Naombeni ushauri haraka sana!

jitombashisho

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
667
2,242
Nina mke na watoto wawili mmoja ni kichanga wa miezi 3.

Sasa basi,ipo changamoto inayonikabili kwa mimi na mwenza wangu mara zote kila niwapo katika kubangaiza kwangu kwa ajili ya kupata chochote kwa ajili ya kujikimu huwa napokea meseji zake za matusi, kashfa na za kunidhalilisha mno na hasa kwa mambo ambayo kwayo si ya kweli!

Muda mwingi huwa sijibu upuuzi wake lakini kwa meseji hii ya sasa ya kunitukania mama yangu kwakweli nipo kwenye daladala imenifanya nifule zaidi ya nyati! Endapo nikifika nyumbani sioni namna ya yeye kuponyoka katika mikono yangu.

Tafadhari naomba mnipe ushauri nimfanyeje huyo kiumbe!?

Mbaya zaidi nimetoka kuhangaika kushusha mashudu yenye zaidi ya kilo 100 kila gunia na ujira ni Tsh 250 kwa kila moja na nkmechoka na natukaniwa mama yangu!

Nakaribia kushuka kituoni.....

Nisilaumiwe!
 
Oooohoooooo...
Mkuu hembu simama kwanza hapo kituoni...
Kunywa maji subiri dk ngapi niite watu humu..
 
Kukutukana ni kosa hiyo ni dharau na kutotii.

Ila mkuu umefanyaje? Au kakurupuka tu kaanza kuporomosha matusi?

Kwa kuwa massage unazo embu mpeleke likizo kwao kwanza, ajirafakari kama anaihitaji ndoa ama laaah. Kwao watamkanya vizuri labda hakufundwa vyema.
 
Huyo mkeo anawivu sana/inaonekana anakupenda sana ILA hana kitu cha kumfanya awe bize; Unaonaje ukamfungulia hata genge dogo awe anauza? hiyo itakusaidia kupunguza au pengine kumaliza hayo matatizo
Kwa leo naomba usimpige ILA panga muda hata wikiendi akiwa na furaha muongee; muulize kwa nini anafanya hivyo na anafikiriaje kama wewe umemtumia hiyo meseji angejisikiaje? Nani anampa hayo maneno ya chuki pengine ni shoga zake wasio kuwa na nia njema na mahusiano yenu
Jitahidi kuongelea mipango ya maendeleo yenu kwa kadri ya uwezo wenu ILI aone kwamba kuna mambo mengi yanaendelea sio mapenzi tuuu
 
Huko si ndo wenyewe mnakuita romantic na ukisasa.
Maumivu ya kichwa huanza taratibu,kwanini hukutumia panadol mapema mpaka maumivu yamezidi?
 
Kina sababu ya yeye kukutukana si bure..ingawa mwanamke mwenzangu amekosea kukutukana
Mengine mtajuana wenyewe
 
Nakupa option chagua moja
1.mtukanie mama yake nayy ili hata akikushtaki popote naww unapata sababu
2. Jifanye kama hujaona SMS yake wala nini fika home endelea na mambo yako yanayokuhusu amka kesho asubuh Achana hela ya matumizi sepa kwenye mizunguko yako usimuulize wala usipige nae story Fanya yako tu
3.mrudishe kwao akajifunze pengne hakufundwa vzr
4. Samehe saba Mara 70 kwa siku moja maisha yaendelee hawa viumbe wakati fulan ili uishi nao unatakiwa mambo mengne ujifanye kama huyaoni wala hayakuhusu atakaa sawa tu huku ukizidi kumuombea
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom