa kwanza.
Angalia hii image, usilazimishe CBG sio comb ya kusoma kwa sasa haina tofauti na HKL.
 
Mbona entry requirements inajieleza apo au English in shida,,Soma maelezo ya Medical doctor na Nursing kama ujaona tofauti basi huna hoja aisee
Tatizo lako wewe mkuu ni moja tu. Utakua umesoma UDOM hivyo ni kilaza wa kwanza.
Angalia hii image, usilazimishe CBG sio comb ya kusoma kwa sasa haina tofauti na HKL. View attachment 1516504View attachment 1516504
We umesoma wapi mpaka unaponda vyuo vya watu!!
 
Mbona entry requirements inajieleza apo au English in shida,,Soma maelezo ya Medical doctor na Nursing kama ujaona tofauti basi huna hoja aisee

We umesoma wapi mpaka unaponda vyuo vya watu!!
Mimi nimesoma Mlimani mkuu chuo kinacho chukua wanafunzi walio fauru sana
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…