Naombeni ushauri jinsi ya kujihadhari nisiuziwe gari la wizi

inspectorbenja

JF-Expert Member
Oct 14, 2012
500
420
Habari wana jf.Nimekuwa nikipita pita kupatana.Unakutana na gari linaonekana lipo order sana,ila bei yake ni ndogo sana.Kuna muda huwa napata mashaka huenda gari hizo zimeibiwa.
Naombeni ushauri je naweza kujihadhari vipi,endapo gari kweli ni zima ila labda lina simtofahamu ili nisije kuingia kwenye migogoro nq vyombo vya sheria.
 
Mkuu, anything cheap is expensive.
Plus Kupatana ni App ina matapeli wengi sana, mimi na mshkaji wangu tukiwa wahanga.

Kama utanunua gari kule just be extra careful otherwise kama una sources zingine za kupata gari achana nayo hiyo App.

Namaste
 
Habari wana jf.Nimekuwa nikipita pita kupatana.Unakutana na gari linaonekana lipo order sana,ila bei yake ni ndogo sana.Kuna muda huwa napata mashaka huenda gari hizo zimeibiwa.
Naombeni ushauri je naweza kujihadhari vipi,endapo gari kweli ni zima ila labda lina simtofahamu ili nisije kuingia kwenye migogoro nq vyombo vya sheria.
Matapeli wamejaa huko. Kuna mtu aliwahi kupost gari huko anauza bei nafuu sana. Walisema gari iko Tabora. Hapo wanawasiliana na dada yangu. Alipomtuma mtu mwingine (mwanaume) akalikague, na kuwaambia katuma mtu, hawakupokea tena simu.
 
Kupatana Sehemu ya kipumbavu Sana yaani kuwa Makini sana ishaniweka Siku 10 ndani kwa ajili ya Vitu Used hivi.

Naona insta ni sehemu sahihi sana kwa ajili ya kupata Gari nzuri hasa Mfatilie jamaa anaitwa Jacktan_Safari huyu huwa anakuunga na mwenye Mali directly sijawahi fanya nae biashara ila naona jamaa hana Tamaa.
 
Mkuu wewe nunua usiogope chochote.
Kubwa ukipenda gari hakikisha unalicheki TRA
1. Hakiki majina matatu kwa kutumia number za gari je zinafanana na kadi ya gari
2. Hakiki hayo majina yanafanana na kitambulisho mtu aliekuzia.
3. Hakiki kama halina madeni na sio exempted
4. Mkataba wa mauziano mpe mtu hela yake walausiogope beba gari lako.
5. Hakikisha unafundi wako ahakikishe kila kitu kiko sawa kwa test drive.

Usisahau picha passport size na id copy kwa ajili ya kufanya transfer na akupe file la gari

Note: Usinunue gari kwamtu ambae sio mmiliki yaani unaona tofauti kuanzia kitambulisho cha mmiliki na kadi majina hayafanani au kwenye mfumo wa Tra na Id ya mmiliki hayafanani.

Lamwisho kuwa makini na madalali wa Kinondoni na Sinza kwa magari ya mkononi wazee wa kula bata hawachelwi kubaki na funguo au kutoa vitu mkikubaliana kuuziana wakati wewe unaenda kutoa hela
 
Asante sana kwa kunipa mwanga,vipi kama gari imepita mikono ya zaidi ya mtu mmoja na haijabadilishiwa jina na ikanifikia mm.Hapo nafanyaje
 
Kupatana Sehemu ya kipumbavu Sana yaani kuwa Makini sana ishaniweka Siku 10 ndani kwa ajili ya Vitu Used hivi.

Naona insta ni sehemu sahihi sana kwa ajili ya kupata Gari nzuri hasa Mfatilie jamaa anaitwa Jacktan_Safari huyu huwa anakuunga na mwenye Mali directly sijawahi fanya nae biashara ila naona jamaa hana Tamaa.
Kaka ulipatwa na nn.Hebu share
 
Asante sana kwa kunipa mwanga,vipi kama gari imepita mikono ya zaidi ya mtu mmoja na haijabadilishiwa jina na ikanifikia mm.Hapo nafanyaje
Achana nayo hapa unaweza kuuziwa gari yenye matatizo.

1. Gari la urithi
2. Gari ya familia
3. Gari ya wizi

Yaani utauziwa gari ambalo halijaidhinishwa kuuzwa na muhusika au msimamizi.
 
Shida kubwa ni ubovu wa magari ya mkononi...ukinunua lazima ununue na toolbox
Sio lazima gari ya mkononi iwe mbovu maana hata za japan ni 2nd hand.
Kwa mtazamo wangu gari ambayo sio mpya yaani 0km ni muhimu ukajua service history yake ili kama ilishapata majanga au kuna vitu vilibadilishwa uwe unajua kabisa unadeal na kitu gani.
Mi binafsi kuna watu utunzaji wao wa magari akisema anauza nanunua kwasababu hizo gari nakuwa nazifahamu historia zake kwa kiasi na pia naweza nikajua sababu halisi ya ye kuiuza kwa urahisi.
Kipengele kinakuja kwenye gari ya dalali yeye ndo kwanza atajitahidi kuficha usijue hiyo gari ilipitia nini kwahiyo ni rahisi kuuziwa gari "mbuche".
 
Sikuhizi watu hawauzi magari ya wizi hakuna kitu kama hicho.... gari ikiibiwa inaenda kukatwa vipande na kila chombo kitauzwa separately.
Kuna yard za magari nazijua hata Kwa majina wanauza magari yaliyotumika hapa bongo ambayo ni kuanzia namba T.....DU Hadi DZ haya magari yanabadilishwa kila kibovu na yanashushwa milage ambapo mteja atanunua kama limetumika Japan...ukiwa na gari namba D imesimama na haikupata ajali unaweza kuwauzia watu wa yard bila shida
 
Mkataba wa makubaliano kati ya mmiliki wa gari ( aliyeandikwa kwenye card), saini zenu wawili na kiambata cha NIDA yake ili ufananishe card ya gari, Pesa muwekee kwenye account yenye jina lake.

Kwahiyo jina la kadi ya gari, NIDA , na Account number viwe sawa biashara itakuwa imeisha salama sana.
 
Sikuhizi watu hawauzi magari ya wizi hakuna kitu kama hicho.... gari ikiibiwa inaenda kukatwa vipande na kila chombo kitauzwa separately.
Kuna yard za magari nazijua hata Kwa majina wanauza magari yaliyotumika hapa bongo ambayo ni kuanzia namba T.....DU Hadi DZ haya magari yanabadilishwa kila kibovu na yanashushwa milage ambapo mteja atanunua kama limetumika Japan...ukiwa na gari namba D imesimama na haikupata ajali unaweza kuwauzia watu wa yard bila shida
Kama ni Yard inamaana kadi ya gari isome jina la kampuni na details za chasis, engine, na mfg zifanane na chombo na upewe efd receipt baada ya malipo hapo utakuwa salama hata kama umenunua kinondoni manyanya
 
KWA MAELEZO MLIYO TOA HUYU HAWEZI KUNUNUA GARI LA BONGO ETI JINA LA KWENYE KADI LIFANANE NA KITAMBULISHO CHA ANAE KUUZIA SASA GARI LIMEPITA KWA WATU KUMI KATIKA KUUZIANA NA YULE MMILIKI WA KWANZA ALIKUFA INAKUWAJE HAPO

USHAURI WA KIBONGO UKIUSIKILIZA SANA HUWEZI KUNUNUA GARI YA MKONONI MWA MTU

MIMI NADHANI USHAURI MZURI NI MAANDIKISHANO KWA MWANA SHERIA NA PESA UMTUMIE HUYO ANAE KUUZIA KWENYE ACCOUNT YAKE USIMPE KESHI

ILA MKIANZA KUSEMA ETI JINA LA KWENYE KADI LIENDANE NA JINA LA KITAMBULISHO CHA ANAE KUUZIA MBONA BIASHARA ITAKUWA NGUMU BASI MIMI NISINGEUZA LILE GARI LANGU
 
Habari wana jf.Nimekuwa nikipita pita kupatana.Unakutana na gari linaonekana lipo order sana,ila bei yake ni ndogo sana.Kuna muda huwa napata mashaka huenda gari hizo zimeibiwa.
Naombeni ushauri je naweza kujihadhari vipi,endapo gari kweli ni zima ila labda lina simtofahamu ili nisije kuingia kwenye migogoro nq vyombo vya sheria.
Nakumbuka mama yangu alinunua huko kupatana yaani ilo gari lilkuwa kichomi, nikushauri kama unataka gari jichange uagize gari kulingana na pesa yako, ukipata gari mpya yaani utafurahi sana kulipokea pale bandarini yaani full burudani
 
Back
Top Bottom